RANIA (7)

Zephiline F Ezekiel
RANIA (7)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA SABA ILIPOISHIA... Rania, ninakitu naomba unisaidie...alisema Mfalme. Aaah...kumbe na wafalme hua wanaomba...alisema Rania huku anacheka kwa chini chini. Mfalme ilibidi atabasamu tu maana hakua na cha kufanya. Mfalme alimweleza ombi lake Rania... Nini?...mimi?... Eti niwe....aah..hapana haiwezekani...alisema Rania baada ya kusikia ombi la Mfalme. SASA ENDELEA.. Rania,hujajua Kwanini nimekuchagua wewe nikiwa najua kabisa huna hiyo taaluma...alisema Mfalme kisha akweka kituo. Hapana Mfalme, kwa vyovyote vile hii kazi siiwezi..nitawezaje kua mganga mimi?...nitaifanyaje kazi hii nisioijua?.. Alisema Rania. Rania, hujajua kitu kimoja, naomba nikuelezee kwa mapana zaidi labda utanilewa...alisema Mfalme. Mimi ni mfalme hapa..lakini naendeshwa sana na baadhi ya watu katika ikulu hii akiwemo mwanangu wa kumzaa mwenyewe. Jukumu la kuchagua mganga ni langu kwakua watu wanaamini mfalme pekee ndio anaweza kupata maono ya kuchagua Mganga wa nchi kitoka kwa mizimu jamb…