MAMA ALISHIKWA KALIO MBELE YANGU (34) Jina: MAMA ALISHIKWA KALIO MBELE YANGU Mtunzi: Omary John Mndambi SEHEMU YA THERATHINI NA NNE TULIPOISHIA... Aliuliza tena lakini badala ya majibu Verity alionekana akidondosha tu machozi. Gwakisa alichofanya alimnyanyua mkewe na kumuingiza chumbani, kule alimlaza kitandani kwani alikuwa hana nguvu kabisa hata za kusimama. IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI 👉INSTALL👈 TUENDELEE... “Umekula?” Verity alitingisha kichwa kuashiriaa hajala, yaani toka jana yake alikuwa hajatia kitu mdomoni, Gwakisa alielekea kwenye friji akakuta kuna maziwa, aliyapasha moto kisha akampa mkewe anywe kwa kumnywesha. Alipomaliza alimlaza tena kitandani apumzike, Gwakisa alikuwa kaka pembeni yake tu anamuangalia, alikuwa akitafakari mambo mengi sana yaliyokuwa yanampa huzuni. Japo alipanga alipe kisasi kwa mke wake kwa kuzaa na mtu mwingine lakini alijikuta tu akimuonea huruma kwa kuwa pia aliamini ile mimba iliingia akiwa hajamuoa bado japo tu hakuambiwa ukweli. Baada ya muda kid…