RANIA (5)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA TANO ILIPOISHIA... Mwanangu nataka tuhame nchi...alisema kaasha huku akimwangalia Rania usoni.. Heee...tuhame?....aliuliza Rania kwa mshangao Mwanangu, ni kwa ajili ya usalama wako tu..alisema kaasha Kiaje bibi?.. Alisema Rania kwa mshangao. Kabla kaasha hajajibu kitu mara walisikia farasi wakija kwa vishindo vikuu.. Wote kaasha na Rania waligeuka kuona ni nini hichsana SASA ENDELEA.. Walipogeuka walishangaa kuona kundi la watu wengi wakikimbia huku na huko kuokoa maisha yao. Walipoangalia zaidi waliona jeshi kubwa nyuma likija... Bibi...akina nani hao?..aliuliza Rania kwa uoga. Wanajeshi wa nchi ya Baseki...alisema kaasha. Haaa..wamekuja kufanya nini?...aliuliza Rania. Kufanya vita na hii nchi yetu...alisema kaasha. Rania alikodoa macho kwa uoga sana..walikimbia na kwenda kujificha kweli handaki. Vita ilipigwa kati ya nchi ya Tharia na Baseki kwa muda wa miaka saba.watu wengi wa pande zote mbili waliuawa na wengine walikimbia nchi Zao. Wakati wa vita familia…