RANIA (15)

Zephiline F Ezekiel
RANIA (15)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA KUMI NA TANO ILIPOISHIA... Usiku wa manane Dom alianza kunyata na kuatafuta kilipo kile chungu... Alitafuta sana mwisho akafika kilipo chungu ingawa alikua hajajua kama ni hapo.. Muda huo huo mganga alikua anakuja kwa ajili ya kuongeza viungo kwenye dawa yake kuiboresha zaidi ili kumkamata Rania.. SASA ENDELEA.. Wakati Dom anaendelea kushangaashangaa mara kwa mbali Alimwona mganga yulee anakuja..ilikua ni kama bahati tu alimwona mapema. Dom ilibidi avunge kua alikua anapita tu..hata hivyo Dom alikua hajajua kama alipokua ndio penyewe Haraka alitoka na kujificha sehemu aone mganga ataweka mambo yake kwenye kona gani. Mganga bila kujua kama kunamtu anamfuatilia nyuma alifika na kuangaza huku na kule hakuona yeyote yule... Akahakikisha ni salama. Taratibu aliweka dawa yake na kunuia maneno fulani ambayo Dom hakuyasikia... Baada ya kumaliza kazi yake Mganga aliamua kwenda zake.. Wakati huo Dom aliasubiria hadi mganga akafika mbali na yeye akaja. Alinyata tara…