MAMA ALISHIKWA KALIO MBELE YANGU (48) Jina: MAMA ALISHIKWA KALIO MBELE YANGU Mtunzi: Omary John Mndambi SEHEMU YA AROBAINI NA NANE TULIPOISHIA... “Hakuna shida, naenda kuridhia ombi la kuachana nae” alijisemea Gwakisa . Alichokifanya ni kupanga ninini amuache nacho Verity , yaani ampe nini kwenye mali zao, aliandika mali zao zote pamoja na zile alizochuma katika ushirika wake na Nisha kisha akaamua cha kumpa ili waachane. IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI 👉INSTALL👈 TUENDELEE... Kwa upande wa Verity aliamka akiwa mchovu sana, aliangalia pembeni na kugundua kuwa mme wake ameshaondoka kwani hakuwepo pale. Machozi yalimtoka usoni kwa jinsi ambavyo maisha yamemgeukia vibaya, aliiwaza aibu inayomuwinda mbele ya jamii. Alikuwa anasubiria jibu kutoka Kwa Gwakisa lakini alitamani ampigie simu amuambie kama vipi apuuzie ombi alilompa. Baada ya kuona anakosa jibu jawabu la mawazo yake alitamani kupata mtu wa kumshirikisha kuhusu lile jambo na hakuona mwingine isipokuwa dada yake. Alijiandaa haraka hara…