CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Alhamisi, 2 Mei 2024

SITOISAHAU FACEBOOK (12)

Mei 02, 2024
SITOISAHAU FACEBOOK (12)

SEHEMU YA KUMI NA MBILI
ILIPOISHIA...
Wakiwa katika maombi mara akaanza kiongozi wa kiroho kulalamika huku akiwa chini anagalagala hovyo. Hakuwa akinena kwa lugha lakini alikuwa akilia kwa kabila la kwao huku akimlaani paka aliyekuwa amemkaba koo huku akimshambulia.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Suzi alikuwa anashangaa tu mtu huyo akilia na kuomba msaada. Baadaye alitulia. Huo mda aliotulia tuli ndio ambao Suzi aliutumia kumsogelea. Dhahama ikahamia kwake!!Sasa aliweza kumuona paka mkubwa rangi nyeusi!! Paka akamkwaruza kadri alivyoweza. Suzi alikimbilia chumbani lakini bado hakumkwepa paka huyu.Wakati nafika na kuufungua mlango ndio wakati huo ambao paka alipotea na kumwacha Suzi ambaye alitimka mbio na kunikuta mimi nikiwa nimeanza kukimbia tayari.

Sasa alikuwa ameweza kuongea.“Ajabu paka huyu hajamdhuru mgonjwa.” Suzi alishangaa. Nami nikashangaa zaidi. Paka hakuwa amemjeruhi mama hata kidogo!.Simulizi hiyo ya Suzi iliniogopesha sana. nikamualika rafiki yangu Maria aishi nasi kwa muda. Wiki ya kwanza tangu afike pale. Mambo yalikuwa vizuri tu. Hapakuwa na mauzauza na michubuko katika paji la uso wa Suzi ilikuwa inafifia.Jioni moja nilikuwa najisomea kwa maandalizi ya mitihani iliyokuwa imekaribia. Suzi ambaye hatukuwa tunasoma darasa moja alinikatisha kidogo. Akaleta maongezi yanayohusiana na imani za kishirikina juu ya kupote kwa John. Nilitega sikio nikamsikiliza kwa makini hadi akayamaliza maongezi yake.

“Ujue nini Bela hapa kuna mtu hawapendi anakufanyizieni” alizungumza huku akiwa amenikazia macho binti huyu wa kisukuma.Kimya nikawa namsikiliza!!“Na hapa ukilemaa wanampoteza na mama.” Alitamka maneno yaliyonishtua. Sasa hapo nikamtilia maanani. Ushauri wake wa mwisho akanisihi niende kwa mganga wa jadi kabla mama hajachukuliwa.Kwa kuwa aliweka neno mama sikuwa na ujanja. Siku mbili baadaye nikaingia kwa mganga wa jadi kwa mara ya pili.

Mara anikwangue kiganja mara anikwangue kichwani mzee huyu!! Mimi kimyaa namsikiliza atasema nini. Akaomba pesa akapewa.Akatoa masharti yake!! Hayakuwa magumu sana. tukatii na kuondoka.Alituomba turejee baada ya wiki moja. Tuliporejea tukakuta matanga. Mganga mjanja mjanja hakuwa nasi tena duniani. Alikuwa amekufa!! Kifo cha ghafla. Siku moja baada ya sisi kuondoka pale.Taarifa ile kila mmoja kati yangu na huyo rafiki yangu tulipokea kimshtuko. Hasahasa mimi. Nilijiuliza kwa nini? Sikupata jibu.Maisha yakaendelea!!

Hapakuwa na mauzauza tena. Na kizuri zaidi hatimaye mama alizinduka kutoka katika usingizi ule wa kifo. Suzi akajivutia kwake kwamba ni maombi yamemwamsha, mimi sikuwa na lolote la kusema.Mama hakuwa na kumbukumbu yoyote ile, alibaki kushangaa shangaa tu. Kwetu ilikuwa siku ya furaha sana. furaha iliyopitiliza. Sasa mama aliweza kula peke yake na hakuhitaji msaada tena. Walau furaha yangu ikarejea huku nikisahau kuhusu imani za kishirikina na kuamini mama alikuwa katika ugonjwa wa kawaida tu!!

Sasa vipi kuhusu John na ile ndoto niliyoiota? Nilijiuliza. Maana mama alikuwa amezinduka lakini John bado hakuonekana. Chuo kilishindwa kusema lolote maana mwanafunzi wa chuo kikuu anachukuliwa kama mtu mzima hakuna anayemlinda, hakuna uzio uliowekwa kumzuia asitoke, hivyo maisha ya mwanafunzi wa chuo yapo mikononi mwa msomaji mwenyewe. Chuo kitasema nini kuhusu kutoweka kwa John!! Ajabu ni kwamba hakutoweka katika mazingira yoyote yanayoelezeka bali ni ghafla tu akagundulika kuwa hayupo chuoNami nikaichukulia ile taarifa kama ilivyo. Kwanza upendo wangu kwa John ulikuwa umepoa sana. nilikuwa nimeanza kuhisi kuwa huyu si mtu mzuri kwangu.

****Baada ya siku tatu. Mama akiandamana na dada yangu Suzi walirejea Makambako. Kama kawaida pesa ilikuwepo. Kwa nini sasa mama yangu asipate jambo la kukumbukwa maishani. Na Suzi naye apate la kujitambia kwa walokole wenzake. Nikawapandisha ndege. Sasa nikabaki kuishi peke yangu tena!! Sikuwa na uoga mkubwa japo sikumruhusu rafiki yangu huyu kuondoka. Tukaendelea kuishi wote.Usiku huu ambao mama yangu alikuwa ametoweka nilikumbwa na hisia ama jambo la ajabu katika mwili wangu.Kichwa kilikuwa kinauma, nilijaribu kumeza dawa lakini hazikunisaidia sana zaidi ya kuniweka katika majaribu ya kupitiwa na usingizi.

“Maria!! Mi nalala shosti.” Nilimwambia rafiki yangu. Alikuwa amejikita katika kuangalia filamu. Hivyo hakuitilia maanani sana taarifa yangu.Mguu na njia nikakivamia kitanda nikaanza kuutafuta usingizi. Mara hizo hisia za kuumwa kichwa zikatoweka. Nikawa katika hisia nyingine zinazokera. Nikaanza kumkumbuka sana John . nikaukumbuka usiku ule mimi na yeye katika hoteli ya kifahari. Nikakumbuka pia jinsi nilivyoanza kuishi naye kama mchumba wangu. Mara nikayakumbuka mapenzi yake.Ni hapa sasa nikaanza kuhangaika!! Nilikuwa namuhitaji John.Nilikuwa nahitaji awe nami kitandani!! Lakini hakuwepo.Nilitaka kujilazimisha kuamka niweze kukabiliana na hisia hizi lakini sikuweza. Nikahisi macho mazito sana!!Mara likawa giza nene!! Kisha ndani ya sekunde kadhaa nikajihisi kama nina mikono ya ziada najipapasa. Mh!! Nikataka kufumbua macho bado yalikuwa mazito.

Nilikuwa nimejilaza na kanga niliyokuwa nimeivaa wakati naandaa chakula. Ile mikono ya ziada nikawa naisikia kabisa ikiiondoa bila idhini ya akili yangu!! Nikajilazimisha kuamka. Sikuweza. Sasa nilikuwa sina nguo mwilini.Kisha ile hali ya kumkumbuka John ikazidi. Nikawa katika kuhitaji huduma fulani hivi ambayo ni John pekee aliweza kunitimizia.Penzi……..Sikuchukua muda mrefu nikapata kile ninachokitamani. Lakini lilikuwa kama gogo limeniangukia kifuani. Nikaanza kupalangana kulitoa. Pumzi zikazidi kuniishia lile gogo halikutoka kifuani kwangu.

Sijui kama zilikuwa dalili za kufa ama vipi.Jamani nakufaaa! Nilipiga mayowe. Sijui kama sauti ilikuwa inatoka ama la! Hofu ya kifo ikanitawala.“He!! We naye unalala uchi? Kulikoni leo?” Niliisikia sauti ikiniuliza. Nikadhani bado nina lile gogo kifuani. Nikanyanyuka kwa nguvu sana. Maria alikuwa akitazamana nami uso kwa uso. Alinishangaa nami nikamshangaa.“Unaota wewe!”“Kwani kuna nini?” Nilimuuliza huku nikijishangaa kweli nipo kitandani, uchi kabisa. Halikuwepo lile gogo pale kitandani.Wasiwasi ukatanda!

“Kweli ni ndoto..ndoto mbaya.” Nilimuunga mkono Maria.Haikuwa ndoto kama nilivyodhani na kujiaminisha kuwa ile kanga ilitoka bahati mbaya katika mwili wangu. Kichefuchefu na kukosa hamu ya kula vikaanza kuniandama, mara niwe nataka vyakula vichachu, mara nikivipata navichukia. Ile hali ikanifanya nihisi ninakaribia kuugua ama nina ugonjwa tayari. Mtu menye pesa kama mimi kwa nini niugue niendelee kukaa ndani wakati kuna hospitali zinaweza kunihudumia vyema.Majuma matatu baada ya hali ile nikafikia uamuzi wa kwenda hospitali.

Sikumshirikisha Maria kwa sababu nilihisi ni jambo la kawaida sana. Nikajikokota hadi hospitali. Daktari akanipokea nikamueleza kila dalili inayonifanya nijihisi aidha nina malaria ama ugonjwa mwingine wowote ule. Sikuwaza hata kwa mbali majibu aliyoyatoa daktari.Mimba!!! Una mimba Isabela, yalikuwa majibuSijui kama akili iliniruka name nikaruka nikamkunja daktari ama ni mizimu ilifanya hivyo. Sijui!!Daktari akatapatapa akanitoa na kunituliza. Huku akisisitiza kuwa ninayo mimba. Na majibu hayo yapo sahihi. Alikuwa ameghadhabika kiasi.

Maajabu haya!! Nimeipatia wapi hiyo mimba.Mimi ni muelimishaji wa mambo ya kimapenzi na mahusiano na jinsi ya kujilinda na magonjwa ya zinaa na mimba zisizotegemewa. Sasa nina mimba ya maajabu!! Anayeelimisha ameibeba…..Nimshirikishe Maria? Nilijiuliza. Nikasita. Maria alikuwa mropokaji sana angeweza kunisambazia habari hiyo na heshima yangu ikashuka. Sikuwa tayari kuabika mbele ya maelfu ya wanafunzi anaoniheshimu sana.

Nikimueleza mama atanilaani!! Maana alikuwa akiniamini sana, bora basi angekuwepo John ningesema ni ya kwake.Sasa hapa namsingizia nani?Hapana sina mimba mimi!! Nilijikataa penye ukweli.Nikaenda hospitali nyingine. Jibu lilikuwa MIMBA.Akili ikahama, na nikaanza kuamini kumbe ule mtihani wa mama kupoteza fahamu ulikuwa mdogo sana. kumbe tatizo likikukumba wewe ndio utaugundua uzito wake.Nikimbilie wapi Isabela mimi!!! Nilitaharuki.Hisia zangu zikaenda kwenye lile gogo usiku ule. Nikajiona nimedhalilishwa kupewa mimba na gogo.

Tena ndotoni!! Chumbani kwangu.Eeh!! Mungu nionee huruma mja wako. Nilikumbuka kumshirikisha sasa Mungu. Baada ya miezi kadhaa ya raha bila kufanya ibada.**Dada yangu Suzi. Alikuwa ni mlokole lakini licha ya hayo yote alikuwa jasiri katika kutunza siri. Hili lilifahamika kwetu sote tangu tukiwa wadogo. Alitunza siri nyingi sana kifuani mwake. Siri za baba, siri za mama, zote alizibeba bila kuzitoa. Ama kwa hakika alikuwa mtu wa kipekee mwenye kifua haswa.Nikamuona mlokole huyu ni mtu sahihi katika kumueleza linalonisibu.Nikampigia simu tukapanga wakati tulivu kabisa wa kuzungumza.

Tukapendekeza iwe usiku. Mumewe akiwa ameingia kazini.Usiku ukafika nikampigia simu.Baada ya salamu za hapa na pale nikautua mzigo.“Dada, yaliyonikuta ni makubwa mdogo wako…” nilianza kumuelezea mkasa ulivyokuwa huku nikisita kumshirikisha ukweli kuwa kuna ndoto ikiambatana na hisia ilinishika na nikahisi nafanya mapenzi ndotoni. Nilihofia ataleta ushauri wa kwenda kwa wachungaji feki kuombewa. Sikutaka kabisa kusikia mambo yake ya kilokole.Nilipomaliza ukawa wakati wake kunishauri ama kusema lolote.

Kwa sauti tulivu tena iliyojaa unyenyekevu Suzi alianza kunieleza neno kwa neno.Sasa nikaanza kutetemeka alipoyatamka haya. Nikaketi chini, mapigo ya moyo yakaongezeka.Nikatamani nife kwa muda. Kisha nikakumbuka kuwa nilikuwa naogopa kufa!!! Nikalipuuzia wazo hilo.Wasiwasi ukazidi. Lakini Suzi alikuwa akiusema ukweli aliouficha moyoni kwa muda mrefu.Suzi aliongea huku akitia msisitizo kwa aliyokuwa anayasema.Ilikuwa ni historia ambayo sikuwahi kuisikia kamwe lakini sasa Suzi alikuwa ananifumbua macho. Uhusiano wa matukio alivyoupangilia ulinitia katika mashaka.Wakati nampigia simu wazo langu kuu lilikuwa kuitoa ile mimba ambayo hata sikuwa na uelewa imeingia vipi katika mwili wangu. Nikamdanganya kuwa mpenzi wangu amenipachika lakini hatukuwa na mpango wa kupata mtoto katika kipindi hicho.

“Bela, Bela..usije ukathubutu kuitoa hiyo mimba!!! Usithubutu!!” alinikanya Suzi, hapo ni baada ya kunieleza kuwa kila msichana aliyethubutu kutoa mimba katika ukoo wetu alipoteza kizazi ama uhai.Maneno hayo yaliambatana na mifano kadhaa ya ndugu zangu ambao hadi leo hii wanalilia watoto. Umri unakwenda na hakuna dalili ya mimba.

USIKOSE SEHEMU IYOFUATA

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Read More

SITOISAHAU FACEBOOK (11)

Mei 02, 2024
SITOISAHAU FACEBOOK (11)

SEHEMU YA KUMI NA MOJA
ILIPOISHIA...
Nikampigia mdogo wangu!!! Nijue kulikoni, wakati huo natetemeka mwili mzima. Jasho likinitoka. Sikutaka kuamini hii ndoto.Kwa hili nilichanganyikiwa kuliko vipindi vyote nilivyowahi kuchanganyikiwa!!

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Simu ikaita. Mara ya kwanza haikupokelewa!!!Nikazidi kutetemeka!!!Mara ya pili simu ikapokelewa.“Dada..shkamoo.”Alinisalimia. Sikuweza kumjibu. Nikamuulizia mama. Akasita kunijibu. Nikamsikia akihema juu juu. Wasiwasi wangu ukazidi.“We Helena!!” nilimuita katika simu.“Abee!!” aliniitikia.“Si nimekuuliza kama mama ni mzima.”“Yeah! Ni mzima. Ila ana homa.”“Naweza kuongea naye sasa hivi?.” Nilimuuliza hakujibu swali lile akazalisha mengine. Nikaanza kuiamini ndoto yangu!!!“Niambie mama ana nini?” sasa nilimkaripia.“Mama ana homa kali amelala!!.”Nikakata simu. Nikasimama wima.

Hofu kuu!!Nifanye nini sasa!! Nilijiuliza. Kisha nikaamua kwa ujasiri kumtafuta John, tayari ilikuwa alfajiri. Nikabonyeza namba zake. Nikawa nasikiliza huku nikitawaliwa na uoga.Simu yake haikuwa hewani. Wasiwasi ukazidi.Ina maana John ndio ameenda Makambako kwa mwalimu Nchimbi!!Nilijiuliza. Sikupata jawabu. Hakuwepo wa kunijibu vilevile.Ilikuwa lazima nifanye kitu. Hapakuwa na muda wa kujilaza tena!!!Nikaufunga mlango nikatoweka!!

Teksi niliyochukua ikanifikisha nyumbani kwa John. Nilikuwa nimeamua kuitoa siri yote ilimradi kuokoa maisha ya mama. NilijiulizaJohn atanifikiriaje kwa haya mashairi ambayo naenda kumuimbia. Litakalokuwa na liwe!! Nilijitia imani.Kama nilivyopiga simu ya John bila kupokelewa ndivyo ilivyokuwa katika mlango wake. Mlango haukufunguliwa na yeyote. Nilibaki katika mshangao hadi alipofika jirani yake na kunitaarifu kuwa hata yeye hajuiJohn alipoenda, ni masaa kadhaa yalikuwa yamepita.

Nilikubaliana naye. Nikatoweka, moyoni nikiwa nazidi kuifuga hofu .John hapatikani nyumbani kwake masaa yamepita, mama yangu ana homa kali. Matukio haya yanayowiana yalinitia mashaka. Mama yangu amekufa! Niliwaza huku nikiichukia hali iliyonikumba. Sikujua ni uelekeo upi natakiwa kwenda, nilisimama chini ya mti nikaanza kuwapigia simu rafiki zake John, wote wakakiri kuonana na John lakini masaa kadhaa yaliyopita. Hakuna aliyemuona muda mfupi uliopita.“Hakuwa na safari yoyote?” Nilimuuliza mmoja wao. Akapinga hoja hiyo. Nikazidi kuumia.

Nilirejea nyumbani kwangu nikiwa nimekata tamaa sana. sikuweza kulala wakati jina la mama likinishambulia kichwa changu.Nilijaribu mara kwa mara kupiga simu ya John. Hali ikawa ileile.Hatimaye nikafikia maamuzi binafsi. Nikaamua kurejea Makambako nikashuhudie tatizo gani limemsibu mama yangu.Kama ilivyokuwa awali nikazungumza tena na kiongozi wa darasa kwa ajili ya kunitetea kwa lolote litakalotokea mimi nikiwa safarini.Nikampatia kiasi kikubwa cha pesa ili kumshawishi zaidi. Akashawishika.

Ndege ndogo ya shirika la serikali ilitua katika uwanja mdogo wa ndege Iringa mjini uliojulikana kwa jina la Nduli. Nilitamani kushuka upesi upesi lakini ulikuwepo utaratibu wa kushuka.Hali ile ua kupanda ndege kama wengine wanavyofanya kwenye magari ilinifanya niamini kuwa pesa ndio kila kitu. Wachache wangeweza kuamini kuwa nilikuwa jijini Mwanza masaa yaliyopita kisha nikawa jijini Dar na sasa mjini Iringa.Kitendo cha kusubiri basi kuelekea Makambako na chenyewe nilikiona ni cha kupoteza muda. Nikakodi gari aina ya Noah.

“Mwendo mkali tafadhali!” nilimsihi.Safari ikaanza.Hali ya mama ilikuwa mbaya zaidi ya homa aliyonielezea mdogo wangu kwenye simu. Ule muda waliokuwa wanashangaa nimefika vipi Iringa mimi niliutumia kumshangaa mama jinsi alivyokuwa anatokwa jasho huku akitetemeka. Alitokwa na vipele vya baridi na kuacha maswali kama anahisi baridi ama la! Maana wakati huo pia jasho lilimiminika.“Mmeenda hospitali?.” Niliuliza swali langu la kwanza. Hakuna aliyenijibu. Nikawatazama nikingojea majibu.Dada yangu akanijibu kuwa walikuwa na mpango huo. Nikatambua anamaanisha nini.

Upesi nikamwagiza mdogo wangu akaenda kuchukua teksi na baada ya muda kidogo mama alikuwa katika machela za akikimbizwa katika wodi ya wagonjwa mahututi. Hospitali ya Ilembula.Madaktari walipima vipimo vyote. Kama nilivyotegemea. Mama hakuwa na ugonjwa wowote. Lakini ajabu!! Alikuwa amezimia. Mama hakuwa akiongea.Baada ya siku nne tukashauriwa kumrejesha mama nyumbani.

Hatukuwa na ujanja tukarejea na mzigo wetu, akawa anahudumiwa chakula kwa njia za mipira. Wakati dada na mdogo wangu wakijiuliza nini kimemsibu mama, nilibaki na siri nzito sana. niliamini kabisa tatizo hili la mama linahusiana kabisa na ile ndoto.Kwa hiyo John ni mchawi!!! Nilijiuliza.Kama ni mchawi basi huyu napambana naye kishirikina. Dawa ya moto ni moto!! Nilijiapiza lakini sikuweza kumshirikisha yeyote kati ya dada ama mdogo wangu. Imani zao za kilokole zilipingana na matendo haya.Nikaamua kufanya kimya kimya!! Ilimradi kuokoa maisha ya mama.Kwa mara ya kwanza nikaingia katika kibanda kidogo cha mganga wa jadi. Nje nikalisoma bango akiwa anajisifia kuwa yeye ni bingwa katika Nyanja tofauti tofauti.

Nilijielezea tatizo langu. Akasema hilo ni tatizo dogo sana. akazungumza lugha alizozijua yeye. Akafoka sana hatimaye akaanza kucheka kama tahira vile. Mwisho akanipatia dawa na maelekezo.Nikatimiza yote aliyohitaji lakini hakuna kilichobadilika.Siku zilizidi kusogea, na kipindi cha mitihani kikajongea zaidi. Nikawa katika mitihani mingi kwa wakati mmoja.Uamuzi wa mwisho niliofikia ni kuondoka na mama akiwa mgonjwa hivyo hivyo. Pia nikaondoka na dada yangu kwa ajili ya kumuhudumia.

Nyumbani akabaki mdogo wangu pamoja na baba.Nilikuwa na pesa na zilizidi kuongezeka lakini ajabu nilikuwa nakonda sana. si ugonjwa wa mama pekee ulionifanya kuwa hivyo bali ile ndoto ya John akishirikiana na Osmani kumchukua mama yangu katika namna ya kuumiza. Walikuwa wanambuluza chini. Sasa mama yupo hoi kitandani. Ajitambui. Na yeye John hajulikani alipo.

Maajabu!!AFE AMA UKUBALIANE NA MIMI!! Niliukumbuka ujumbe huo, niliotumiwa siku chache kabla mambo hayajaharibika. Nikaanza kujiuliza ni kitu gani kilimaanishwa. Kisha nikaikumbuka ile namba +6666666. Haraka nikakimbia chumbani, nikachukua simu nikaingiza zile namba. Simu ikaita lakini haikupokelewa. Nikajaribu tena na tena hali ikabaki kuwa kama ilivyo.Wiki moja ilipita. Nilikuwa najilazimisha kwenda chuo. Na siku hii pia nilikuwa nimeenda.

Lakini hali ya pale chuoni niliona kama hainifariji kabisa. Nikaamua kurejea nyumbani majira ya mchana walau nimuone mama yangu!!Nilipofika getini kabla ya kugonga nilisita. Kwa mbali nilisikia vurumai ikitokea ndani. Na hakuwepo mtu zaidi ya dada yangu pale ndani.Au mama ameshtuka!! Nilijipa imani. Lakini haikudumu kwa muda mrefu. Mlango ukafunguliwa nikamwona mwanaume.Ina maana Suzi ameanza kuingiza wanaume hapa ndani!! Nilikisia kwa mashaka. Kisha nikaamua kuulinda ushahidi. Nikafungua geti nikutane na yule mwanaume nimuhoji.

Tayari nilikuwa nimekasirika.Kwa mwendo wa upesi nikaingia ndani. Hatua za harakaharaka sasa nikawa nakabiliana na yule mwanaume. Tofauti na mategemeo yangu kuwa atashtuka. Aliunyanyua uso wake akanitazama. Nilitaka kukimbia lakini mwili ukawa dhaifu. Sijui kama alikuwa anajaribu kutabasamu au alikuwa anazomea.Uso wake ulikuwa umevimba sana na ulikuwa umechubuka. Ni kama alikuwa amekwanguliwa.Mwanaume huyu wa ajabu akasimama wima akajaribu kuongea akashindwa akanielekeza kwa vitendo kama ananizuia vile kuingia nyumbani kwangu.

Kuna nini sasa!! Nilijiuliza.Akazidi kunisisitiza kwa vitendo nisiingie. Hakuweza kutoa sauti.Kabla hata sijajua nimjibu vipi kwa ishara alinyanyua miguu yake akaliendea geti akatoweka.Akaniacha nikiwa katikati ya kuingia ndani ama kurejea getini. Hali yake usoni ilinitia mashaka sana, nilihisi na mimi nikiingia nitatoka kama yeye. Uoga ukatanda!!Bado sikujua nifanye nini. Sikukumbuka hata kumpigia simu Suzi ambaye ni dada yangu. Nikaanza kunyata kuusogelea mlango, kisha nikaghairi nikaliendea geti nikalifungua likawa wazi kabisa.

Nikaufikia mlango nikataka kuufungua, roho ikawa inasita.Niligundua kuwa nilikuwa natetemeka sana!! nikakishusha kitasa. Mara nikasikia vishindo vikisogea kwa kasi pale mlangoni. Mawazo yangu yakaenda moja kwa moja kwa kiumbe ambacho kimemtia majeraha yule bwana niliyepishana naye. Mbio! Nikatimua.Nyuma vishindo vikaendelea kunifuata kimyakimya.Ilikuwa vyema kwamba nililiacha geti wazi. Nikapenya na kuzidi kukimbia. Sasa mdomo ulifunguka nikaanza kupiga kelele kama chizi. Huku ninazidi kukimbia!!!

Nilipoweza kugeuza shingo kutazama nyuma. Kweli kilikuwa kiumbe cha ajabu!! Kiwiliwili kile kilikuwa kimevaa nguo za dada yangu. Suzi. Lakini usoni hakuwa Suzi. Huyu naye alikuwa ameumuka uso wake. Alikuwa anatisha. Nikiwa nimejikita mawazo yangu katika kumtathimini yule kiumbe anayenikimbiza mchana kweupe mara nikajikwaa.Yule kiumbe naye akawa ananikaribia!!!Maajabu yule kiumbe aliponifikia na yeye hakuwa akizungumza lolote kama yule. Ishara za vidole zikawa zinanielekeza jambo fulani. Sikuelewa lolote!! Cheni yake shingoni ikanifungua akili kuwa yule alikuwa ni dada yangu!! Lakini sasa amekuwaje.

Sikupata jibu umati ukawa umetuzunguka! Kila mtu akitaka kuhoji na kufahamu nini kimetokea. Suzi aliwashangaza wengi sana. Alikuwa amevimba na hakuweza kuzungumza lolote.Kwa ishara hizohizo sasa akaanza kuwaelekeza washangaaji wengine wakamfuata. Baadhi wakiwa na silaha mikononi. Wanawake wakiwa nyuma nyuma…..na baada ya kuifikia nyumba kila mtu akawa anaogopa kuingia ndani ya nyumba yangu. Nyumba ambayo niliizindua kwa mbwembwe za hali ya juu.

Nilifadhaika.Mwanaume mmoja aliyekuwa ameshikilia kisu tayari kwa lolote litakalokuja mbele yake aliingia ndani. Sisi tukabaki kushuhudia nini kitatokea. Suzi ambaye bado sura yake ilikuwa imeumuka alikuwa amejiweka mbali kabisa huku akionekana kutawaliwa na uoga.“Mbona hamna kitu!!” Alizungumza yule mwanaume baada ya kutoka. Mmoja baada ya mwingine wakaanza kuingia katika nyumba yangu. Hakuna madhara waliyopata.Suzi alikimbizwa hospitali. Baada ya siku tatu aliweza kuzungumza.

Kumbe yule mwanaume ambaye nilikutana naye siku ya tukio akiwa ameumuka usoni alikuwa ni kiongozi wa kiroho katika kanisa analolifahamu Suzi maana yeye ndiye alimleta kwa ajili ya kumfanyia maombi mama yangu mzazi.Wakiwa katika maombi mara akaanza kiongozi wa kiroho kulalamika huku akiwa chini anagalagala hovyo. Hakuwa akinena kwa lugha lakini alikuwa akilia kwa kabila la kwao huku akimlaani paka aliyekuwa amemkaba koo huku akimshambulia.

USIKOSE SEHEMU IYOFUATA

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Read More

SITOISAHAU FACEBOOK (10)

Mei 02, 2024
SITOISAHAU FACEBOOK (10)

SEHEMU YA KUMI
ILIPOISHIA...
Osman alinitazama akacheka huku akijiziba mdomo. Nikaita tena. Hakuna John aliyetokea kunisaidia.“Amelala wewe acha kelele.” Alinionya Osman ambaye sasa alikuwa amemaliza kula na alikuwa anakunywa maji. Nikamshangaa.Alikuwa ananijibu bila wasiwasi wowote.“Unajua nini Isabela.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Tulia tuzungumze, mbona haya mambo madogo tu!!.” Aliendelea kuzungumza Osmani. Kidogo nikatulia sasa, akafanya tabasamu kisha akaendelea kuongea.“Nimefuata kitu kimoja tu hapa!! Kimoja tu.”“Nini?.” Niliweza kumuuliza sasa. Nikijilazimisha kuwa jasiri.“Kitambulisho changu.” Alinieleza huku akiwa amenikazia macho. Sauti yake ilisikika vyema kabisa. Hakuwa katika kutania hata kidogo.“Kitambulisho? Kitambulisho gani?.” Nilihoji. Bado nilikuwa chini.“Kile nilichokupa siku ile. Pale wapi sijui. Unapajua wewe.”“Sina kitambulisho cha mtu.” Nilijibu kwa jeuri.

Kama vile jibu lile lilikuwa sawa na kumtukana aliruka akanifikia, kiganja chake kikanyooka akanitandika kofi moja. Maumivu yakapenya hadi mahali machozi yalipojihifadhi, yakatoka kwa fujo huku kilio nacho kikisindikiza.“Sasa nadhani unaweza kuniambia. Kitambulisho kipo wapi.”“Nilikichoma moto.” Nilijibu huku kigugumizi kikinitawala na kilio cha kwikwi.Yule bwana akakodoa macho baada ya kuisikia taarifa hiyo.“Umefanyaje?” aliniuliza, sikumjibu. Nilikua natetemeka sana, nilianza kumuogopa sana Osmani, kwanza niliwaza kile kitambulisho ni cha John iweje aseme chake? na kwanini siku ile alinipa akasema nilikidondosha? Mhh!! Ushirikina!! Nilianza kuamini kwenye imani hizo ambazo nilikuwa siziamini kabisa hapo kabla.Wanafunzi wa SAUT wanaanza kuniroga, wananionea wivu!! nilihisi

“Isabella Isabella!!alinishtua John kutoka kwenye mawazo niliyokua nayo, nilipoangalia kwenye kiti alipo kaa Osmani nikapigwa na butwaa! Osman hakuwepo, Kheeee!! Nikashangaa, John akafikiri nimemuitikia yeye akatoka kutoka kwenye mlango wa chumbani alikosimama akanifuata. Uso wake ulikuwa umetawaliwa na uzembe wa usingizini. Bila shaka alikuwa ametoka kuamka.

“Vipi baby mbona upo mezani? nilishangaa chumbani sikuoni, chooni haukuwepo kulikoni mpenzi au njaa”? Aliniuliza John kwa sauti ya kukwaruza kwaruza. Bado nilikuwa nimekaa chini palepale nilipoanguka baada ya kumshuhudia Osmani akiwa ndani ya chumba changu. Nilishindwa nianze kumjibu vipi John.Mdomo ulikuwa mzito. Pepo la usingizi lililokuwa linamkabili John lilizidi kutwaa nafasi. Akaonekana kushindwa kuvumilia. Akajivutavuta kuelekea chumbani. Mh!! Nibaki peke yangu hapana!!!

Nilikata shauri. Hata taa sikukumbuka kuzima nikatimua mbio. Nikamfuata John. Sasa nilikuwa katika wasiwasi mkubwa hii haikuwa ndoto tena!!!Nilichokiona ni kweli kilikuwa kimetokea.Nilifika chumbani na kumkuta John naye akimalizia kujifunika shuka. Nikaingia kwenye shuka kwa fujo. Hakuligundua hili vurumai labda kwa sababu ya usingizi mzito. Nikamkumbatia John huku nikitetemeka.Hayawi hayawi hatimaye yakawa!! Asubuhi ikafika.

John wangu akaamka wa kwanza. Kuamka kwake kukanifanya na mimi kuukatisha usingizi wangu usiokuwa na ladha kabisa.“Hivi jana ilikuwa ndoto eeh!!.” Alianzisha mazungumzo John.“Umeamkaje mpenzi jamani.” Nikamkatisha kwa salamu, maana hatukuwa tumesalimiana. Akanijibu kisha akaendelea kuzungumza.“Jana si nikaota aisee. Dah!! Ndoto nyingine nazo!! Ila kuota pesa ni dalili za utajiri.”“Ndoto gani tena. Nikamuuliza.”“Eti amekuja mgeni sijui ilikuwa nyumba gani. Umezungumza naye, alipotoka eti akakuachia wewe Cheque mezani sijui milioni ngapi huko.

Nilipotokea si wivu ukawa umenizidi. Nikawa mkali. Akawa kama anahairisha kukupatia. Mi nikaondoka, baadaye nikawa nachungulia mh!! Akaiweka sijui chini ya sahani ile. Ulipotoka kumsindikiza nikawahi kufunua nikakuta amekuandikia kiujumbe hata sikukielewa. Sasa nikawa nakusubiri unieleze yule ni nani. Mara kuku wako haoo wakawika kumekucha tayari!!!” Alimalizia kwa kicheko kirefu John. Nami nikaungana naye. Tukacheka.

“Una wivu we mwanaume!!.” Nilimweleza.“Ah!! Ndoto tu hizo.” Alifunga mjadala.Wakati John anaingia kuoga, mimi niliamka na kuanza usafi wa hapa na pale. Nikiisaili nyumba yangu. Sasa nilikuwa sebuleni. Nilipofika pale palikuwa kawaida tu!!Hivi kumbe jana nilikuwa naota!! Nilijisemea.Nikaanza kutoa vyombo mezani. Tayari kwa kuviosha na ambavyo havijatumika nivirudishe mahala pake. Ni hapo ndipo nilipopatwa na mshtuko mwingine mkubwa. Chini ya sahani moja palikuwa na karatasi. Karatasi ya rangi ya kijani kibichi. Hili jani ama karatasi? Nilijiuliza. Nikajikaza nikausogeza mkono nikalishika.Lilikuwa karatasi!! Nikalinyanyua kwa uoga mkubwa. Bado liliendelea kuwa karatasi. Mkono wa pili nao ukajisogeza ukalipakata.

Kisha nikaligeuza.Maandishi!!! Ya rangi nyeupe. Kiswahili sanifu, maneno machache.AFE AMA UKUBALIANE NAMI.Nani sasa? Nikajiuliza.UTAMFAHAMU HIVI KARIBUNI.. Maandishi yale yalimalizia kama yanayojibu swali langu.Mwisho zikawekwa alama ambazo nilihisi kuwa ni namba za simu. +666666666. Simu ya wapi hii!! Nilitafakari.Nikahisi wazimu unataka kunipanda. Akili zikasogeleana niliposikia John akiufunga mlango wa bafuni. Nikatwaa kile kikaratasi nikakificha kabatini.Sikutaka John agundue kitu chochote. Maana kugundua kwake kungesababisha nimueleze pia juu ya kitambulisho, pia juu ya mauaji aliyoyafanya ndotoni na sasa yametokea kweli. Haukuwa wakati muafaka wa kumueleza.

**Jina langu lilizidi kukua katika chuo cha mtakatifu Augustino, wasichana wengi walitamani sana wawe kama mimi maana hakuna kitu ambacho nilikua sina, takataka zote za urembo nilikua nazo, cha ajabu mimi Isabella sikuonekana kuwa karibu na msichana yeyote yule, hata rafiki yangu Happy nilimsahau, hela kitu kingine bwana nilisahau mema yote aliyonitendea Happy maana maisha yalivyokua yananipiga mtu wa kwanza kumfuata alikua yeye lakini kwa wakati ule nilimsahau kabisa

Mtu wa jirani yangu alikua John nilisahau kabisa kuwa John aliniacha kwa ajili ya umasikini wangu, sikufikiria kabisa kuwa anaweza kuwa yupo nami kisa ya pesa nilizokua nazimiliki,pesa za kutotolea jasho zaidi ya kuwaelimisha tu watu kidogo. kweli mapenzi ni upofu.(Utata)Mama weeeeeeeeeeee!!!nilishtuka kutoka kwenye ndoto mbaya, ndoto iliyonitoa jasho jingi nililowa utafikiri nilijimwagia maji,.

Ilikuwa ndoto mbaya nyingine katika orodha ya ndoto zangu za hivi karibuni. Niliota nipo kwetu Makambako, siku hiyo tulienda kupamba ukumbi wa sherehe na mama yangu ambaye alizoeleka kama Mwalimu Nchimbi, tulimaliza saa tano usiku, hatukupata gari la kuturudisha nyumbani tukaanza kutembea kwa mguu kwa sababu mahali pale hapakuwa mbali sana na nyumbani, mara tukashangaa nyuma vijana wawili wanatukimbiza. Tuliamini kuwa walikuwa vibaka.

Mama akaanza kukimbia na mimi nikafuata nyuma huku tukipiga kelele za kuomba msaada, hatukupata msaada wowote tukazidi kukimbia kwa juhudi zote na sasa kila mmoja akaanza kuchoka.Mama akasema maneno fulani ya kukata tamaa huku akimkabidhi Mungu madaraka ya kuamua kitakachotokea kwetu. Mimi sikuwa na neno la kuongezea nikiwa nimekata tamaa niligeuka nyuma kutazama vijana haoa watatuua kwa silaha gani. Badala ya kutilia maanani silaha zao kali walizobeba, macho yangu yakatua kwenye sura zao.

Osmani!! Alikuwa anatabasamu. John!! Yeye alikuwa amekunja sura kwa ghadhabu. John wangu!! Nilishangazwa sana na uwepo wa John katika kunikimbiza mimi na mama yanguNiliendelea kutulia nikitegemea maswali kutoka kwa viumbe hawa wasioonyesha huruma hata kidogo. Sikuulizwa swali.

Mara wakagawana majukumu. John akamwendea mama na Osmani akanifuata mimi. Alikuwa ameshikilia kitu mfano wa mkia, aliponifikia akanitandika nao mikononi. Maumivu yakapenya nikatokwa na yowe kubwa sana nikaanza kugalagala. Akaniacha pale akamfuata mama. Wakasaidiana na John kumnyanyua mama halafu wakaanza kukimbia naye huku wakimburuza.

Nilipiga kelele nikiwasihi wamuache mama yangu. Lakini hakuna walichobadilisha walizidi kukimbilia na kupotelea gizani. Nilipiga mayowe sana lakini hakutokea mtu wa kunisaidia. Nilipoanza kujigalagaza kwa kukata tamaa ndipo nikakutana na ardhi ya ajabu, ardhi inayonesanesa. He!! Ardhi ya wapi hii?Nilijiuliza huku nikijilazimisha kufumbua macho yangu, macho yalikuwa mazito sana kufumbuka. Nikajilazimisha hadi yakafumbuka.Nikakutana na giza nene, nikaanza kupapasa huku na huko, nikakutana na vitu vingine viwili vinabonyea nilipojilazimisha zaidi kuvitazama ndipo nikakutana na mito miwili katika kitanda changu. Na ile ardhi ndio hiki kitanda changu cha sita kwa sita. Ndoto!!!

Nikawasha taa lakini nikahisi maumivu makali katika mikono yangu, Kheee!nikashtuka kukuta mikono yangu imevimba na ina alama ya kama michirizi hivi, hofu ikanitanda mhh!! ina maana ilikua ya kweli ama? Kama ni kweli kwa hiyo John amempeleka wapi mama yangu?Wamempeleka wapi mwalimu Nchimbi!! Nikaendelea kutahamaki. Hali hii sasa ilikuwa ya hatari kupita zote.

Gusa popote katika maisha yangu ila chunga usimguse mama yangu. Nichezee uwezavyo, ninyanyase uwezavyo lakini kamwe usiyafanye haya kwa mama huyu aliyenibeba tumboni kwa miezi tisa. Kwa gharama yoyote lazima ujutie ama la nijute mimi.Kama hii ni kweli John lazima anieleze ni wapi wamempeleka!!Nilijiapiza.Upesi nikapapasa na kuipata simu yangu ya mkononi. Bila kujalisha ulikuwa usiku wa saa ngapi ilikuwa lazima nimpigie mama niweze kujua nini kinatokea huko walipo , nikajaribu kumpigia hapatikani!! Nikaogopa kukubaliana na ukweli huo. Kwamba na ndoto ile ilikuwa sahihi kama zilizopita na kuondoka na uhai wa wanadamu.

Mungu wangu mama hapatikani ana nini jamani? nilijiuliza hivyo huku nikisahau kuwa huo ulikua usiku na inawezekana akawa amezima simu.Ilikua kama saa tisa za usiku..nikampigia baba naye akawa hapatikani, kwa baba sikuwa na wasiwasi niliamini huenda amelala vilabuni.Nilijiuliza maswali mengi huku nikijiuliza kwanini mambo yale yananitokea mimi, ni wapi nimekosea.Niliumiza kichwa sana hatimaye usingizi ukanitwaa. Na kuwaza kukakoma!!!Bila kujua hatma ya mama!!!

Nilishtuka baadaye kutoka usingizini baada ya simu yangu kuita kwa mda mrefu, kuangalia jina ni la mdogo wangu, usingizi wote ukaniisha nikakumbuka ile ndoto ya usiku, hofu ikanitanda nikawaza au mdogo wangu alikua ananipigia kunipa habari za msiba wa mama? mara simu ikakatika.Nikampigia mdogo wangu!!! Nijue kulikoni, wakati huo natetemeka mwili mzima. Jasho likinitoka. Sikutaka kuamini hii ndoto.Kwa hili nilichanganyikiwa kuliko vipindi vyote nilivyowahi kuchanganyikiwa!!

USIKOSE SEHEMU IYOFUATA

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Read More

Jumatano, 1 Mei 2024

SITOISAHAU FACEBOOK (9)

Mei 01, 2024
SITOISAHAU FACEBOOK (9)

SEHEMU YA TISA
ILIPOISHIA...
Alimalizia, bado alikuwa ametazama mbele tu. Akiyang’ata meno yake kukabiliana na pepo la hasira.Mshtuko!! Nikatoa kelele ya kuogopa, lilikuwa yowe ambalo hata John aliyekuwa anatazama mbele lilimshtua akapata nafasi ya kuniangalia.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Nilikuwa wima!!! Mikono kichwani mara kiunoni, wakati mwingine najiziba uso. Mithili ya mwendawazimu.John alidhani nasikitika kwa jinsi alivyonitazama lakini sikuwa katika kusikitika, nilikuwa naogopa sana. Kitambulisho kilichoibiwa si ndio hichi katikati ya maziwa yangu ama!!! La haula!!Ndio hichi kitambulisho cha muuaji. Muuaji mwenyewe si ndio huyu mbele yangu. John ndiye muuaji anayejitafuta mwenyewe.

Mbiombio nikakimbilia chumbani. Sikujiamini tena kuwa mbele ya John. Sikuwa na uwezo wa kumueleza chochote juu ya kitambulisho chake. Kitambulisho kile kilikuwa na utata mkubwa.Nilipokuwa natimua mbio kwenda chumbani, John naye nyuma akanifuata. Muuaji nyuma yangu, lengo langu nifike chumbani niwahi kujifungia mlango. Maziwa yakaruka kwa fujo wakati nakimbia, kitambulisho kikazidiwa ujanja kikakosa pa kujificha. Upesi kikachoropoka.Kitambulisho haramu kikadondoka katika marumaru.Nikasita kuendelea mbele. Sikutaka John akione kile kitambulisho.

Niliweza kusimama nikageuka. John huyo anakuja mbiombio. Macho ya John kwangu. Macho yangu katika kitambulisho kilichokuwa katika marumaru. Kila mmoja na wazo lake.Kitambulisho sasa kikawa katikati yetu. John na mka zake modeli ya ‘wanchoma kumoyo’ akakikanyaga bila kutambua kile kitambulisho wakati ananikimbilia. Kitambulisho ni manira laini sana, kikaisikia kero ya kukanyagwa na bwana John. Zilikuwa zimebaki hatua moja na nusu niweze kukichukua ndipo nikakumbana na wakati mwingine matata ambao nisipousimulia utanilaumu mwisho wa simulizi.

Mi sitaki lawama!!!John akateleza, baada ya kukanyaga kile kitambulisho. Marumaru ikampokea kwa shangwe, kisogo kikatoa mlio kama chuma kilichogongana na chuma kingine. Kitambulisho kikaachana na kile kiatu kikawa mbele yangu.Shida yangu ilikuwa kukiwahi kitambulisho. Sasa kitambulisho kimetulia na John ametulia tuli sakafuni.Mamaaaa!!! Niliita tena, mama mwingine nani sasa zaidi ya mwalimu Nchimbi huko Makambako? Atanisikiaje sasa wakati nipo Mwanza. Ujinga!!

Nikimbie!!! Nilijiuliza huku nikitetemeka.Kwenda wapi sasa?? Ujinga mwingine.Mara damu nzito nyuma ya kisogo cha John. Macho yamefumbwa kistaarabu. Mdomo wazi.Nikahisi kuchanganyikiwa sasa. Damu ikazidi kusambaa katika marumaru ile nyeupe.“Atakufia huyu Isabella shtuka fanya kitu.” Sauti ikaniambia. Sasa hapo nikashtuka, nikainama nikakwapua kitambulisho chenye utata. Nikakimbia nje.

Taksiii!! Nikapiga kelele. Ikasimama, ikaanza kurudi nyuma. Macho ya dereva taksi badala ya kunitazama usoni na kunisikiliza shida yangu, yakawa yananitazama huku mapajani. Nilipojitazama, mbio nyingine mpya kurudi ndani. Nilikuwa nimevaa kinguo kifupi sana. Hakina tofauti na chupi. Kanga iliyokuwa inanisitiri ilikuwa imedondoka huko ndani.Dereva teksi alinisubiri. Nikarejea nikiwa nimeegesha kanga kiunoni.Nina mgonjwa!! Ni mume wangu. Ameanguka!!! Nilimsihi huku nikimvuta. Akanifuata. Tulipofika ndani bado John alikuwa ametulia tuli vilevile.

“Ameanguka!!.” Nilijibu bila kuulizwa. Dereva akafanya jitihada za kumnyanyua John. Wapi haikuwezekana. Kila aliposhikwa ili anyanyuliwe alilegea na kuangukia upande mwingine.Mimi nilikuwa mtazamaji na nilikuwa namuogopa sana John.“Hebu ngoja nakuja!!!.” Aliniaga dereva. Nikaamini anaenda kuleta msaada zaidi. Nikangoja kwa muda fulani dereva hakurudi!! Nilipotoka nje hapakuwa na dereva wala teksi.Nilitamani kupiga kelele. Nikahaha huku na huko. Baada ya robo saa nikaona teksi. Ilikuwa inakuja pale kwangu. Iliposimama alikuwa ni yule dereva. Nyuma yake ikafuatia Ambulance.Wakashuka wataalamu. Wakamtwaa John asiyejitambua.

Bahati nzuri walikuwa wananitambua. Ukarimu ukaongezeka maradufu.John akafikishwa hospitali. Agha Khan.Hakuwa amepasuka sana. Ulikuwa ni mpasuko wa kawaida. Akashonwa. Lakini akatakiwa kupumzika. Fahamu zilimrejea baadaye. Hakuwa msumbufu, alielewa upesi nini kinachoendelea.Siku iliyofuata ndio siku ambayo John alitakiwa kutoka.Nililazimika kurejea nyumbani kuchukua pesa kwa ajili ya malipo. Nikiwa katika teksi, niliwaza juu ya kile kitambulisho. Nikahisi kitaniletea matatizo iwapo nitaendelea kukishikilia, tayari kilitaka kuutwaa uhai wa John. Sasa kitazua mengine.

Sasa nimpatie ama vipi? Nilijiuliza. Sikupata majibu.Ile ndoto ya muuaji anadondosha kitambulisho ilikuwa inanikera maana haikutaka kufutika kabisa. Haikuwa ndoto kama ndoto nyingine maana sasa niliiona sura ya muuaji. Muuaji alikuwa John.Nguvu ya penzi lake ikanikwamisha kumwambia mtu yeyote ukweli huu. Hata yeye pia sikumwambia.“Hichi kitambulisho simpatii.” Niliamua kusimamia upande huo.Wazo la kukitia moto lilikuja baada ya kuwa nimefika nyumbani. Dereva teksi alibaki nje akinisubiri.

Nilikiendea kile kitambulisho nikatoka na mafuta ya taa na kiberiti.Dakika tano baadaye, moshi ulikuwa ukipepea juu, kitambulisho kilikuwa kinateketea. Sikuondoka hadi pale nilipohakikisha natazama na majivu mbele yangu.Hata hayo majivu, niliyakusanya nayo nikayafukia na mchanga.Rasmi nikawa nimekizika kitambulisho!!!Kitambulisho cha muuaji.Baada ya hapo nilifanya usafi kidogo kuondoa zile damu katika marumaru.

Nikiwa ndani ta gari kurudi hospitali walau nilijisikia kuwa nimeutua mzigo mkubwa uliokuwa unanielemea. Mzigo wa kitambulisho.Nilifanya malipo kisha teksi ileile ikaturudisha nyumbani. Mimi na John. Sasa alikuwa anajitambua kabisa. Alitakiwa kupumzika. Na hicho ndicho nilichofanya baada ya kufika nyumbani. Nikamwongoza hadi chumbani akaenda kulala.Mimi nikarejea katika usafi mkubwa sasa sehemu mbalimbali katika nyumba. Redio ilikuwa ikiniliwazana mziki mkubwa niliojaribu kuuimba kwa kukoseakosea.

Na ni redio hiyo hiyo iliyoniziba masikio nisiweze kumsikia mtu amliyeingia ndani bila mimi kujua. Alama za matope katika marumaru zilinishangaza na kujiuliza yametoka wapi.Hakungoja niumize akili yangu sana akanijibu.“Haujambo binti.”Sikumwambia chochote, nikawa namshangaa bado. Akatabasamu.“Haujambo!!!.” Akanisalimia tena, sasa alikuwa analazimisha nijibu.,“We ni nani katika nyumba yangu?.” Nilimuuliza.“Osmani kwani vipi.”Osmani!! Nikaliweka jina katika kumbukumbu kama niliwahi kukutana nalo hapo kabla. Yes!! Niliwahi kukutana nalo. Hata pale chuo tulisoma na akina Osman, wengi tu. Lakini huyu ni Osmani yupi. Nikaendelea kufikiria. Akatabasamu tena kama vile anaisoma akili yangu. Tabasamu lile likanisogeza kwenye jibu, niliwahi kuliona tabasamu hili. Ndotoni!! Hapana.Hoteli, na nilikuwa nimelewa!!! Ndio siku hiyo nililiona.

Si hapo tu, na siku nyingine tena. Lini?Huyu alikuwa ni dereva wa teksi aliyekuwa nami siku ya sakata la kitambulisho. Ni huyu aliyenikumbusha kuwa nimedondosha kitambulisho.“Unataka nini katika nyumba yangu?.” Nilimuuliza nikiwa na hofu.Akatabasamu tena.“Nina mazungumzo na wewe.”“Nitakupigia kelele za mwizi naomba utoke ndani ya nyumba yangu.” Sasa nilifoka. Nikiwa nimesimama wima. Lakini dhahiri nilikuwa katika kutetemeka.Akatabasamu kama kawaida yake. “Kweli unataka niondoke au unatania. Halafu nirudi saa ngapi. Au usiku ndio itakuwa vyema?.” Aliniuliza kwa utulivu kama vile nilikuwa nampa ushirikiano mkubwa kabisa.

Sikumjibu!! Midomo ilikuwa inatetemeka. Sasa wazo la imani za kishirikina likanitawala. Hapa kuna namna.Hapa kuna namna kweli mamaaa weeeee!!! Nilipiga kelele kubwa, kelele haswa. Yule aliyejiita Osman alikuwa amepotea mbele yangu. Alichoacha ni matope yale aliyoingia nayo.Riadha kubwa kuelekea chumbani. Mlango ulikuwa umeegeshwa nikasukuma. Nikamrukia John kitandani nikamkumbatia kama vile tunagombana. Naye akiwa katika usingizi wake akatoa yowe kubwa la hofu. Akanisukuma huko. Nikamrukia tena. Hadi alipokuwa sawa ndipo aliniuliza kulikoni.

Limtu John, limtu!! Nililia.John akanituliza akanishawishi kwamba zile ni ndoto za mchana. Wala sikupoteza muda kukubaliana naye. Ile haikuwa ndoto.Amesema anarudi baadaye John. Nilimkumbusha.“Atanikuta mimi hapa na atakoma kuingia katika nyumba hii usiogope.” Aliongea kiujasiri John. Mimi nimemkumbatia bado.Sikumueleza lolote juu ya huyo Osman. Kwamba niliwahi kukutana naye hotelini nikiwa nimelewa na pia aliwahi kunipatia kitambulisho ambacho kimepotea Iringa.Niliogopa sana kuzua mengine.Nikajikunyata na siri yangu.

Nilikuwa ninaenda na John kila hatua. Siku hiyo. Iwe jikoni, bafuni, na popote pale. Sikutaka kumwachia. Masaa yakahesabika na uoga ukaanza kukimbia.Usiku ukafika. Bado ni mimi na John. John mara nyingi alikuwa ananicheka. Alishangazwa na uoga wangu.Laiti kama angezijua baadhi ya ndoto nilizowahi kuota huenda naye angeogopa ten asana tu!!!.Hii sasa haikuwa ndoto. Nilitamani kubaki kumkumbatia John lakini. Nimuheshimu nani sasa John ambaye hata nyumbani sijamtambulisha kama mchumba ama mwalimu Nchimbi. Mama yangu mzazi aliyeniagiza maji ya kunywa. Nikamtazama John nikatamani kumtukana kwa kusababisha nichelewe kuitikia wito. Nikamsukuma huko. Nikajitoa mikononi mwake.

Nikamsonya!! Nikavaa kanga yangu nikafungua mlango nikatoka.Nikaenda hadi lilipo jokofu, nikachukua maji yaliyokuwa katika kopo dogo. Nikachukua na kikombe nikajongea sebuleni.Hapo mama atagomba kweli!!! Nilijishauri.Sasa nilikuwa sebuleni. Mama hayupo.Mwalimu Nchimbi naye kwa kununa. Hapo keshanuna huyo.Nikataka kwenda kumuangaza nje. Lakini sikuona maana hiyo nikataka kumuita, mdomo ukawa mzito sana. Nikageuka huku na huko. Hola!! Nikageuka tena. Hakuna kitu.Nikajisonya!! Kisha nikaguna mwenyewe kuwa ninamtafuta mtu gizani.Mpuuzi kweli mimi!!! Nikasogea ukutani nikaanza kupapasa. Nikakipata kiwashio, nikabonyeza. Waaa!! Pakapendeza.

Nikageuka. Waaaa!!! Mdomo wazi, mtu anakula chakula.Pwaaaa!! Nikaachia kikopo na glasi.Osmani!!!Osmani anakula chakula nilichopika mimi.“Kaa hapo sahivi jamaa si amelala au.” Aliniambia kwa sauti isiyosikika vizuri, alikuwa na pande la nyama mdomoni.Puuuu!! Nikaanguka. Lakini fahamu zipo pamoja nami. Namtazama Osmani.

“John!!!! John!!!” Nilianza kuita kwa sauti ya juu sana. Osman alinitazama akacheka huku akijiziba mdomo. Nikaita tena. Hakuna John aliyetokea kunisaidia.“Amelala wewe acha kelele.” Alinionya Osman ambaye sasa alikuwa amemaliza kula na alikuwa anakunywa maji. Nikamshangaa.Alikuwa ananijibu bila wasiwasi wowote.“Unajua nini Isabela.

USIKOSE SEHEMU IYOFUATA

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Read More

SITOISAHAU FACEBOOK (8)

Mei 01, 2024
SITOISAHAU FACEBOOK (8)

SEHEMU YA NANE
ILIPOISHIA...
“Yeah! Umejuaje kwani?.” Aliniuliza.“Ni yule alikuwa ndugu yako au sio..”“Ni yeye Michael ndio jina lake. Binamu yangu.” Alisema kwa masikitiko makubwa sana John kisha akainama. Hapakuwa na haja ya kuuliza kama alikuwa anajizuia kutoa machozi.“Pole John.”

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Nilimwambia kwa sauti ya chinichini.“Wamemnyonga binamu yangu wameona kumuua Jesca haitoshi aaah!!.” Alilalamika mwisho akashindwa kuendelea akaanza kulia kwa sauti ya juu. Nikawa katika hali mbili ghafla. Kwanza hofu kubwa kwani alichozungumza John sasa kilitaka kuwa kile ambacho nilikiota. Pili nikawa katika kumbembeleza Michael kwa juhudi zote. Huku nafsi ikiniambia ninambembeleza muuaji.Lakini muuaji gani huyu sasa asiyejitambua kuwa ameua? Nilijiuliza.Nikahisi kuchanganyikiwa.

“Isabela.” Aliniita.“Bee!!.”“Nitahakikisha namfahamu huyo muuaji…kitambulisho chake kilidondoka na polisi wamedai wanafanya upelelezi.” John alitoa kauli nyingine. Kauli ambayo ilinishtua upya. Niliona kitambulisho kwenye ndoto. Lakini mwenye hicho kitambulisho alikuwa ni John mwenyewe na muuaji ni John.Ina maana John anaapa kujitafuta mwenyewe ama!!Nilichanganyikiwa!!!Nilitamani kumweleza John juu ya ile ndoto lakini sasa hamu yote ilikuwa imetoweka. Sikuwa na haja ya kumweleza, ataniamini vipi. Kwamba ni yeye aliyemuua binamu yake kwa kumnyonga na kuwa hicho kitambulisho ni cha kwake.

Hapana hawezi kuniamini hata kidogo!! John ataniona mjinga na ataidharau ndoto yangu.Nikaghairi kumweleza. Siri hiyo ikajikita na kuanza kuutesa moyo wangu. Mateso makali.Baada ya maziko hayo. Sasa chuo kilikuwa kimesimamia kidete juu ya upelelezi juu ya vifo mfululizo vya wanafunzi katika chuo cha mtakatifu Augustino. Kitambulisho kilichookotwa eneo la tukio kilikuwa kimeamsha hamasa ya kumjua muuaji. Polisi walikuwa makini sana katika hili na walikuwa watulivu wakiendelea na upelelezi kimya kimya.Alipotoka msibani John alikuwa na jingine jipya. Alikuwa amepoteza kitambulisho cha chuo.

“Yaani sijui hata kimepoteaje. Maana kilikuwa kwenye Wallet yangu. Sasa ah!!” Alinieleza John. Sasa ndoto ikawa imekamilika kabisa.Ni John alikuwa muuaji. Lakini muuaji wa ndotoni.Ndani ya siku saba nilikuwa nimekonda sana. Uzito ulikuwa umepungua. Ni serikali ya ubongo wangu pekee iliyojua ni nini kinanisibu.Si John wala mtu mwingine aliyejua nini kinanisibu.Nilikuwa nawaza juu ya usalama wa John. Niliona kama anaenda kukutana na hatia kubwa sana ambayo hawezi kuikwepa. Lakini kosa lile alilifanya katika ndoto yangu mimi pekee!!!

Kivipi niwe na hofu!!Nilijifariji kuwa ile ilikuwa ni ndoto tu lakini hapana bado nilikuwa hoi bin taabaniSuala la kupoteza kitambulisho chake lilinipagawisha.kimawazo.****Hakuna ambaye hakujua kuwa sikuwa na tabia ya kunywa pombe baada ya kuanza rasmi kuwa muelimishaji rika la vijana. Nilikuwa nahamasisha sana kuhusu jambo hili na kuipinga vikali pombe.Wataalamu wa mambo walikiri kuwa pombe husaidia kupunguza mawazo sana. Sasa Isabella mimi nilikuwa na mawazo. Tena mawazo makali yaliokuwa yakishambulia ubongo wangu.Kitambulisho!!!Hichi ndio kiliniua kabisa. Hamu ya kula, raha ya kuwa na pesa zote hazikuwa na maana tena.

Siku hii nikaamua kwenda kugida pombe. Lakini kwa siri kubwa kabisa nikaamua kwenda mbali na chuo. Mbali na John.Mbali ya kila jicho linalonifahamu kwa ukaribu.Mkolani!!!! Nikajichimbia huko. Nikatafuta baa safi kabisa, nikajiweka sehemu ambayo si rahisi kugonganisha macho na watu.Moja, mbili, tatu…nikaanza kuhesabu idadi ya chupa zinazokuwa tupu mbele yangu. Ni siku nyingi nilikuwa sijapata kinywaji hichi. Basi ilikuwa burudani.“Dada mna vyumba hapa?.”Nilimuuliza muhudumu mmoja. Akakiri kuwa vyumba vipo. Nikamwomba anifanyie Booking.“Standard, Suite ama Deluxe.” Aliniuliza. Swali hilo likanikumbusha wakati tunampeleka dokta Davis kuchagua hoteli ya kulala.Alijibu vipi vileeee.“Deluxe.” Nilimwambia kwa kujifan ya nimefikiria sana.

Sikuwa na muda wa kuulizia bei. Pesa ilikuwepo ya kutosha.Baada ya kusikia kichwa kinachemka sasa nikahamishia makazi chumbani. Elfu sabini ilinitoka kwa malipo ya chumba.Hata sikujuta!!Mashambulizi ya kunywa pombe yaliendelea kwa fujo. Kitanda cha sita kwa sita kikinisubiri iwapo nitapitiwa na usingizi.Chumba hakikuwa na mbu hata mmoja. Nani kakudanganya raha ni mpaka uende ulaya?Hata Mwanza kuna raha, sehemu yoyote kuna raha.Cha muhimu hizo raha jipe mwenyewe!!!Isabella nilikuwa najipa raha mwenyewe.

Muhudumu wa kike alikuwa bize kila mara kuja kunitazama kama nimemaliza pombe alete nyingine ama labda nahitaji kutafuna kuku akachome ama afanye lost ni mimi tu!!!. Na hiyo ndio ilikuwa kazi yake kwa ujira wa elfu ishirini niliyompa.Ni kweli nilikuwa nimelewa lakini bado nilikuwa ninao uwezo wa kuona. Safari hii mlango ulipofunguliwa aliingia mwanaume, huyu hakuwa na mavazi kama ya yule muhudumu.Alijitambulisha kwa jina sikuweza kusikia. Akataja wadhifa wake, ulikuwa wadhifa mkubwa lakini hata hivyo pia sikuweza kusikia vyema.

Macho yalikuwa yameanza kupoteza nuru. Nikaingia gizani.Saa nne asubuhi ndipo niliamka.“Dada mchemsho tuweke nini na nini?.” Aliniuliza yule dada niliyemlipa usiku uliopita. Hakika alifanya kazi yake ipasavyo.“Leta supu ya mbuzi..supu ya mbuzi unanielewa.” Nilimwambia. Akanielewa akaondoka.Hangover ilikuwa inacheza na kichwa changu. Na sikuwa na mawazo yoyote.Baada ya kunywa supu niliyoipenda kabisa nilijisafisha na kubadilisha nguo. Nikalipia bili zote, kisha yule dada nikamwongeza pesa nikaondoka.Nilipotoka nje niliangaza hapa na pale nikaona teksi, nikaipungia mkono.

“Nipeleke mjini.”“Elfu nane.”Akanitamkia sikumjibu. Nikaingia garini. Akaondoa.Hapakuwa na foleni. Dakika ishirini nikawa nimefika.Nikatoa pesa yake na kumpatia.Nikaanza kuondoka baada ya kuwa nimemweleza kuwa hiyo elfu mbili abaki nayo. Nilikuwa nimetoa noti ya shilingi elfu kumi.Sasa nilikuwa naondoka kabla hajaniita tena.“Umedondosha kikadi chako.” Aliniambia. Nilipogeuka. Nilitazama chini, ni kweli nilikuwa nimedondosha kitu. Nikajongea na kukiokota.“Asante!!” nilimshukuru. Sasa nilimtazama usoni kwa mara ya kwanza.

Nilitaka kumuita jina lake kwa sababu nilihisi ninalijua jina hilo. Hata sura mbona nilikuwa nimewahi kuiona hapo kabla? Lakini kabla sijajua anaitwa nani. Teksi ilipigiwa honi ikapisha njia ikaondoka zake.“Ah!! Huenda aliwahi kunibeba hapo kabla.” Nilijipa moyo.Nikafungua pochi yangu na kuhifadhi hicho nilichookota.“Mungu wangu!!!!” nilipiga kelele kwa nguvu sana. Nilikuwa nimesimama wima.Kwa kuwa halikuwa eneo la watu wengi nilipata sekunde kumi za kuhakikisha nilichokiona.

Hakika kilikuwa chenyewe.Kilikuwa kitambulisho cha chuo ni heri kingekuwa changu.Kitambulisho cha John mikononi mwangu. Kitambulisho kinachoaminika kupotea ,msibani huko Iringa , kitambulisho nilichokiona ndotoni.Kitambulisho cha muuaji!!!Ewe dunia funguka unimeze!!! Ni sala niliyoiomba kimyakimya. Nilikuwa nimezizima siwezi kwenda mbele wala kurudi nyuma.Harufu ya kifo!!!!Nilisahau ni jambo gani lilikuwa limenipeleka huko mjini. Yale mawazo niliyoamini nimeyapunguza kwa kunywa pombe sasa yalikuwa yamerudi kikamilifu.

Tena mara mia zaidi.Hofu ikatanda. Nikachukua teksi nyingine nikarejea nyumbani kwangu.Nilikuwa natetemeka, na kila nilipoguswa na kitu nilishtuka. Hata nywele zangu za bandia kichwani ziliponigusa shingoni nilitetereka.Nilipohakikisha kuwa nimeifunga milango vyema kabisa na ndani nilikuwa peke yangu. Nilifungua mkoba wangu nikakitoa kitambulisho.Hapakuwa na mabadiliko. Kilikuwa kitambulisho rasmi cha chuo kikuu matakatifu Augustino. Mmiliki akiwa John Joseph.Mpenzi wangu.Nililazimisha akili yangu kutafuta kumbukumbu huenda siku moja aliwahi kunipatia kile kitambulisho. Hapana kitu kama hicho.

Au aliweka mwenyewe bahati mbaya akakisahau? Hilo swali walau kidogo liliamsha uhai na kunipunguzia hofu.Akija nitamuuliza!!! Nilimaliza hivyo. Nikautua mzigo wa mawazo.Nikaingia maliwatoni nikasafisha mwili wangu kijuu juu. Nikajitupa katika sofa iliyokuwa sebuleni. Ule uchovu wa ulevi jana usiku ukawa unanishawishi kusinzia.Nikajifikiria kwenda kulala chumbani. Mara mlango ukagongwa.Nikajikausha!! Ukagongwa tena.Nikaenda kufungua. Alikuwa ni John.Alilazimisha tabasamu!! Nami nikatabasamu. Hatukusalimiana.

Tayari kakereka jana sikulala nyumbani!!! Niliwaza, huku nikijiandaa kukabiliana na maswali atakayoniuliza kwa fujo. Wanaume wana mikwara!!!!Akafika hadi katika lile sofa nililokuwa nimejilaza awali. Akajitupa hapo. Akazishusha pumzi kwa nguvu sana. Kisha akajishika kichwa. Mimi yangu macho nikawa nasubiri lawama.“I hate this…..” Alisema huku akiwa kama anajisea mwenyewe.Yaleyale!!! Nikajisemea.“Uko ok!! John!!” Hatimaye nilimuuliza. Hakunijibu!!“John jamani….” Nilibembeleza. Bado hakunijibu kitu. Nikaamini kuwa John amekerwa sana na kitendo changu cha kulala nje biula taarifa.

Wazo!!! Wazo likanijia. Nikasimama tena bila kumuaga nikatoweka pale hadi chumbani. Nikazama katika mkoba. Nikachomoa kile kitambulisho.Nikakisokomeza katika sidiria niliyokuwa nimevaa. Kisha nikarejea sebuleni. Wanaume dawa yao ndogo tu!! Mfanyie kitu anachopenda kwa wakati!! Baaasi hakuna ujanja tena.John akishaona kitambulisho chake ndo basi tena anasahau kuhusu suala langu la kulala nje. Najua mada itageuka na yatazaliana maswali.

Umekitoa wapi? Ilikuwaje? Dah!! Siamini.Kwisha mchezo!! Nilijiaminisha.Sasa nilikuwa mbele ya John. Bado alikuwa kama anayefikiria kitu kabla ya kuzungumza. Nikamsubiri labda atasema kitu hakusema. Nikamuita akaitika kwa kichwa chake kutingishika.“I hate…my country (naichukia nchi yangu).” Alisema huku akitazama mbele. Nikaurudisha mkono uliokuwa umekama kile kitambulisho tayari kwa kumshangaza. Nikakirudisha katika sidiria ili nipishe kwanza anachotaka kusema John.

“Nini tena mpenzi wangu jamani.” Tayari nilikuwa ubavuni mwake wakati anayasema haya. Hakujibu upesi bali alicheka kwanza. Kicheko cha kujilazimisha.“Eti kile kitambulisho….kile kitambulisho kile.” Alianza kuzungumza, nikafarijika kusikia mada ni juu ya kitambulisho na sio wivu wowote wa kimapenzi. Kisha akamalizia, “kile kitambulisho eti kimeibiwa ama kupotea katika mazingira ya kutatanisha. Serikali yetu bwana..haya sasa kuna haja gani ya kuipenda?” Alimalizia, bado alikuwa ametazama mbele tu. Akiyang’ata meno yake kukabiliana na pepo la hasira.Mshtuko!! Nikatoa kelele ya kuogopa, lilikuwa yowe ambalo hata John aliyekuwa anatazama mbele lilimshtua akapata nafasi ya kuniangalia.

USIKOSE SEHEMU IYOFUATA

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Read More

SITOISAHAU FACEBOOK (7)

Mei 01, 2024
SITOISAHAU FACEBOOK (7)

SEHEMU YA SABA
ILIPOISHIA...
Sauti ile ilikuwa inakanya kwa ghadhabu. Waliposimama na mimi nikasimama. Lakini nikiwa nimejiweka tayari tayari kukimbia iwapo itabidi.Yule mbwa aliheshimu amri ile akaacha kumshambulia yule binti pale chini.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Akaondoka kuifuata sauti ilipotokea. Baada ya yule mbwa kuondoka alitokeza yule kijana aliyekuwa anaamrisha. Alitutaka radhi wote kwa pamoja.Mh!! Mimi sihusiki na hili lakini!! Nilijikanya.Kumbe huyu mbwa sio John!!!Au au au!! Ile ndoto imeniathiri akili!!!Nilitaka kurudi chumbani ili niweze kuzungumza na John lakini wasiwasi ukanitawala zaidi.Sikurudi, siku hiyo nililala kwa rafiki yangu.Mbwa!! Hiyo ndio ikawa pointi ya kujitetea, hakuna aliyejua ni kipi kimenikimbiza kiasi kile.Nikaoga, kisha nikalala na kuamka salama.

“HOFU YATAWALA CHUONI SAUT” Alizungumza kwa sauti kuu mtangazaji. Akaanza kuielezea habari hiyo. Mimi nilikuwa nimelala bado. Lakini sikio lilikuwa wazi.“Kijana mwingine amekutwa amekufa kwa kugeuzwa shingo yake, amekutwa na kisu kikiwa na damu lakini hakuwa na kovu lolote mwilini mwake. Huenda alikuwa katika kupambana na muuaji kabla ya mauti kumkuta.”Sijui hata ni muda gani niligeuka, na kukaa kitako. Habari ilikuwa imenishtua. Nilidhani kuwa ni ndoto tena imejirudia lakini haikuwa ndoto hii ilikuwa ni habari inaendelea.

Salma alikuwa ameshika tama akisikitika, hakupata nafasi ya kuniona jinsi nilivyokuwa katika mshtuko mkuu. Nilijilazimisha kulala tena lakini haikusaidia, taarifa hiyo ikanirudisha katika kumfikiria John.Hapana John hawezi kuwa muuaji!!! Nilipingana na maono yangu ya usiku. Nikapuuzia.(Kizaazaa ufukweni)Jina langu lilikuwa limeanza kukua pale chuoni kutokana na elimu ya mahusiano niliyokuwa naitoa. Mwanzoni watu hawakujua ninamaanisha nini lakini mwishowe wakaanza kunielewa. Wasichana waliotendwa walikuwa wanakuja kupata ushauri kwangu. Waliokuwa wakigombana na wapenzi wao nilihusika katika kusuluhisha.

Nilianzisha vikundi kadhaa vya kupinga unyanyaswaji wa wanawake hasahasa katika suala la mapenzi. Kwa kuwa mapenzi yalikuwa yameteka asilimia kubwa ya mawazo ya watu basi nilieleweka kirahisi.Kwa kutumia pesa alizokuwa akituma Davis na kampuni yake niliweza kuandaa semina kadhaa huku nikialika wataalamu wa saikolojia. Masomo waliyotoa yaliwagusa wengi.Sasa kila mtu aliweza kunifahamu walau kwa jina kama hajapata nafasi ya kujua sura yangu.Kampuni iliyoniajiri ya SAVE THEM ilipotuma wajumbe wake kutoka marekani kufika chuoni kwetu kwa ajili ya tamasha kubwa kabisa lililohusisha mambo kadha wa kadha huku nikipandishwa cheo na kuwa muwakilishi wao katika vyuo vikuu vyote nchini ni hapo ndipo jina langu lilikuwa zaidi.

Vile vifo vya wanafunzi sita katika siku sita mfululizo vilikumbukwa kwa kusimama kimya dakika moja kabla ya ufunguzi wa tamasha lile.Vifo vikasahaulika na mambo mengine yakaendelea.Ile ndoto niliyoota kisha nikamfuma John na damu mgongoni niliamini kuwa yalikuwa ni mauzauza tu haukuwepo ukweli wowote.John alikuwa amerejea kuwa mpenzi wangu rasmi na penzi lilikuwa moto sana. Jesca akasahaulika!!!Isabella mimi sikushangaa sana sasa nilipoteuliwa katika baraza la mawaziri wa serikali ya wanafunzi. Nilikuwa naheshimika.Malipo makubwa niliyokuwa napata yalibadilisha maisha ya nyumbani. Yote haya yalikuwa ndani ya miezi miwili.

Kila mara nilikuwa nikifikiria kuhusu hapa nilipo naishukuru facebook, kwani ni hii ilinikutanisha na dokta Davis na sasa nilikuwa mtu kati ya watu.*Ilikuwa siku ya sita ya juma yaani kuanzia jumatatu sasa ilikuwa jumamosi. Siku hii kimvua cha rasharasha kilinikumbusha kulitafuta sweta langu ambalo lilikuwa chini kabisa ya kabati langu la nguo.Licha ya kuwa na nguo nyingi nilikuwa na sweta moja. Mafua yalikuwa kidogo yananisumbua, uchovu wa siku iliyopita pia ulikuwa unanisumbua. Siku iliyopita ilikuwa siku ndefu sana, ilikuwa ijumaa ya kukumbukwa, kampuni ninayofanyia kazi ilikuwa imenihamishia katika nyumba kubwa kabisa ya vyumba vine, sebule na mahala pa kulia chakula. Ilikuwa na geti na ua kubwa tu.

Baada ya kujaza vitu ndani, nilialika watu kwa ajili ya uzinduzi rasmi. Nilialika marafiki wapatao sitini, akiwemo raisi wa chuo, watangazaji wa redio SAUT, marafiki wenye hadhi ya kuwa marafiki zangu, waalimu wenye heshima zao pale chuoni akiwemo ‘Dean of students’ aliyeitwa Mama Nasania, John naye alialika marafiki zake. Hapakuwa na michango wala kadi za michango. Na katika sherehe hiyo hapakuwa na kipengele cha kutoa zawadi.Ndio hakikuwepo hicho kipengele. Sasa zawadi gani ya wewe kumpatia Isabella akaifurahia. Nilikuwa na kila kitu.

Kwa kuwa sikuwa na ratiba yoyote zaidi ya kupumzika niliamua kumeza dawa aina ya pilton. Ili mafua yaweze kupungua kiasi kabla sijaamua kwenda hospitali kumwona daktari.Sijui nilikuwa nawaza nini hadi nikabwia tembe mbili za Pilton.Leo nitasinzia aisee!! Nilijisemea, huku nikiendelea na shughuli za hapa na pale ndani kwangu. Nilikiweka chumba katika hali ya usafi sana kwani siku hiyo John alikuwa na ratiba ya kulala nyumbani kwangu. Kwa mara ya kwanza!!!Nilikuwa katika hali ya ufahari sana. Wadogo zangu waliopoteza heshima kwangu sasa wakawa wananiita dada kwa herufi kubwa.

Hatimaye ule wakati ukafika. Madawa yakanitwaa nikaanza kurembua macho. Sikuwa na ujanja wowote nilikiendea kitanda nikakiangukia usingizi ukanitwaa.Giza nene likatawala hadi pale ulipokuja mwanga tena nikiwa natazama filamu katika kioo kikubwa.Filamu hii ya sasa ilikuwa inachekesha na ilinisahaulisha kabisa uchovu niliokuwanao. Vijana mchanganyiko wa kike na wa kiume walikuwa wapo katika fukwe ambazo sijawahi kuziona kabla, mara wakimbizane mara warushiane maji. Wengine waoga wa kuogelea kama mimi. Wengine wamevaa nguo za kuogelea huku wale walionichekesha wakiwa wamevaa suti ufukweni.

Sikuanza tu kucheka kwa sababu wamevaa suti. Ila nilikuwa nacheka zaidi maana hata John na yeye alikuwa amevaa suti. Tena kibaya zaidi alikuwa amevaa suti na moka. Kama anaenda kanisani jamani!!!!John hakujali lolote. Aliendelea kupunga upepo.Kipengele cha kuchekesha mara kikaisha ghafla likatokea giza, nikakereka, ile giza ni kama iligundua kuwa nimekereka. Ikatoweka, mwanga ukarejea tena.John hakuonekana. Nilipoangaza kidogo nikamuona John akiwa anaogelea na suti yake.Wenzake wakiwa wameacha vichwa juu, yeye alikuwa amezamisha mwili mzima baharini.He!! Nikashtuka nikataka kufumbua macho ila macho yakawa mazito!!!John ana mkia!!!! Mkia wa samaki!!!Nikatapatapa nipige kelele lakini bado sikuweza nilijihisi nimewekewa kitu kizito kifuani. Na mdomo ulikuwa kama umewekewa zipu ya kuuzuia usiamke.

Ule mkia wenye kiwiliwili cha John ukaanza kuyakata maji katika hali ya kushangaza.Mara!!! Meno, meno ya John yalikuwa mengi, huenda ni zaidi ya thelathini na mbili. Halafu yalikuwa makali.Au ni ya bandia? Nilijiuliza.Meno yale hayakuwa ya urembo kama nilivyodhani. Jibu likaanzia pale yaliporarua mikono ya mwanadada mmoja, mikono ikatoweka, wa pili akajaribu kukurupuka mguu mmoja akauacha baharini, wa tatu akasalia bila kichwa, mvulana wa nne aliyeshuhudia bahari ikiwa na rangi nyekundu alikuwa mtaalamu wa kuogelea alikata maji, John aliye katika mfumo wa samaki naye akamfuata kwa kasi.

Yule bwana akafika ufukweni, John alipofika huko akashindwa kupiga mbizi. Akawa kama anatukana kwa lugha anazojua mwenyewe. Yule aliyeokoka akawa anataka kukimbia lakini akaghairi akafanya kitendo ambacho kiliniharibia kabisa filamu yangu.Akaokota mawe na kuanza kumrushia yule samaki mtu.Mawe yakawa yanampata barabara. John samaki akawa anajaribu kukwepa. Yule mtu akajua anaishinda vita ile na kweli John alionekana kuzidiwa. Lakini pasipo kutegemea na katika hali ya kushtua sana. Nyuma ya yule mtu akatokea tena mtu aliyenishtua sana. Huyu sasa alikuwa ni John wangu huyuhuyu. Huyu alikuwa John kamili na hakuwa na mkia. Yule aliyekuwa anaponda alipogeuka kutafuta mawe akakutana na sura ya John, alikuwa kifua wazi.

Pasipokutegemea John alisukumwa chini, akapinduka, lakini yule bwana alijaribu kukimbia tayari mguu wake ulikuwa umekamatwa.John alipogeuka ilea lama ya kuchanwa na kisu ikaonekana. Nikabaki kama zoba siwezi kupiga kelele wala kutoa msaada wowote.Huyu naye akageuzwa shingo, kisha ghafla pakawa giza sikuweza kuona mbele. Lakini nilihisi kama napoteza fahamu hivi.Macho yalipopata ujasiri na kufunguka nilikuwa nimezungukwa na watu wenye nguo nyeupe.Kila jicho likinitazama mimi.Hofu mpya ikaanza.Watu hawa walitabasamu vizuri lakini sikujua kwa nini wanatabasamu.

“Pole sana!!.” Mmoja waoa liniambia.“Nini kwani…eeh!! Hapa ni wapi.”“Hospitali ulipoteza fahamu.” Mwanaume aliniambia.Sasa akili ilianza kuunganika upya nikawatambua kuwa wale ni madaktari. Kilichonisibu nikashindwa kukielewa vyema. Nikavuta kumbukumbuku nikakumbuka kuwa ni ndoto. Ndoto nyingine ya maajabu. Ndoto iliyonifanya nizimie dah!! Hii ilikuwa hatari zaidi ya kawaida. Nikatamani kumshirikisha mtu yeyote kati ya wale madaktari lakini nikaamini kuwa hawataelewa.

Mtu sahihi wa kumueleza ni John. Huu ni wakati muafaka wa kumueleza kila kitu kinachotokea. Ni John pekee ambaye anaweza kunielewa juu ya shida hii. Sikuona mtu mwingine wa kumueleza.Nilipumzika kwa masaa kadhaa kisha John akaruhusiwa kuondoka na mimi. Ni yeye aliyenileta pale hospitali baada ya kugundua kuwa nilikuwa nimezimia.Ilikuwa ni tukio la kawaida mtu kuzimia lakini lilikuwa si la kawaida kwa sababu aliyezimia ni Isabela. Mtu mwenye heshima zake pale chuoni. Kila mtu alitaka kujua nini kimenisibu. Nashukuru John alikuwa akiwajibu kwa niaba yangu.

Sasa tulikuwa chumbani. John alinikorogea uji wa ulezi akatia maziwa na pilipili manga. Alijua kuwa ninaupenda sana uji wa aina hiyo.Nilipomaliza kunywa kikombe cha kwanza. Nilitaka kuanzisha ile mada juu ya nini kilinitokea ndotoni.Maajabu!! Nilipomuita naye aliniita ndani ya sekunde hiyo hiyo. Tukajikuta tunacheka.“Nani sasa aitike ya mwenzake.”“Ladies first.” John alidakia. Basi sikuwa na ujanja mimi nikaitika nimsikilize John anasema nini.“CR (Class representative) wa PR (Public relation)….”“Amekufa??.” Niliuliza hata kabla John hajamaliza kunieleza. Tayari picha ilianza kuja kichwani.“Yeah! Umejuaje kwani?.” Aliniuliza.“Ni yule alikuwa ndugu yako au sio..”“Ni yeye Michael ndio jina lake. Binamu yangu.” Alisema kwa masikitiko makubwa sana John kisha akainama. Hapakuwa na haja ya kuuliza kama alikuwa anajizuia kutoa machozi.“Pole John.”

USIKOSE SEHEMU IYOFUATA

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Read More

Jumanne, 30 Aprili 2024

SITOISAHAU FACEBOOK (6)

Aprili 30, 2024
SITOISAHAU FACEBOOK (6)

SEHEMU YA SITA
ILIPOISHIA...
Nilivuta kumbukumbu ya sura ya Basu, nikamfananisha na yule mhanga wa kwenye ndoto.Hofu!!! Alikuwa mtu mmoja.Nikapiga ukelele wa hofu.“He Mungu wangu nimemuunguza dada wa watu.” Yule muhudumu alipiga kelele huku akizima mashine.Hakugundua kuwa nilikuwa dunia nyingine kabisa tofauti na hiyo aliyokuwa anadhania.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Alinimwagia maji akaniosha nywele. Sikujali ubora wa kazi, nilikuwa nimehamakinika. Akili ilimuwaza Basu.Kama amekufa kifo cha kufanana na kwenye ndoto maana yake nini?Au nataka kuwa mtakatifu??? Nilijiuliza. Huku nikiamini moja wapo ya dalili za kuwa mtakatifu ni kuyajua yanayokuja kupitia ndoto.Mh!! Utakatifu gani huu lakini hata kanisani penyewe siendi?? Nilitengua mawazo yangu.“Dada nakuita jamani!!.” Sauti ya yule muhudumu ilinishtua.

Inavyoonekana alikuwa ameniita mara nyingi sana.Nilikuwa sipo kawaida na niliombea sana wasiitambue hali hii.Simu yangu ikaita nikaitoa kuitazama alikuwa ni Dokta Davis.Nikapokea na kuiweka sikioni.“Samahani nipo saluni.” Nilimsihi.“Usijali nilikuwa nakutaarifu ukatazame salio katika akaunti yako.”“Hamna shida.” Nilimjibu na kukata simu.(Kovu la ajabu mgongoni)

Nilipotoka pale saluni nilitaka niende kwanza nyumbani kwangu lakini nikaona kwanza nipitie benki kutazama salio.“Laki sita elfu sitini na sita na mia sita sitini na sita.” Hiki ndio kiasi kilichokuwa kimeongezeka katika akaunti yangu. Sikushtuka sana safari hii, nilikuwa nimeanza kuizoea pesa hii kubwakubwa.Sikuwa na haja yoyote ya kutoa pesa kwani bado nilikuwa na pesa nyingi ndani. Niliingia katika bajaji iliyokuwa imenileta nikamuamuru anipeleke Kijiweni, huku ndipo nilikuwa naishi.Tulipoifikia kona ya kijiweni nilitelemka na kuliendea duka la madawa nikachukua dawa za kutuliza maumivu.

Nilipofika chumbani nikanywa na kujipumzisha kidogo kwa minajiri ya kuoga baada ya dakika kadhaa. Nilikuwa bado nawaza kuhusu kifo cha Basu kwa kung’atwa, lilikuwa jambo la kushangaza sana. Na kilikuwa kifo cha kustaajabisha, kivipi afe kama ndoto yangu ya usiku? Nilijiuliza sana. Sikupata jibu. Nikajitia imani kuwa hizo ni ndoto.Suala la kwamba ninaandaliwa kuwa mtakatifu lilinisaidia kupungaza hofu.Lakini utakatifu gani sasa huu wa kuupata bila kwenda kanisani??

Kwani watakatifu wote walikuwa wanaenda kanisani!! Nilijiuliza. Kisha nikaukatisha mgogoro huu wa nafsi kwa kumpigia simu John, nilizungumza naye kidogo akaniambia yupo njiani kuelekea Nyegezi kona kutazama maiti ya Basu.Aliposema jina hilo nikashtuka lakini hakugundua kwa sababu hakuonyesha wasiwasi na wala hakuuliza swali.“Basu…Basu amekufa?” Nilijifanya sijui lolote. John akanieleza stori ileile kama mama mnene wa kule saluni aliyosema.Nikaingia katika fumbo, sikumjua mfumbuzi!!!Nikapitiwa na usingizi!!!

Nilikuwa nautazama sasa umati wa watu ambao sikuelewa ni shughuli gani walikuwa wakiifanya. Sikuwatilia maanani sana na wala sikujuaeneo lile ni wapi. Mara nikamuona mtu ambaye ninamfahamu. Nilitamani kumuita lakini niliamini kwa zile hekaheka alizokuwa nazo wala asingeweza kunisikia. Nikapuuzia!!Sikujua nilikuwa nimejikita katika shughuli gani lakini kuna jambo nilikuwa nafanya.Mara nikamwona tena yule mtu ambaye nilionekana kumfahamu, sasa alikuwa katika mtafaruku. Wenzake wote walikuwa wakimpigia kelele katika namna ya kupingana. Alikuwa peke yake na hakuna aliyemuunga mkono. Mara wenzake wakaanza kumzonga sasa hayakuwa mabishano tena bali ugomvi. Mtu mmoja anachangiwa na watu zaidi ya kumi. Ugomvi ukawa ugomvi. Kuna jambo walikuwa wanalazimisha. Jambo hilo huyo mmoja hakuunga mkono kabisa.

Baada ya kuzidiwa mara yule mtu akawaponyoka. Akaanza kukimbia. Alikuwa anakimbia huku akiangalia nyuma. Nilikuwa natabasamu nikimtazama maana alionekana kuwa na hofu kuu.Alipogeuka mara ya kwanza lilikuwa kundi la watu watano wakimfukuza, akazidi kukimbia, alipogeuka tena walikuwa watatu, akajitahidi kujitetea kwa kuendelea kukimbia, wakabaki wawili. Safari hii hakugeuka.Alipokuja kugeuka sasa alikuwa amekaribia kukamatwa. Lakini cha kutia moyo alikuwa anakabiliwa na mtu mmoja tu. Japo alikuwa amechoka lakini hata huyu aliyekuwa anakabiliana naye alikuwa anahema juu juu. Walikuwa wanatazama kama majogoo yanayofanyiana ubabe.Mara jogoo lililokuwa linamkimbiza jogoo mwenzake likamrukia yule mkimbizwa. Wakaanguka chini, ugomvi ukazuka.

Wakagalagana hapo chini kwa namna ya kuchekesha. Nami nikawa nacheka.Mara yule mtu niliyekuwa namfahamu akaangushwa vibaya. Halafu yule aliyemuangusha akachomoa kisu kidogo, upesi akamchana nacho mgongoni. Akatoa ukelele wa uchungu na hofu.Kuchanwa huko kukawa kumemrejesha upya katika ugomvi. Sasa alikuwa na nguvu kamilifu. Yule aliyekuwa na kisu alipojaribu kumchana tena akawa amechelewa mkono wake ukadakwa, kisha kikafanyika kitendo cha sekunde kadhaa tu cha kuikamata shingo ya mwenye kisu na…na….na…“Mamaaaaa!!!” Nikakurupuka usingizi!!

Nilikuwa nimelala masaa sita. Niliyapikicha macho yangu huku na huko niweze kuangalia vyema mbele.Ukungu ulikuwa umetanda. Nikajipikicha zaidi nikaweza kuona, na sasa niliweza kusikia. Mlango ulikuwa unagongwa kwa nguvu. Fahamu zikanirejea vizuri, nikauendea bila hata kuulizia nikafungua. Alikuwa ni jirani yangu.“Kakasirika kweli John dah!! Amegonga mlango, kapiga simu yakohupokei.” Alinieleza huku na yeye akionekana kukasirika.Nilipiga mwayo mrefu kisha nikamuuliza kuwa alikuja saa ngapi. Akanijibu. Kisha akajieleza shida aliyokuwa nayo nikamsaidia . akaondoka!!!

*Sikuweza kuhudhuria msiba uliomuhusu Basu, akili yangu ilikuwa imechoka sana. Baada ya harakati za hapa na pale nilijipikia chakula kisha nilipomaliza nikalala tena.Mara hii mlango ulipogongwa nilisikia vyema kabisa. Nikasimama na kwenda kumfungulia. Alikuwa John na ilikuwa saa tatu usiku.John alikuwa amefanya mfano wa hasira usoni, nililitambua hilo na sikuwa na haja ya kumuuliza kwa nini amekasirika.Baada ya kuzungumza naye dakika kama kumi hivi huku nikijiweka karibu naye. Alilainika na uso wake ukaunda tabasamu.

Tulizungumza mengi na mpenzi wangu huyu wa zamani. Na kama vile tulikuwa tumeambiana kwa pamoja tukageukiana tukakumbatiana kwa nguvu. John alikuwa analia.Nilijua kuwa anamlilia Jesca, sikutaka kumuuliza najua angelia zaidi. Nilichofanya ni kuzidi kumkumbatia, viatu vikabaki sakafuni, sasa tukawa kitandani. Lugha iliyozungumzwa ilikuwa lugha ya mapenzi.John alikuwa mtulivu kama aliyesafiri kwenda ulimwengu wa mbali. Nikaitoa shati yake akawa amebakiwa na singlendi. Nikataka kuitoa na ile.“Ngoja nikaoge kwanza baby…” aliniambia kwa sauti nzito yenye kutamanisha.

Nikatulia nikamtazama naye akanitazama.“Twende wote pliiz.” Nilimsihi. Hakujibu chochote nikajua kuwa maana yake ni kwamba twende.Nikaziondoa nguo zangu, nikajivika upande wa kanga.“He!! Sa na hiyo singlendi waipeleka bafuni kufanyaje tena!!!” Nilimuuliza John baada ya kumuona akiingia na ile singlendi bafuni.“Si haujataka kunivua sa mi ntafanyaje?.” Aliniuliza kitoto. Nikatabasamu, nikamwendea, akakimbilia upande mwingine wa chumba nikamfata tukawa kama tunagombana. Japo hatukutumia nguvu sana!!!

“Ukiweza kunivua nakubeba mgongoni!!” Alinipa motisha nikazidisha juhudi. Nikaitoa nikawa mshindi.Mshindi kubebwa mgongoni!! Ikumbukwe hiyo.Mimi ndiye mshindi, mgongo mali yangu.John akachuchumaa nikawa nyuma yake.Ile nataka kupanda mgongoni nikaona kitu cha ajabu.Kovu!!! Kovu bichi!!! Kovu katika mgongo. Kovu la kuchanwa na kisu!!

“Mamaaaaa!!” nikapiga kelele. John akasimama. Tayari nilikuwa katika kona ya chumba nikiwa natetemeka sana!!!“Sabe sabe!! Umekuwaje…” aliniuliza huku akinisogelea. Nikawa namkimbia, lakini wakati huu haukuwa mchezo tena nilikuwa katika hofu ya ukweli. Nilikuwa namuogopa John.John alinisihi niache utani!!! Lakini sikuwa natania. Nilikuwa katika kumaanisha.Hali ilikuwa tete. John alikuwa ananitisha.Nikiwa katika kumkimbia John. Sasa aligundua kuwa kuna jambo limenisibu. Akanifuata kwa kasi. Akanivagaa. Nikajilazimisha kujitoa mikononi mwake huku nikipiga kelele. Ghafla akaninasa vibao viwili.

Sasa hapo ndio nikachanganyikiwa mwenzenu na kuamini kuwa dunia imefika mwisho. Nililia huku nikimtaja mwalimu Nchimbi.Lakini cha ajabu na kukera huyo mwalimu Nchimbi hata hakuwa akinisikia.Iliniuma. John akaniongeza vibao vingine viwili. Sasa yale maumivu akili ikasogeleana.“John una damu!! Una damu!!”“Damu??” aliniuliza.“Mgongoni umekuwaje wewe.”“Mgongoni pamekuwaje kwani…alilalamika huku akijipapasa”Maajabu mengine jamani!. Mkono wake haukuwa na damu. Akanigeukia.

Nikatamani kuiaga dunia niende likizo mbinguni. Hakuwa na kovu. Mgongo laini kabisa wa kiume ukatazama nami. Nikaruka mita kadhaa.Akapoteza uelekeo kuniona naruka vile nikataka kukimbia nje.Akanidaka kanga yangu. Kanga ikateleza ikauacha mwili.Shanga nane za rangi tofauti zilizokishika vyema kiuno changu ndio pekee zilizosalia katika mwili wangu. Sasa John alikuwa amebaki na kanga mkononi mimi nikiwa nina shanga kiunoni. Nusu nilikuwa nje na nusu nilikuwa ndani.Swali likavamia kichwa changu.

Nikimbie na shanga kiunoni kwenda nje ama nirudi chumbani kwa John huyu wa maajabu!!! John niliyemuhisi kuwa sasa ni Nikiwa katika kujiuliza iwapo nirejee ndani ama nikimbie hivyo hivyo uchi na shanga kiunoni, mara John akaanza kunisogelea huku akiniomba mkono wangu.Anakuita akuue!!! Sauti iliniambia.Hapohapo nikaamua kutimua mbio. Ilikuwa ni kama bahati kwenye kamba ya kuanikia nguo nikakutana na kanga nikaikwapua nikawa nakimbia huku naifunga.Ikawa kama ni muendelezo wa igizo. Wakati nadhani nipo peke yangu katika kukimbia mara nikashangaa tukiwa watatu. Wote wasichana. Mimi nilikuwa kimya. Wenzangu walikuwa wakipiga kelele za kuomba msaada

.John anatafuna watu!! Niliwaza. Nikaongeza mwendo zaidi. Sikuwa tayari kutafunwa. Mawazo yangu yote yalikuwa kwa mwalimu Nchimbi. Anavyonitegemea!!! Atabaki na nani? Nikazidi kukaza mwendo. Kanga ikiwa imenikaa vizuri katika staili ya kupitia shingoni.Mara mmoja akaanguka huku akipiga kelele. Ni hapo ndipo niligeuka, kutazama kulikoni. Niliamini kabisa kuwa ni John anatafuna mtu pale lakini ghafla nikashuhudia mbwa mkubwa akimgalagaza msichana mwingine. Nikatoa ukelele wa hofu kuu.

He!! John kageuka mbwa!!! Nimekwisha mimi. Ewe mwenyezi Mungu nisaidie. Sasa nilikumbuka kusali.Msikimbie nyie!!! Sauti kutoka nyuma ilitukanya. Haikuwa sauti ya John lakini ilikuwa sauti ya kiume.“Spider acha!! Spider shenzi acha!!! Acha!!!.” Sauti ile ilikuwa inakanya kwa ghadhabu. Waliposimama na mimi nikasimama. Lakini nikiwa nimejiweka tayari tayari kukimbia iwapo itabidi.Yule mbwa aliheshimu amri ile akaacha kumshambulia yule binti pale chini.

USIKOSE SEHEMU IYOFUATA

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Read More

SITOISAHAU FACEBOOK (5)

Aprili 30, 2024
SITOISAHAU FACEBOOK (5)

SEHEMU YA TANO
ILIPOISHIA...
Nikaipokea simu nimsikilize shemeji yangu alikuwa akisema nini. Huyu alikuwa ni rafiki yake na John.“Pole shemeji yangu…” Aliniambia kwa sauti iliyokata tamaa.“Mh!! Asante..bana ndo mipango ya Mungu.” Nilimjibu.“Haya bwana mi ndio naelekea huko kumpa kampani mshikaji.”

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Kumpa kampani mshkaji?? Mshkaji gani tena hapa. Nilijiuliza. Sikupata jibu simu ikawa imekatwa.Baada ya dakika kadhaa nilikuwa katika taksi nikielekea maeneo ya Kijiweni ambayo ndio nilikuwa naishi. Hapakuwa na foleni kama kawaida hivyo baada ya dakika chache nilifika chumbani kwangu. Njaa ilikuwa imenishika, sikudumu sana pale ndani nilivua viatu vyangu vya kufunika na kuvaa vya wazi kisha nikatoka. Kuelekea kwenye mgahawa kupata chakula.

Nikiwa katika mgahawa niligundua kuwa kuna kitu napungukiwakatika himaya yangu. Simu!!!Nilikuwa nimeisahau kwenye pochi yangu.Sikutilia maanani sana kwa kuwa tayari nilikuwa najua ni wapi ipo.Nilijikita katika kusubiri chakula huku nikifanya tathmini ya hapa na pale juu ya kazi ya kipekee hiyo niliyokuwa nimepata kutoka nchi za kigeni. Ilikuwa ni kazi moja ya kipekee sana iliyokuja katika maisha yangu wakati muafaka kabisa.

Nikiwa katika kuiwaza hiyo kazi, nikakumbuka ‘umaarufu’ na wenyewe pia nilikuwa nautaka kwa namna yoyote, siwezi kuimba mziki, sijui kuigiza. Sasa nitakuwaje maarufu!!!Pesa, pesa ndio kila kitu. Pesa zitanipa umaarufu. Nikiwa kimya hivihivi kila mtu atajilinganisha na mimi wakati mimi nipo matawi mengine kabisa. Niliwaza hayo!!!Au nigombee uraisi wa chuo?? Nilijiuliza. Nikakatishwa na chakula kilicholetwa mbele yangu. Hivyo sikupata nafasi ya kutafakari majibu.Baada ya saa zima nilirejea chumbani. Moja kwa moja katika mkoba wangu. Simu ilikuwepo. Nikaitwaa nikajilaza kitandani.

Nikatazama kama kuna mtu alinipigia.Yeah!! John alikuwa amepiga na wengine watatu, mama pia akiwemo. Nikawapanga katika orodha nianze na yupi. Niliamini nikianza na mama hatutamaliza maongezi maana tulikuwa na mengi ya kuzungumza.Nikaamua kuanza na John. Nilipopiga simu ikawa inatumika, nikaamua kumpigia mama.Tulizungumza mengi huku akiniahidi kuwa siku inayofuata atanitumia shilingi elfu ishirini za kitanzania kwa ajili ya matumizi pale chuoni.Kidogo nicheke kwa sauti kubwa lakini nikajibana kucheka.

Pesa ninayotumia kwa nauli ya siku moja, leo hii mama anataka anitumie kwa ajili ya matumizi. Kichekesho!!!Wakati naendelea kubadilishana mawazo ya hapa na pale mama. Simu ya John nayo ilianza kuingia. Nikamdanganya mama kuwa salio limeisha nikakata simu nikamtwangia John huku nikiwa bado nakitafakari kielfu ishirini cha mama.John hakuwa anaongea, lakini nilisikia kwa mbali vilio vya kwikwi. Kuna nini? Nilijiuliza.“Halo, halow…John.” Niliita sikujibiwa.Niliendelea kumsikiliza, alikuwa kimya, nikakata nikampigia rafiki yake. Yeye alipokea upesi tu!!“Vipi upo na John?”“Nimeachana naye muda si mrefu, amechanganyikiwa kabisa.”“Amechanganyikiwa? Kwa nini?.” Nilimuuliza kwa wasiwasi.“Dah!! Yaani amezinguana na madaktari huko hospitali hatakikuamini kabisa.”Simu hii ilizidi kunichanganya. Nikajikadiria majibu yangu, ina maana John ana Ukimwi ama? Mungu wangu nimekwisha!!! Nilihamaki.

Suala la kusikia John, kuzinguana na madaktari, amechanganyikiwa. Utata!!!Sasa na mimi nikaanza kuhaha, kana kwamba niliyoyawaza ni sahihi.Upesi nikanunua muda wa maongezi nikampigia tena rafiki yake John. Nikamsihi anieleze nini kimetokea.Bila kusita akaanza kunieleza. Mwishowe nikapata jibu kamili. John hakuwa ameathirika na UKIMWI bali mshtuko. Jesca aliyeanguka wakati wa kuaga mwili wa marehemu viwanja vya Raila Odinga na yeye amefariki.

Cha ajabu na kushtua hakuna ugonjwa wowote uliohusika katika kifo hicho. Nilifadhaika nikakaa chini, sikukumbuka hata kuaga tayari nilikuwa nimekata simu.Mbona hivi vifo vinakuja mfululizo kiasi hiki?? Nilijiuliza na hakuwepo timamu yeyote wa kunijibu.Jesca naye kama ilivyokuwa kwa aliyetangulia aliagwa na wanafunzi uwanja uleule wa Raila Odinga. Halikuwa jambo la kushangaza bali lilimezwa na huzuni. Haikuwa mara ya kwanza vifo kutokea katika maisha ya chuo, lakini hiki kifo cha Jesca kilikuwa cha ghafla mno. Iliuma sana!!!

Wiki mbili zilikatika tangu Jesca aache simanzi kubwa katika chuo cha Mtakatifu Agustino. Nilikuwa karibu sana na John nikimfariji kwa kumpoteza mpenzi wake. John kwa kiasi kikubwa sana alifurahia ukaribu wangu kwake. Kiasi kikubwa upweke ukawa unatoweka.

USIKU WA MANANE
Kila kona ya jijini Mwanza ilikuwa imetulia, upepo ulikuwa unavuma kiasi cha kuyumbisha miti midogomidogo iliyoota pembezoni mwa barabara. Magari machache yalikuwa yakiipa usumbufu barabara ya lami ambayo ilikuwa katika mapumziko baada ya suluba ya mchana.Gari dogo aina ya Corolla ilipata hitirafu ambayo ilionekana kuwasumbua vichwa abiria waliokuwa ndani yake. Kila mmoja alionekana kumsukumia mwenzake mzigo wa kutafuta suluhu ya ya gari hilo. Wale abiriawatatu wote walikuwa wanafunzi wa chuo cha mtakatifu Augustino.

Baada ya muda wa kujadiliana hatimaye mwanafunzi mmoja aliyetambulika kwa jina la Joseph alivua shati lake akaweka pembeni akaingia katika ufundi. Wenzake wawili walitulia wakimtazama.Baada ya dakika kadhaa mwanafunzi mmoja alibanwa haja ndogo. Taratibu akajivuta kichakani. Sijui kwanini aliamua kukitafuta kichaka cha mbali wakati usiku ulikuwa mnene na hapakuwa na watu wakipita hovyo. Alikifikia kichaka taratibu akaanza kuifungua zipu yake tayari kwa kukidhi haja yake ya wakati huo.Ghafla aliiachia suruali yake na kutazama mbele katika namna ya kukodoa huku akiwa na hofu kuu.

Alikuwa akitetemeka huku akifanya namna ya kushtua kama anatisha kitu kibaya kinachomkabili. Nilitamani sana kujua ni nini hicho mbele yake lakini nikaendelea kuwa mtazamaji wa filamu hiyo ya ajabu.Kisha kama aliyesukumwa akaanguka chini. Akawa anajaribu kupambana kwa kujirusha huku na huko. Alikanyagakanyaga lakini hakufua dafu. Alirusha mikono hewani, bado alionekana kukabwa ipasavyo.Ghafla nikajiona kuwa mtu wa ajabu sana, kwa nini nashuhudia jambo hili na sitoi msaada wowote. Nikataka kupiga kelele. Lakini koo lilikuwa limekauka.

Kwanza ni filamu!! Nilijiambia tena.Mara yule kijana akatulia tuli. Nami hapo nikashtuka!!!!Ndoto!! Ndoto mbaya.Nilikuwa nimeung’ata kwa meno upande wa kitanda. Nilikuwa natokwa jasho na nilikuwa naunguruma kama mbwa mwenye ghadhabu anayejiandaa kubweka.Nilihisi kama maumivu kwa mbali katika bega langu.Taharuki!! Kamwe sijawahi kuota ndoto kama hii!! Mbaya sana.Nilitazama saa ilikuwa saa tisa usiku. Giza nene nikiwa peke yangu kitandani.

Nilisimama nikafanya ishara ya msalaba. Nilikuwa natetemeka. Na nilivyokuwa muoga wa filamu za kutisha, basi nilikuwa sikamatiki kwa hofu.Nilikuwa nimebanwa na mkojo lakini nilipaogopa sana chooni. Nikaamua kurejea kitandani. Mkojo ukazidi kunibana. Sasa nikajiona kuwa bwege, nina choo ndani halafu naogopa kukitumia.Ni ujinga kujikojolea kitandani wakati kuna choo ndani ya nyumba!!!Nikaiuweka uoga kando nikaenda bafuni. Nikachuchumaa niweze kukojoa, nikahisi maumivu kiunoni.Mh!! Nimelala vibaya ama!! Nilijiuliza huku nikijilazimisha kuchuchumaa.

Nilipochuchumaa ndipo nikagundua kuwa nanukia marashi yasiyokuwa ndani ya chumba changu. Hilo pia nikalipuuzia.Nikamaliza haja zangu nikarejea kitandani. Nikajidhihaki kwa hofu ya kijinga niliyoiruhusu initawale.Usingizi ukanipitia. Sikuota tena!!!!Asubuhi majira ya saa mbili nikashtuka usingizini. Ilikuwa siku ya jumamosi, nikaamka kuwahi saluni kutengeneza nywele.Kabla ya kufika saluni nilipita hotelini nikapata kifungua kinywa.Niliwakuta wateja wawili tu hapo saluni, hivyo mahesabu yangu yalikuwa sawa, sikuwa nimechelewa sana.

Nilisubiri kidogo zamu yangu ikafika. Baada ya mimi kuanza kuhudumiwa walimiminika wateja wa kutosha.Kila mmoja na haja yake.Saluni huwa ni eneo zuri sana kwa wale wabahili wa kununua magazeti ya udaku, kujipatia habari nyingi burebure tena kwa uhakika kwa sababu hata nafasi ya kuuliza maswali huwa inapatikana.Penye wengi pana mengi. Na sasa tulikuwa wengi pale saluni. Mara kimya kikatawala alipoingia mwanamke mnene. Sikuwa namjua jina lakini haikuwa mara ya kwanza kumwona.

Baada ya kimya hicho ambacho uswahilini kinaitwa ‘jini kapita’ wote tulilipuka na vicheko.Hata yule mama mnene na yeye alilipuka kwa kicheko kikubwa. Kisha tena akauvaa uso wake wa awali.“Mnacheka wakati watu tuna msiba” Alikoroma, nusu akimaanisha na nusu ukionekana dhahiri kuwa ni utani.Wengine wakacheka na wengine wakakaa kumsikiliza.“Halafu mjue sitanii jamani.” Alikazia kisha akaendelea, “Basu ametutoka.”“Basu? Basu ndio nani?.” Mwanamke moja aliuliza.Nami nikapatwa na kihoro cha kuuliza. Nikajizuia lakini sikuweza.“Basu huyu wa BBA (Bachelor of Business Administration).” Niliuliza.

Mama yule mnene kumbe na yeye alikuwa mwanafunzi. Akaiunga mkono kauli yangu. Kwa kueleza kuwa ni mwanadarasa mwenzake.Basu alikuwa amekufa!!!Nini kimemuua jamani, si juzi tu alikuwa anacheza mpira kwenye haya mashindano ya FAWASCO? Niliuliza.Msomaji mashindano ya FAWASCO ni mashindano ya michezo mbalimbali huwa yanafanyika chuoni SAUT. Na katika mashindano haya watu wengi walitokea kumfahamu Basu kutokana na umahiri wake uwanjani.Yule mama mnene akashusha pumzi kabla ya kujibu kwa sauti ya kunong’oneza.“Ameng’atwa shingoni huko Nyegezi Kona. Amekutwa kwenye mawe huko.”“Niniiii!!!!.” Kila mmoja wetu alishtuka kwa namna yake. Wahudumu walisimamisha walichokuwa wanafanya wote wakamgeukia mama mnene. Hakuna kauli aliyobadilisha alimaanisha alichokisema.

Mapigo yangu ya moyo yalikuwa yanaenda kasi. Ile mashine kichwani ikageuka mzigo. Nikahisi kizunguzungu.Alichokizungumza yule mama kilifanana na hali fulani halisi, ilikuwa ni hali gani na kwa nini nilikuwa natetemeka? Nilijiuliza. Sikupata jawabu. Nikafumba macho nikakumbuka saa nane usiku!!!!NDOTO!!! NDOTO YA KUTISHA!! Ndoto iliyonipelekea kushituka nikiwa na maumivu makali. Na si maumivu tu. Nilikuwa nimekiuma kitanda kwa nguvu sana. Na…na …..na nilikuwa nakoroma kwa hasira. Kama Mbwa!!! Nilikuwa kama mbwa!!!

Hiki nini!! Nilitaharuki kwa hofu. Sikusema kitu chochote, niliulazimisha utulivu!!! Lakini moyoni hapakuwa na amani.Inamaana nimekiota kifo cha Basu? Nilijiuliza. Bado sikupata jibu.Nilivuta kumbukumbu ya sura ya Basu, nikamfananisha na yule mhanga wa kwenye ndoto.Hofu!!! Alikuwa mtu mmoja.Nikapiga ukelele wa hofu.“He Mungu wangu nimemuunguza dada wa watu.” Yule muhudumu alipiga kelele huku akizima mashine.Hakugundua kuwa nilikuwa dunia nyingine kabisa tofauti na hiyo aliyokuwa anadhania.

USIKOSE SEHEMU IYOFUATA

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Read More

SITOISAHAU FACEBOOK (4)

Aprili 30, 2024
SITOISAHAU FACEBOOK (4)

SEHEMU YA NNE
ILIPOISHIA...
MWANZA
Ulikuwa usiku wa kipekee sana kwangu, ndio kwanza nilikuwa nimerejea jijini Mwanza, kwa usafiri bora wa ndege. Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Sijui niseme mara ya pili!! Maana mama alinihadithia kuwa nilipokuwa mtoto niliwahi kupanda ndege!!!Baada ya kushuka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere bila kuwa na wa kunipokea sasa hapa uwanja wa ndege wa Mwanza nilihitaji mtu fulani ajue kuwa nimekuja na ndege!! Huyo mtu ni nani kama sio John!!!

Nilimwomba John afike kunipokea. Nilifanya hayo makusudi ili kumkomoa kwa ubaya alionifanyia. Ubaya wa kuniacha na kuwa na mahusiano na msichana mwingine.Ni kweli John alikuwa amenitenda vile lakini John bado alikuwa moyoni mwangu. Nilikuwa nampenda sana John. Walikuwepo wanaume wengi lakini nafasi ya John bado nilikuwa sijaona wa kumrithisha.John aliposikia nakuja na ndege hakusita kunikubalia. Labda ili athibitishe kwamba kweli nimekuja na ndege ama la. John alinipokea huku akinipapatikia, niliifurahia hali hiyo. Tulichukua taksi iliyotufikisha katika hoteli yenye hadhi ya juu ya La kairo jijini Mwanza tukajipatia c

umba. Chumba cha bei ya juu kabisa!! Sikuwa na wasiwasi kuhusu pesa!!Wakati huo John tayari alikuwa amemdanganya mpenzi wake wa wakati huo Jesca kuwa hatarejea chuoni siku hiyo kwa kuwa kuna rafiki yake anaumwa. Ameenda kumsalimia.Usiku majira ya saa nne, tayari tulikuwa tumelia sana baada ya kukumbushiana yaliyopita. John akaniomba msamaha nami sikusita kumsamehe. Kilichofuata hapo ni kurejesha hisia za zamani na kuanza kushambuliana, kila mmoja akijitahidi kuamsha hisia za mwenzake, baadaye kidogo.

Vita!!!Vita ya miili. Kila mmoja akitamani kuibuka mshindi, hapakuwa na mwamuzi. Wakati vita hiyo ikiendelea ikaanza kusikia kama sauti ikiniongelesha kwa kabila kama kihehe vile, lakini sikuweza kuielewa lakini niliwahi kuisikia mahali. Ni kweli niliwahi kuisikia mahali, lakini sasa sikuwa nakumbuka ni wapi. John alikuwa bize, huenda alikuwa akifurahia peke yake. Nilitamani kumwambia John azisikilize zile sauti lakini hakuweza kunisikia alikuwa ulimwengu mwingine.John alipokoma, na sauti zile nazo zikatoweka. Ni kama vile zilikuwa kando ya dirisha zikitusemesha ama zikinisemesha.

“John walikuwa wanasemaje?.”“Nani?. Hao wahudumu ama.?” Aliuliza kwa utafiti.“Hapana!!!anyway acha ilivyo.” Nilimaliza mjadala.John hakuuliza zaidi.Nilielekea bafuni kujisafisha, kisha nikarejea tena pale kitandani. John alikuwa amesinzia. Sikuwa na hamu naye tena bali nilizitafakari zile sauti zilikuwa zikisema nini.Lakini kama John , hajazisikia basi hakuna sauti yoyote!!! Nilijipa moyo.Asubuhi John alikuwa wa kwanza kuamka. Aliingia aliwatoni akajisafisha na kuniamsha. Nami nikafanya kama alivyofanya kisha tukaondoka. John akaelekea alipopajua nami nikaelekea chuoni.

Zile sauti nilizozisikia usiku ule sikuzikumbuka tena. Nilichokumbuka ni kwamba mimi na John tulikumbushia enzi.Sikuweza kujua ilikuwa ni saa ngapi, lakini niliamini ilikuwa ni usiku tena usiku sana. Kuna sauti zilikuwa zimezungumza nami, tena kwa lugha ninayoielewa, zilikuwa sauti zenye furaha sana.Nikiwa bado natafakari sauti hizo zilizungumza nini na mimi. Mara simu yangu iliita. Alikuwa ni rafiki yangu wa darasani. Nikajiuliza kulikoni. Nikaipokea simu.

“Isabella, Isabella….Jenipher jamani. Jenipher!!”“Amekuwaje tena. Eh!! Nambie.”“Jenipher yupo hoi hospitali hapa.” Alijitahidi kuongea bila taharuki lakini alisikika akitetemeka. Baada ya pale hata kabla sijamjibu, simu yake ilikatika.Nilipojaribu kumpigia hakupatikana. Nikajilazimisha kulala, huku nikiamini kuwa lile ni tatizo la kawaida tuAsubuhi palipopambazuka, taarifa ilikuwa nyingine, taarifa ya kushtua nafsi!! Jenipher msichana aliyekuwa akiishi na huyo rafiki aliyenipigia usiku uliopita.alikuwa amefariki baada ya jitihada za madaktari kugonga mwamba.

Ilikuwa habari ya kusikitisha sana kwani kilikuwa kifo cha ghafla mno.Sikuzikumbuka zile sauti za usiku ule zilikuwa zinasema nini na mimi.Sasa nikawa nawaza juu ya msiba huo!! Msiba wa ghafla!!Mwili wa marehemu uliagwa katika viwanja vya Raila Odinga. Kila aliyehudhuria alijawa na simanzi, hasahasa kutokana na kilio cha mama mzazi wa binti yule ambaye alikuwa haishi kumlilia mwanaye huyo wa pekee aliyefanikiwa walau kufika chuo kikuu.Tofauti na watu kuwa na majonzi niliweza kubaini sura ya mtu mmoja ilikuwa na hofu kuu. Huzuni ikiwa mbali naye.

Huyu alikuwa ni John. Sikujua kwa nini alikuwa katika hali ile. Niliyalaumu macho yangu kwa kumtazama vile huenda alikuwa sawa lakini hapana nafsi haikuridhika.Muda wa kuaga ulifika ilianza familia ya marehemu iliyoungana nasi pale chuoni, kisha wakafuata wanafunzi wa kike. Nilinyanyuka na kuungana na msafara mrefu uliokuwa na nia moja ya kumsindikiza marehemu.Jua kali lilikuwa likinisumbua sana na kunifanya nitokwe jasho sana, si mimi pekee niliyelalamika bali na baadhi ya wasichana waliokuwa nyuma yangu nao walilalamika. Lakini mwendokasi wa foleni haukuwa mbaya tuliamini kuwa muda si mrefu kila mmoja atakuwa amemuaga marehemu.

Kwa akili zangu timamu nilisikia mivumo kwa mbali sana. Sikuwa nimesinzia ili nijilaumu kwamba ni ndoto. Hapana nilikuwa najitambua kabisa. Mivumo ile ilikuwa mithili ya mkutano wa injili unaofanyika mbali kiasi na wanatumia spika kubwa kuhamasisha watu wengi waweze kusikia. Kisha sauti hizo kutwaliwa na upepo kisha kurudishwa. Sikuweza kusikia maneno yote na hata hayo niliyoyasikia yalikuwa nusunusu. Nilitaka kumuuliza aliyekuwa mbele yangu lakini bahati mbaya hatukuwa tukifahamiana. Lakini wa nyuma yangu nilikuwa namfahamu nikaamua kumuuliza kama kuna kitu anasikia.

“Eti dada unasikia nini?.” Nilimuuliza.“Sijui hata kuna nini huko mbele hata dah!! Jua kali kweli.” Alinijibu nje kabisa ya swali nililomuuliza. Nikameza mate kulainisha koo langu, alikuwa amenikera.Ghafla nikagundua kuwa foleni ile ilisimama, sasa nikagundua kwa nini yule binti alinijibu vile. Kumbe hakunielewa kabisa.Kimyakimya nikamsamehe!!!Foleni ile haikuweza kusogea mbele, nilikuwa bado katika kutafakari,kulikoni ghafla ilitawanyika. Haikuwa foleni tena bali purukushani. Kila mmoja akataka kutazama kilichopo mbele. Mwanzoni ilikuwa foleni ya wasichana lakini sasa ulikuwa mchanganyiko wa jinsia zote. Kila mmoja akijitahidi kwa kadri anavyoweza kutazama mbele kuna nini.

Nilikuwa mmoja kati ya walioparangana na kufanikiwa kuona mbele. Alikuwa ni Jesca , aidha kwa hiari ama lazima alikuwa amekumbatia ardhi isiyokumbatika. Alikuwa ametulia tuli kumaanisha labda amekipenda kitendo kile. Tulibaki kushangaa kwamba kuna nini kimetokea. Wasichana tukiwa katika mshtuko wanaume walijiongeza wakavua mashati yao na kuanza kumpepea Jesca. John akiwa mstari wa mbele kumtetea huyu mpenzi wake kutoka katika hali aliyokuwanayo.Niliweka kando hasira na chuki dhidi ya binti huyo ambaye kwa maksudi alininyang’anya tonge mdomoni kwa kumchukua mpenzi wangu John kutoka katika himaya yangu. Niliuvaa ubinadamu, huruma ikanishika.Jesca hakutingishika hata kidogo. Sasa alibebwa mzega mzega hadi akawekwa katika kivuli. Zoezi la kumpepea liliendelea.

Yule mwanadada mwingine aliyekuwa ametulia tuli katika jeneza na yeye alikuwa amesahauliwa kwa muda. Cha ajabu hata mama yake mzazi naye macho yake yalikuwa yakifuatilia kwa ukaribu tukio la Jesca kuanguka.Sio maajabu haya!!!!Harakati za kumpepea Jesca ziliendelea hadi gari ya huduma ya kwanza ilipofika eneo lile. Jesca alipakizwa na gari ikaondoka kwa kasi huku ikipia ving’ora vya kuashiria hatari ama dharula.Nilifanya ishara ya msalaba na kumkabidhi Jesca kwa Mungu kutokana na tatizo lililomsibu.

Zoezi la kuaga liliendelea tena upesi upesi. Wakati huu sikumuona tewa John. Bila shaka aliongozana na mpenzi wake alyekuwa amekumbwa na maswahibu.Ile kufikiria kuwa Jesca ni mpenzi wa John. Wivu ukanipiga kikumbo nikajisikia vibaya. Nikahisi kuwa naonewa. Kisha nikaukumbuka usiku wangu wa mwisho na John. Ulikuwa usiu wa kipekee….na…na……na usiku wa kwanza kusikia sauti zile zisizokuwa na maana. Sauti za maajabu.Sasa zinamaanisha nini? Hilo lilikuwa swali. Nje kabisa ya uwezo wangu kujibu. Lakini nani hasa wa kunijibia????Baada ya taatibu zote za kuuaga mwili kufanyika. Zilifuata taratibu za kifamilia. Kuondoka na mwili wao.

Mwili ambao ulikuwa umeagizwa kuja kusoma kwa lengo la kuisaidia familia hapo baadaye mwili huu sasa ulikuwa unarejeshwa nyumbani kwa ajili ya kuzikwa. Inauma sana.Baada ya watu kusambaa niliwasha simu yangu kwa ajili ya kumpigiaJohn na kumjulia hali Jesca. Lakini kabla sijapiga, iliingia simu ya Dokta Davis. Nilishtuka kwanza maana ile kazi niliyoagizwa hata siku moja nilikuwa sijaifanya. Nikaanza kutunga uongo kisha nikapokea simu.“Pole sana na kazi!!! Usijali utazoea. Naona unachoka sana hata kupiga simu inakuwa tabu. Bila shaka ulifika salama na kazi uliianza mara moja." Aliongea bila kuweka kituo Dokta Davis. Nilibaki kujichekeshachekesha, kisha nikakiri kuwa kazi inaenda vizuri sana.

“Safi sana …safi sana.” Alinisifia Dokta. Nikajisikia vibaya kwa kuwa nimemdanganya.Tulizungumza mengi huku akinisihi niangalie akaunti yangu maana kuna pesa ilikuwa imeangulizwa.Taarifa hiyo ilikuwa furaha sana kwangu. Kiukweli nilikuwa napenda sana pesa.Nilipotoka pale eneo la viwanja vya Raila Odinga nilijivuta taratibu hadi nikazifikia ATM, nikazama ndani nikadondosha kadi yangu. Nikatazamana na akaunti yangu ikiwa imekenua, kunifurahisha mimi. Milioni tatu, laki sita na elfu sitini na sita zilikuwa zimeongezeka katika akaunti yangu.

Nilitabasamu mwenyewe, huku nikichomoa kadi yangu. Sikuwa na haja na pesa kwani kwenye pochi laki moja na nusu ilikuwa inasubiri matumizi yangu.Nilipokuwa natoka katika kituo hicho cha kujichotea pesa. Nilianza kuwaza kuhusu umaarufu. Wanafunzi mia nne wa darasani kwetu pekee kunifahamu hilo niliona kama halitoshi. Nilihitaji walau nusu ya chuo waweze kunifahamu. Sikupata muda wa kufikiria kuwa sifa haziliwi wala hazinenepeshi.

Mawazo yangu hayo yasiyokuwa na maana sana yaliingiliana na mlio wa simu.“Isije ikawa taarifa mbaya…” niliwaza.Nikaipokea simu nimsikilize shemeji yangu alikuwa akisema nini. Huyu alikuwa ni rafiki yake na John.“Pole shemeji yangu…” Aliniambia kwa sauti iliyokata tamaa.“Mh!! Asante..bana ndo mipango ya Mungu.” Nilimjibu.“Haya bwana mi ndio naelekea huko kumpa kampani mshikaji.”

USIKOSE SEHEMU IYOFUATA

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Read More