MAMA ALISHIKWA KALIO MBELE YANGU (54) Jina: MAMA ALISHIKWA KALIO MBELE YANGU Mtunzi: Omary John Mndambi SEHEMU YA HAMSINI NA NNE TULIPOISHIA... Gwakisa alipepesuka kisha Sam akamuachia lakini alipotaka kumvaa Sam suruali yake iliyokuwa usawa wa magoti ikamzuia hivyo ikawa ni nafasi nyingine kwa Sam kumvuta na kumpiga kichwa kizito kilichomfanya arudi kinyume nyume ambapo kabla hajafika kwenye kochi ili aliangukie alikutana na kebo ya umeme iliyotua kisogoni kutoka kwa Verity na hapo hapo akazima. IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI 👉INSTALL👈 TUENDELEE... Glory alitembea kichwa chini akiwaza mkosi ambao unataka kumfikia katika hatua zake za mwisho kumaliza chuo, alitembea taratibu hata mbele alikuwa hana umakini napo. “Dada vipi mbona umemiliki njia?” “Oh samahani Kaka yangu niko mbali kimawazo” “Haaa Kumbe Glory, Vipi mawazo gani tena rafiki yangu” “Ah kawaida tu Kaka Charles , mambo mengi” “Alafu nimeona jina lako Notes board unaitwa kule economics , Kuna nini?” “Dah yani hicho ndio kinanipa ma…