RANIA (1)

Zephiline F Ezekiel
RANIA (1)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA KWANZA Maskini wa mungu Rania,huna bahati mjukuu wangu...alisikika akisema bibi kaasha akiwa amembeba Rania ambae ndo alikua amemaliza kuzaliwa mda huo.. Kaasha alikua akitokwa machozi yasiyo pimika baada ya mka mwana wake hikkan kupoteza maisha baada ya kujifungua mtoto Rania.. Sijui mwanangu atalichukiliaje hili swala...anampenda sana mke wake halafu ndo kamwacha mapema kiasi hiki..jamani mwanangu mimi eeee....alilia kaasha. Vijakazi wake walijaribu kumbembeleza lakini haikusaidia kitu...alilia sana. Muda  mfupi baadae pame alifika akiwa na zawadi mbalimbali alizo mletea mkewe ambae alitarajia kumkuta amejifungua. Aliingia ndani kwa shamrashamra maana alikua alishadokezwa na rafiki yake kua mkewe alishajifungua tayari..mtoto wa kike. Cha ajabu alipoingia ndani alimkuta mama yake akilia..alipoangalia pembeni aliona mwili wa mtu aliepoteza maisha...bila kuuliza alikwenda na kuufunua. Pame hakuamini macho yake baada ya kumwona aliefariki,..alikua mkew…