MAMA ALISHIKWA KALIO MBELE YANGU (54)

Zephiline F Ezekiel

SEHEMU YA HAMSINI NA NNE
TULIPOISHIA...
Gwakisa alipepesuka kisha Sam akamuachia lakini alipotaka kumvaa Sam suruali yake iliyokuwa usawa wa magoti ikamzuia hivyo ikawa ni nafasi nyingine kwa Sam kumvuta na kumpiga kichwa kizito kilichomfanya arudi kinyume nyume ambapo kabla hajafika kwenye kochi ili aliangukie alikutana na kebo ya umeme iliyotua kisogoni kutoka kwa Verity na hapo hapo akazima.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

TUENDELEE...
Glory alitembea kichwa chini akiwaza mkosi ambao unataka kumfikia katika hatua zake za mwisho kumaliza chuo, alitembea taratibu hata mbele alikuwa hana umakini napo.

“Dada vipi mbona umemiliki njia?”
“Oh samahani Kaka yangu niko mbali kimawazo”
“Haaa Kumbe Glory, Vipi mawazo gani tena rafiki yangu”
“Ah kawaida tu Kaka Charles, mambo mengi”
“Alafu nimeona jina lako Notes board unaitwa kule economics, Kuna nini?”
“Dah yani hicho ndio kinanipa mawazo saivi”
“Twende tukae hapo kantini unielezee vizuri”

Kwakuwa Glory alikuwa anahitaji ushauri ilibidi amfuate Charles ambaye wamekuwa marafiki na mara nyingi walikuwa wakisoma pamoja.
Walisogea kando kidogo kisha wakaketi na kuagiza juisi kisha wakaanzisha mazungumzo yao, Glory alimueleza Charles kila kitu kilichotokea na mpaka alipoitwa na Yule Mhadhiri na yote aliyoambiwa.

“Kama ni yu kwakweli nashindwa hata kumhisi vibaya kwasababu mhadhiri Yule sio kama hawa wengine ambao ningeweza nikasema huenda kuna kitu”
“Unamaanisha nini CHARLE?”
“Namaanisha kuwa wangekuwa hawa wahadhiri wengine wenye kashfa za kutoka na wanafunzi ningesema huenda kuna kitu anataka kwako lakini Yule nashindwa kabisa kumpa kashfa hiyo.”

Baada ya maelezo hayo kutoka kwa Charles Glory aliinamisha kichwa kidogo akiwaza mazingira aliyokutana nayo kutoka kwa Yule Doctor na jinsi alivyomuomba namba ya simu.

“Vipi mbona una mawazo tena?”
“Lakini Charles unajua doctor kaniomba namba ya simu?”
“Haaa Kweli?”
“Ndio”
“Mh basi hakuna mwema rafiki yangu, inawezekana nae ni wale wale”
“Sitaki kuamini hivyo, sitaki kabisa na naomba Mungu anisaidie kwakweli maana mambo hayo namimi tofauti kabisa, siyawezi na siyataki”
“Unajua Glory”
“Enheee”
“Wewe ni msichana mrembo sana, hakuna mwanaume yeyote hapa chuoni hakutaki na hatamani kuwa na wewe, hata mkuu wa chuo nina uhakika lazima anakupenda anajizuia tu”
“Wewe Charles wewe, acha kumsingizia mzee wa watu, kwahiyo hata wewe umo si ndio?”
“Ni vile tu Glory wewe na mimi ni kama mbingu na ardhi, sina hadhi yako lakini endapo ningeweza hakika nisingekuwa na kingine cha kuhitaji hapa duniani, ila sikuwezi!”
“Haaaa Charles, sitaki kuamini kuwa na wewe uko hivyo”
Charles hakusubiri zaidi ya hapo ila alinyanyuka na kuchukua Begi lake kisha kwa macho yaliyokuwa yanalengwa na machozi akamuangalia Glory na kumwambia.

“Kwaheri Glory ila kaa ukijua kuwa wewe ni kama tone la maji jangwani, kila mtu analitaka apone kiu yake. Nakupenda sana ila sitaweza ushindani!”

“we Charles subiri kwanza!”
Charles huku akiwa na macho yenye machozi kwa mbali alisimama akageuka upande aliopo Glory!
“Kuna sehemu Dr Kanji anataka tuonane leo, naomba unisindikize simuamini kabisa Yule mwanaume”
“Ila naogopa Glory, endapo akiniona nawewe atanichukia sana, anaweza akanifanyia kama wewe alafu mimi ni mwanamme sio mwanamke nitajinasuaje?”
“Usijali, hatakuona ila wewe utamuona, naomba unisindikize hakuna mtu mwingine ninayemuamini isipokuwa wewe”
“Sawa utanipigia simu”

Ni kweli kwamba Glory alikuwa hamuamini mtu mwingine pale chuoni kwao kwani wengi walikuwa na kinyongo nae kwasababau walikuwa wanamuonea wivu, sio hivyo tu wengi wao pia walikuwa wamemtongoza na kukataliwa hivyo kumjengea chuki.

Kuna wakati hata alivyokuwa anafaulu sana walianza kumzushia kuwa anatembea na wahadhiri ndio maana wanampa maksi kubwa lakini uvumi huo ukafa kwani uwezo wa Glory ulionekana hata kwenye midahalo na semina mbalimbali ambapo uwezo wake wa kujenga hoja ulikuwa na tofauti kubwa kwa kulinganishwa na wenzake.

Mara baada tu ya Kuachana na Charles simu yake iliita akaitoa kwenye wallet yake na kukutana na namba ya dr Kanji ikimpigia.
“Hellow Doctor”
“Hellow Glory”
“Nakusikia Doctor”
“Nakusikia pia, nimekupigia kukujulisha kwamba nimefunga ofisi kwa ajili ya kujiandaa kuonana na wewe”
“Heee” Glory alijibu kwa mshangao!

“Mbona umeshangaa Glory?”
“Kwani kuonana na mimi mpaka ujiandae?”
“Ndio Gory, wewe ni wa tofauti”
“Sasa kama ni hivyo naomba tuahirishe Doctor, nahisi hofu moyoni mwangu”
“Usiwe na Hofu, huna haja ya kuogopa”
“Sawa doctor ila sitachelewa kwasababu Kaka yangu ananihitaji nyumbani”
“Usiwe na wasiwasi”
……………………………………………

Akili ya Rafiki ilikuwa imechafukwa vibaya, alichokuwa anawaza yeye ni namna ya kumtoa mtoto NICE kwenye macho yake nay a watu wengine.
Alijikuta akikosa amani juu ya uwepo wa Yule mtoto, aliona amekuwa kikwazo kwenye furaha yake. Kabla hajawaza sana akamkumbuka mme wake kuwa toka asubuhi hawajaonana, aliamua kuchukua simu yake na kumpigia.

Alipiga mara ya kwanza ikaita bila kupokelewa mpaka ikakatika, akaamua kujaribu tena ndipo ikapokelewa.

Jisni Sam alivyopokea simu ni kama alikuwa anahema kwa kasi kiasi cha kumuogopesha Rafiki,
“Vipi mme wangu unakimbizwa nini?”
Kabla Rafiki hajajibiwa kuna sauti aliiikia ikitokea upande wa pili alipokuwa anaongea mme wake. Sauti ile alikuwa anaifahamu na ilikuwa inafanana nay a Mdogo wake Verity.

Mapigo yake ya moyo yalikita haraka haraka huku vitu kadhaa vikipita kwenye akili yake ila akajitahidi kuficha hisia zake.
“Vipi nimesikia sauti ya Mdogo wangu hapo nipe nimsalimie”
“Sasa nitampaje wakati hujaniambia ulichonipigia”
“WEWE mpe tu kwanza”
Verity alipewa simu akaongea na dada yake ambaye alionyesha kuchangamka tu viuri mpaka walipoagana na kumkabidhi Sam aongee na mkewe.
“Kumbe umeenda Kwake si ungeniambia na mimi twende wote jamani”
“Ilikuwa ghafla tu mke wangu?”
“Ghafla kivipi tena?”
“Nilikutana nae njiani nikaamua kumpa lifti ila nakuja nyumbani saivi”
“sawa”
Rafiki alikata simu ila hasira ndani ya moyo wake ilizidi mara dufu, aliamini kuwa ujio wa Mtoto Nice ndio unazidi kuvuruga kila kitu, alijua kuwa mtoto hhuyo ndie anawaunganisha tena Sam na Verity.

Hofu yake ilizidi kuongezeka kwa jinsi ambavyo verity amezidi kupendeza lakini pia akiwa ni muathirika, itakuwaje endapo Sam akirudiana nae si watakuwa kwenye hatari.

“Huyu mtoto sina budi kumuondoa” alipigia msumari wazo lake.

Dakika zilizidi kuyoyoma na Gwakisa bado hakuamka. Hofu iliwajaa Sam na Verity wakihisi huenda wameua.

“wala hajafa” sam alisema hivyo baada ya kumpima kwa utaalamu aliokuwa nao na kugundua kuwa Gwakisa alikuwa amezimia tu.

“Nisaidie tumuingize kwenye gari langu”
“Unataka umfanyeje?”
“Wewe usiwe na hofu”
Verity na Sam walimbeba Gwakisa mpaka kwenye gari lake kisha akaondoka nae…..

Ndani ya gari Sam alishusha vioo vya gari ili kuruhusu upepo kuingia ndani kwa wingi, hili alilifanya akiamini kuwa kuruhusu upepo kumpuliza Gwakisa kwa wingi anaweza akaamka na kweli ikawa hivyo.

Walipokaribia nyumbani kwa Gwakisa akamshusha huku Gwakisa akionekana kama mtu aliyetoka usingizini kwani alikuwa anajaribu kuvuta kumbukumbu ya kitu gani kilichotokea.

Taratibu akiwa anaelekea kuingia ndani kwake huku Sam akiwa ameshaondoka tayari alikuwa anaanza kukumbuka taratibu kidogo kidogo hadi pale alipokumbuka tukio zima,
Hasira ilimrudia tena hadi akang’ata meno yake mwenyewe.

“Sam safari hii tutapambana na sitokuacha” Gwakisa alijisemea kimoyo moyo.

Kilichokuwa kinamuuma Gwakisa sana kuhusu Sam ni jinsi ambavyo amekuwa akimuingilia kwenye mambo yake. Aliakumbuka jinsi Sam alivyompa mimba Verity na kisha kubambikiwa yeye, alikumbuka pia jinsi alivyoamua kujipoza kwa Nisha na kisha Sam kuja kumpokonya tena.

Kwa akili ya Gwakisa aliamini pia kuwa Verity aliamua kumuacha kwasababu ya Sam na ndio maana baada ya kuachana Verity na Sam wanakuwa karibu sana.

Kuanzia siku hiyo Gwakisa alikuwa anajipanga jinsi gani ya kupambana na Sam ili ammalize.
…………………………
Glory alikuwa ndani ya Gari na Rafiki yake aliyeitwa Charles wanaelekea kwenye appointment na Mwalimu wake wa chuoni anayetambulika kama Doctor Kanji.
Gari ile aliazima kwa kaka yake kama ambavyo amezoea siku zote kuazima gari hiyo na kuendea chuo ama kwenye mitoko yake mingine.

Siku hiyo pia alikuwa nayo yeye na ndani ya Gari yupo Charles, makubaliano yo ilikuwa kwamba watakapofika sehemu waliyokubaliana Charles atashuka na kukaa kando akimsubiria Glory mpaka amalizane na doctor wake.
Glory alipofika tu na kuegesha gari ili washuke alimuona Kanji akija usawa wa gari lake kumaanisha kuwa alishafika hapo mda mrefu.

“Jifiche Charles, Kanji huyo anakuja”
“Yuko wapi?”
Wakati Charles anaulizia alipo Kanji tayari doctor huyo alikuwa ameshafika ikabidi Glory azime taa haraka ya ndani ili Charles asionekane. Hii yote ni ili kutengeneza mazingira ambayo Dr Kanji hatajua kuwa Glory amekuja na mwanaume mwingine.
Baada ya Glory kufungua mlango alitoka na kushikwa mkono na Dr Kanji kisha wakaelekea sehemu ambayo Kanji alishaiandaa kwamba watakaa.

Kanji alivuta kiti na kumsogezea Glory kisha akamshika mabegani na kumkalisha kwenye kiti, Glory alikuwa anajisikia kero kwa kila ambalo Dr Kanji alikuwa anamfanyia kwani hakupenda ile hali.

Baada ya kukaa vizuri kwenye kiti mhudumu alikuja na kusimama mbele ya Glory na kumuulizia ahudumiwe nini.
“Naomba maji makubwa”
“No Glory please”
“Kwanini Dr?”
“Utakunywaje maji kajika mazingira kama haya?”
“Siku nyingine nitakunywa kitu kingine lakini kwa leo naomba maji tu”
Dr Kanji alimuita Yule mhudumu na kumnongo’oneza jambo kisha akamuachia na kisha Yule muhudumu akaondoka zake.
Baada ya kama dakika tatu Yule muhudumu alirudi na chupa kubwa yenye mvinyo kisha akaweka pale mezani na kuwamiminia wote wawili.
Wakati anamaliza kumimina alikuja mhudumu mwingine wa jikoni akiwa na sinia lenye vipande vingi vya kuku wa kubanikwa kisha akaweka pale, kwenye sinia kulikuwa na kila aina ya vikorokoro ambavyo hutumika kulia chakula kwenye mahoteli makubwa.

Walinawishwa mikono na kuanza kula huku glory akiwa anakula kwa aibu aibu. Baada ya muda kidogo tu alitangaza kushiba na kunawa mikono kisha akajifuta na tishu na kusogea pembeni.

Dr kanji nae aliendelea kula taratibu hadi aliposhiba nae akaacha, aliongeza mvinyo kwenye glasi yake na ile ya Glory ambaye alilalamika kuwa hataki kuongezewa zaidi ya pale lakini Dr Kanji aliendelea kumimina hadi glasi ilipojaa.

“Samahani Dr ”
“Bila samahani”
“Naomba tuongee yale mambo ili niwahi kurudi nyumbani”
“Sawa Glory”
Dr Kanji alikata funda mbili za mvinyo glasi ikawa nyeupe akamimina nyingine na kunywa kidogo kisha akawa anamtazama glory kwa macho ya upole yenye hisia kali.

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)

Chapisha Maoni