Mtunzi: Omary John Mndambi
SEHEMU YA HAMSINI NA MOJA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Katika kulisimamia hili aliamua kujiweka bize sana na kazi zake za ofisini pamoja na miradi mbali mbali, swala la starehe aliliweka kando akawa ni mtu wa sala kila wakati.
Pamoja na hayo maamuzi yake lakini kupendeza kwake na muonekano alioupata akiwa kama binti ambaye hajawahi hata kuzaa mbele ya macho ya watu ikawa ni mtihani.
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
TUENDELEE...
Wanaume wengi walimtaka sana kimapenzi.
Kuna wakati aliona kero na kutamani hata kutotoka nje ili asikutane na wanaume wasumbufu lakini isingewezekana, kazi na miradi yake ilikuwa ni lazima atoke nje akaisimamie.
Kwakuwa alikuwa na oda ya kupeleka kuku wa Nyama kwenye mahoteli mengi akawa anakutana na aina tofauti ya watu wakiwemo wanaume wakwere.
Siku moja akiwa kwenye kazi zake akiwa anatoka kuonana na mteja wake ambaye alikuwa anamdai fedha hapo hapo akakutana na mteja mwingine.
“Samahani dada yangu”
“Bila samahani”
“Nadhai wewe unasambaza kuku wa Nyama kwa Oda?”
“Ndio Kaka, vipi unataka unipe tenda?” Verity aliuliza hivyo huku akiondoa kunyanzi zilizokuwa usoni kwani alipokuwa anaitwa na wanaume huwa anajiuliza mara mbili mbili kuwa kuna kati ya kutongozwa ama biashara.
“Sasa naomba tuonane Kesho ili tuongee vizuri”
“Oooh Kaka yangu mambo mazuri kama hayo yasisubiri kesho, kama ni kazi naomba tuongee leoleo nikikuacha hapa unaweza ukaghairi, ”
Yule mwanaume alipomuona Verity anavyoongea kwa unyenyekevu ukichanganya na muonekano wake akajikuta ameduwaa huku akikubaliana nae kufanya maongezi siku hiyo hiyo.
“Basi tutafute sehemu nzuri tukakae”
“Sawa haina shida”
Kwakuwa Yule Bwana alikuja na Gari ilibidi amwambie Verity waingie kwenye gari yake alafu yeye Verity apaki pale ataichukua akirudi baada ya maongezi. Safari ilianza huku Yule bwana akiwa ndie mwendeshaji kisha kimya kidogo kikatawala ndani ya gari.
“Ila sijakufahamu jina, by the way mimi naitwa Verity”
“Oh mimi naitwa Mr Sanga”
Hatimaye walishuka kwenye hoteli moja ambayo Verity aliijua fika kuwa inamilikiwa na aliyekuwa mume wake yaani Gwakisa.
Walitafuta sehemu nzuri ya kukaa kisha maongezi yao yakaanza.
“Unajua dada yangu mimi nina tenda ya kusambaza KUKU wa nyama kwenye Kambi ya Jeshi JKT hapa mjini Ila nimepata nyingine Kule chuo cha askari magereza ”
“Oh honngera sana, tenda kubwa sana hizo”
“Nikweli ila kwasasa nimezidiwa mwenyewe sitaweza na ninaogopa kuwaangusha watu walioniamini lakini pia sittaki waone sina uwezo wa kuhudumia”
“Enhee”
“Naomba kama una uwezo tuunganishe nguvu”
Kwa Verity hii ikawa habari nzuri sana, japo idadi ya kuku waliokuwa wanahitajika ni kubwa mno kwani ilikuwa kwa wiki mara tatu wanachuo wa magereza wanakula Kuku hivyo kuku zaidi ya elfu moja wanatakiwa mara tatu kwa wiki.
Yaani hapo kila mmoja anatakiwa apeleke idadi ya kuku wasiopungua 1500 kwa wiki. Verity aliifurahia tenda hii lakini ilimuumiza kichwa kwani alitakiwa kupanua sana mradi wake angalau awe na kuku wa kufuga wasiopungua elfu kumi.
Hapo hapo wazo la kufungua mabanda zaidi likachipuka huku akifikiri kuajiri watu wengi zaidi. Waliandikishana mkataba pale kila mmoja akabaki na nakala kisha wakakumbatiana ishara ya kufurahia makubaliano.
Wakati wakiwa wanakumbatiana Gwakisa nae alikuwa anaingia pale hotelini, kabla hajaketi alipigwa na butwaa kuona mwanadada aliyevaa gauni fupi jeusi anakumbatina na mwanaume huku kigauni kikipanda kidogo na kuacha sehemu za nyuma ya miguu kuwa wazi kidogo na za kuvutia sababu ya kunyanyua mikono.
Gwakisa alibaki ametumbua macho akisubiri mwanamke huyo ageuke ili amjue ni nani kwani alikuwa amemchanganya akili.
Alijikuta mdomo wake ukiwa wazi baada ya kuonana uso kwa uso na Verity, Verity nae alishangaa lakini hakutaka kuendeleza mshangao akampungia Gwakisa mkono na kuondoka zake huku Gwakisa akizidi kuwakodolea macho tu!
………………………………………
Milioni mia mbili na hamsini zilikuwa zimeingia kwenye akaunti ya Sam, alishangaa sana lakini hakuna mtu hapendi pesa, Sam nae alizifurahia.
Alipomaliza kila kitu aliondoka zake, alipoingia kwenye gari alipigiwa simu, aliichukua simu na kuangalia ile namba hakuijua ila akapokea.
“Mheshimiwa kiasi cha fedha umekiona?”
“Ndio nimekiona”
“Sawa, sasa hiyo ni nje ya mkataba tumeamua upate ya kutumia kidogo”
“Anhaa…!”
“Ndio hivyo, alafu siku sio nyingi ile nafasi ya cheo chako kupanda itatangazwa”
“Sawa”
“Kumbuka kuzingatia mkataba na nakutakia kazi njema”
Kila sam alipokuwa anakumbuka mkataba akili yake ilikuwa inaumia mno… shauku yake ilikuwa ni kulitumikia jeshi la polisi kwa uaminifu mkubwa sasa leo anatakiwa awe sehemu ya uhalifu! Hii ilikuwa inamuumiza sana kichwa.
Katika kipindi ambacho alikuwa anapanda vyeo mfululizo alikuwa anajikuta kuwa na uzalendo wa kuitumikia nchi kwa moyo mmoja kama shukrani kwa upendeleo alio kuwa anaupata lakini kumbe hata waliokuwa wanaratibu mipango yote ya Kozi mbalimbali na vyeo vyake ni hao watu ili wamtumie!
Kwa upande mmoja alikosa amani lakini kwa upande mwingine kila alipokuwa anazifikiria fedha moyo wake ulikuwa unapata nafuu flani japo sio ya kudumu.
…………………………..
Kila siku zilipokuwa zinasogea watoto wake walikuwa wanakua na kuchangamka huku wakizidi kuonekana kufanana nae sana.
Mtoto aliyezaa na Nisha japo alikuwa wa kiume lakini alionekana kuwa mzuri wa sura mno, labda kwa sababu mama yake ni chotara.
Sam alitamani awaunganishe watoto wake wafahamiane ila kimbembe kilikuwa kwa mkewe, imani yake ni kwamba angevuruga ndoa yake na Rafiki kitu ambacho hakutaka kitokee kamwe.
Alichoamua ni kuendelea kutunza ile siri tu,
Akiwa njiani kuelekea kwa Nisha mawazo mengine ya jinsi ya kumwambia Verity kuhusu mtoto wake yaliendelea kukiumiza kichwa chake.
Alijiuliza atamuingia Nisha kwa njia gani, je? Atamuamini kuwa hakuhusika kwenye kumteka mtoto wake? Hapo aliumia sana,
Hata hivyo tayari alikuwa ameshafika nyumbani kwa Nisha na kupokelewa na Msichana wa kazi ambaye alikuwa na Nice wamekaa sebuleni.
“Dadiiiiiii” Sam aliitwa na mwanae.
Alimdaka na kumkumbatia na hapo hapo Nisha akatokea na kumkaribisha ndani chumbani. Huko waliongea mengi kuhusu namna ya kumwambia Verity kuhusu kupatikana kwa mtoto.
Walipokubaliana mwishowe wakaamua kumpigia Verity Simu ili waonane sehemu, Verity nae japokuwa alikuwa na mambo yake mengi lakini alimheshimu sana Sam na kukubali kuonana nae.
Safari ya kwenda kuonana na Verity ilikamilika huku kwenye gari wakiwa wamekaa Sam, nisha na Nice.
Walipofika walitafuta sehemu nzuri wakakaa nje ikiwa ni nje kidogo ya mji kisha wakamjulisha Verity ni sehemu gani wamekaa.
Verity nae alimaliza mambo yake haraka haraka kisha akavaa vizuri na kujiangalia kioo akajiona amependeza kisha akabeba poci yake ili aondoke.
Mara zote Verity alipokuwa anaitwa na mtu yeyote hususani wa Kiume hali inakuwa tofauti mtu huyo anapokuwa ni Sam. Haelewi hata siku moja kwamba kwanini inakuwa hivyo, sio kwamba ana tama ya kingono na Shemeji yake huyo kwa mara nyingine lakini hamchukulii kama wanaume wengine.
Katika maisha yake yote aliwahi kupenda mara moja tu na mwanaume aliyempenda sio mwingine bali ni Sam. Mpaka wakati huo hakupenda awe na hadhi mbovu mbele ya sam na ndio maana alikuwa akijua kuwa anaenda kuonana na Sam alikuwa anajitahidi kupendeza.
Alitoka nje ukumbini akachukua gari yake na safari ya kuelekea kule aliko Sam ikaanza, ndani ya akili yake alikuwa anawaza sana kuwa ni jambo gani hilo ambalo sam amemuitia. Shauku ilikuwa kubwa sana na ndio maana aliamua kuacha vyote aende.
Muda wote Sam nae kiroho kilikuwa kinamdunda akimfikiria Verity na hali ambayo atajisikia baada ya hapo.
Kila wakati alikuwa anamuangalia Nice ambaye alikuwa yuko sawa tu wala hana presha yeyote kwani alikuwa hajui anaenda kukutanishwa na nani.
Ghafla mlangoni Sam alipigwa na butwaa alipotupa macho yake kule, alimuona mwanamke mrembo sana ambaye amependeza kweli kweli. Hakuwa mwingine bali ni Verity. Urembo wake ulikuwa umeongezeka mno hadi Sam akakosa namna na kubaki amesahau ishu ya mtoto na kuganda anauchunguza urembo wa shemeji yake.
Taratibu Verity alikuwa ansogea pale Sam na Nisha walipokaa ila macho yake yakawa yanamkagua mmoja mmoja kati ya NISHA ,SAM na Mtoto aliyekuwa anamuona pale.
Verity hakuweza kukaa, mapigo ya moyo wake yalikuwa yanaenda mbio sana akabaki anamuangalia mtoto aliye mbele yake. Siku zote damu ni nzito kuliko maji, Japokuwa Nice alikuwa amebadilika sana lakini kuna kitu kilikuwa kinakita kwenye moyo wa Verity.
“Karibu ukae Shemeji”
Sam alimkaribisha Verity huku akiwa amesimama na kumshika mabegani, Verity alikaa lakini macho yake hayakubanduka kwa Nice na wakati huo huo akwa anawaangalia Sam na Nisha kama vile kuna kitu anafananisha au anasubiri kuambiwa huku akitamani kuuliza lakini mdomo unakwama……………..
Akili ya Verity haikukaa sawa pamoja na kukaribishwa aketi lakini alikuwa kama mtu maruweruwe, alikaa huku bado anaendelea kumtazama Sam Nisha pamoja na mtoto aliyekuwa kakaa mbele yake.
Mhudumu aliyekuwa amekaa kando alimuona Mgeni aliyekuja na kukaa pamoja na Akina Sam hivyo akaenda ili kumsikiliza.
“Samahani dada nikuhudumie nini”
“Nice” Verity alimjibu Yule muhudumu kwa kutaja jina la Nice, hii yote ni kwasababu mtoto aliyekuwa mbele yake alimkumbusha sana kuhusu binti yake aliyepotea siku nyingi na hivyo akili yake yote ilikuwa imemjaa Nice.
“Umesemaje dada?” Yule muhudumu ilibidi aulize.
Verity hakuweza tena kuagiza kwani baada ya kutamka jina Nice Yule mtoto aliyekuwa mbele yake aliitikia.
Taratibu Verity alikuwa anashusha pumzi na kuzipandisha kwa kasi, mapigo yake ya moyo yalikuwa juu sana.
Nisha na Sam walilijua hili kiasi kwamba hata wenyewe walianza kuogopa.
Wakati huo NICE nae baada ya kusikia jina lake akawa anaendelea kumuangalia Yule mama asijue kuwa ni mama yake.
“Mletee maji makubwa” ou akijitahidi sana kutunza mot ilibidi Sam aagize kinywaji kwa niaba ya Verity.
Mhudumu alienda kuleta yale maji na kumpa Verity ambaye aliyafakamia kwani alihisi roho yake inatangatanga.
Baada ya kunywa kama glasi mbili hivi alimtazama Sam na kumwabia…
“Shemeji nimekuja kama ulivyonitaka nije, naomba uniambie ulichoniitia”
“mbona una haraka sana shemeji, kwanza hongera sana naona unazidi kupendeza tu”
“Asante wala usijali, ila nina haraka kidogo kuna mambo nayafwatilia”
“Sawa shemeji utaondoka tu ila nilidhani kwakuwa huu ni wito wangu basi uupokee kwa mikono miwili wala usiwe na haraka sana”
“Sawa nimekubali lakini ni vizuri sasa tukija kwenye mada yenyewe.”
Sam alivuta pumzi ndefu kisha akaamua kuweka mambo wazi…
“Shemeji kwanza nimeamini kuwa damu ni nzito kuliko maji kwa hiki nilichokiona hapa”
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)
