RANIA (2)

Zephiline F Ezekiel
RANIA (2)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA MBILI ILIPOISHIA... Jao..kamata huyu twende nae kwenye jumba la kifalme akapate adhabu yake..hawezi kua na dharau kiasi hiki kwangu mimi...aliamuru fasha. SASA ENDELEA.. Jao alimkamata Rania na kumfunga kamba,lakini hata hivyo rania hakua na hofu yoyote. Wakiwa njiani wanaelekea kwenye kasri(jumba la kifalme),mara walikutana na omandi mlinzi mlinzi mkuu wa mfalme.. Fasha...aliita omandi baada ya kumwona fasha.. Fasha aligeuka na kumwangalia vibaya sana omandi kisha akasema:unaruhusiwa na nani wewe kuniita jina langu badala ya kuniita mwanamfalme?...alisema fasha. Nisamehe sana mwanamfalme.....alisema Omandi akiwa ameinamisha kichwa chake. Haya unashida gani?..aliulza mwanamfalme. Mfalme ameniagiza kuja kukutafuta..alisema omandi. Fasha alishtuka sana na kumuuliza omandi: nani amemwambia kua sipo kwenye kwenye kasri? Hilo mimi sijui...alisema omandi Haya twende...alisema fasha. Mheshimiwa...na huyu binti ni nani?..aliulza omandi. Fasha alimgeukia na kuwangal…