
SEHEMU YA ISHIRINI
ILIPOISHIA...
Mama.. Ni kuhusi Rania... Alisema DomAmekuaje Rania?.. Aliuliza Rai...
Wakati huo Rania alikua amekaribia kwao Dom maana hapakua mbali sana....
SASA ENDELEA..
Mama..kwanza kuna mauaji yana.....alisema Dom kisha mama yake akamkatisha.Najua mwanangu... Watu wameshauawa wengi zaidi ya unaowajua...alisema Rai.
Rania ameshachukua hatua yoyote?... Aliuliza Rai.
Ndo najaribu kumzuia maana hana nguvu ya kutosha kupambana na ufalme... Alisema Dom.
Mwache usimzuie...alisema Rai.
Mama!!!!...aliita Rai kwa mshtuko.
Ndio muda wake...unahisi kama akisubiri nguvu atazipata lini?.. Aliuliza Rai.
Dom alikaa kimya kidogo.
Mwanangu, Rania alizaliwa kwa ajili ya hili jambo... Kama umeamua kumpenda Rania inabidi ujikane...kubaliana na hatari zote... Alisema Rai.
Nakuombea ufanikiwe ili angalau ukamilishe kazi niliyopewa mimi ya kumlinda Rania na imenishinda....alisema Rai.
Mama..hivi kwani ni nani aliekupa hiyo kazi?..aliuliza Dom.
Ni babu yako mzaa baba yako.. Alinipa hii kazi kwa kua mimi nilikua na taaluma ya mambo ya ibada na uganga...alisema Rai.
Babu yangu nani?..aliulza Dom
***"
Huku Rania alikua amefika kwao Dom.. Ile anaingia tu mara yule ndege alikuja na kutua juu ya bega lake.
Rania... Ndege amejileta...alisema Namadi.
Rania alimkamata ndege yule na kumfunga..
Rai kabla hajajibu swali la Dom mara alimwona Rania akiwa amemkamata ndege yule..
Rania.... Alisema Rai kwa mshangao.
Dom aligeuka na kuangalia anakoshangaa mama yake. Alishangaa kumwona Rania akiwa pale.
Rania alipomaliza kumfunga yule ndege miguu na mabawa yake alitembea moja kwa moja hadi kwao Dom kumsalimia mama yake Dom.
Alipogeuka tu kuanza safari ya kwenda kumsalimia mama yake Dom mara alikutanisha macho na Dom.
Alishtuka ila ilibidi ajikaze tu na kwenda alipokua mama yake Dom.
Alifika na kuwasalimia wote Dom na mama yake na baada ya salamu alikaa kwa ajili ya maongezi..
Rania, huyo ndege unampeleka wapi?.aliuliza Rai.
Nina shida nae mama... Anakazi kubwa sana.. Alisema Rania.
Rania alieleza kazi yenyewe kwa mama yake Dom na Dom mwenyewe akiwepo.
Mmmh.. Mpango mzuri ila sio rahisi kuukamilisha...ika hata hivyo Fanya tu utafanikiwa....alisema Rai.
Sawa mama..ukifanikiwa huu mpango hahisi nnitakua nimetatua tatizo la mauaji...baada ya hapo nitaendelea na mipango mingine..alisema Rania.
Jambo jema....Alisema Rai
Baada ya hapo Rania na Dom walikua wakiongea wawili.
Rania, kua makini kwenye kazi yako.. Alisema Dom.
Nitahakikisha nakua makini maana nilikamatwa ni kifo.. Alisema Rania.
Na ndio maana sipendi ufanye hivyo...alisema Dom.
Hata hivyo sitaogopa kifo siku zote ..inabidi nijikaze..alisema Rania..
Dom alimwangalia Rania kwa muda mrefu kwa macho ya huruma kwakua kazi yake ilikua ngumu mno.
Rania.. Nitakusaidia kwa lolote utakalohitaji lililo ndani ya uwezo wangu.... Alisema Dom.
Rania alifurahi kusikia hivyo.
Asante Dom.. Siku zote hua unanifanya nihisi sipo peke yangu.. Alisema Rania.
Ni ngumu kukusaidi kwenye mpango huu wa sasa ila nitakusaidia kuhakikisha unaingia ikulu na mipango yako yote ukiwa ikulu nitashirikiana na wewe .alisema Dom.
Nashukuru sana Dom kwa kujitolea kwako...unanifanya nipate moyo wa mapambano.... Alisema Rania..
Dom alimsogelea Rania na kumkumbatia..Rania nae hakua mbishi..alitoa ushirikiano..
Hakikisha unarudi salama Rania... Alisema Dom huku akiwa amemkumbatia Rania akiwa kifuani kwake.
Nitarudi salama Dom... Niombee nirudi salama.. Alisema Rania kwa sauti ya chini.
Hakika Dom alikua na wasiwasi mkubwa sana juu ya mpango wa Rania.. Aliuona ni hatari sana.
Waliondoka pamoja. Dom alirudi ikulu na Rania alirudi nyumbani akiwa na Namadi.
Usiku ulipoingia Rania na Namadi walifanya kama walivyo panga..
Rania aliingia ikulu kiwiziwizi Akiwa na yale mavazi ya watumishi wa ikulu.
Moja kwa moja alikwenda na chai ya kutosha akavunga kama ametoka nayo jikoni.
Kama alivyopanga...walinzi walisinzia na Namadi akafanya kazi yake..
Walipomaliza walitoroka haraka sana sana
Kesho yake asubuhi hali ilikua mbaya sana ikulu.
Watu walijawa taharuki Baada ya kuona kolokolo kafia lango kuu la kasri.kulikua na mijadala mizito.
Jamani, inamaana kuna mauaji yanaendelea?...walijiuliza watu bila majibu sahihi.
Mfalme.... Mfalme... Kuna kitu kibaya kimetokea.. Alisema omandi baada ya kupata taarifa zile.
Kuna nini?..aliuliza mfalme.
Kolokolo amekufa kwenye lango kuu la kasri... Alisema omandi.
Haaa..nini?.. Aliuliza Mfalme kwa mshtuko nankuamka kwenda kushuhudia
Mfalme hakuamini macho yake baada ya kuona kolokolo amekufa.
Aliogopa sana akijua kua kuna janga litaikumba nchi kama asipoacha mauaji.
Haraka alirudi nyumbani kwake na kukaa huku akihema.
Baba...punguza hofu..huenda ni watu tu wameamua kukuogopesha...alisema Fasha.
Hapana mwanangu.. Ndege huyo hawezi akapatikana na mtu yeyote yule...huyu ndege ni wa maajabu na hua haonekani popote tofauti na kwenye matukio kama haya.. Alisema Mfalme.
Sasa itakua ni hao wazawa wa kelkuni uliowaua ndo imesababisha haya. Alisema Fasha.
Ni kweli.. Hii ni Mara ya pili kutokea ishara hii kwenye utawala wangu.. Mara ya kwanza ilitojea njaa kali sana..na sasa nikiendelea na haya mauaji linatokea janga jingine...alisema mfalme.
Ndio baba...bora uache.. Alisema Fasha..
Mganga.. Unasemaje juu ya hili?..aliuliza Mfalme.
Ninaungana na mwanamfalme.. Alisema mganga.
Walikubaliana kusitisha tabia ya kuwaua wazawa wa kelkuni.
Baada ya hapo mganga alimpelekea malikia suya taarifa zote
Lakini malikia.. Nina wasiwasi kidogo... Alisema mganga.
Wasiwasi upi?..aliuliza suya.
Ndege huyu hawezi kupatikana popote isipokua kwenye matukio kama haya au sehemu anayoishi NADHISH au mtoto au mjukuu halali wa kelkuni.
Hapa yanawez kua mawili.. Inaweza kua ndege huyu kama hapa mwenyewe au kauawa na kuletwa hapa ili kutia hofu ufalme..alisema mganga..
Kwanini unasema hivyo?. Aliuliza malikia.
Kama kuna janga la kutokea hua napata ishara..lakini huyu ndege kipindi hiki ameanguka sijapata hata ishara!!!...alisema mganga.
Kwahyo unahisi ameletwa?. Aliuliza suya.
Bila shaka ameletwa...lakini kama ameletwa...inawezekanaje NADISH au damu ya kelkuni tofauti na Fasha ambae yeye anakinga akanyage hapa na atoke salama?..alijiuliza mganga.
Hapa kutakua na kitu hakiko sawa..alisema malikia.
Lakini dawa nazikagua kila siku ziko vizuri... Alisema mganga bila kujua kilichokwisha tokea.
Hebu nenda kaangalie tena...alisema malikia.
Mganga aliamka haraka na kwenda kuona na kukagua dawa.
*****
Rania, kwahiyo sasa hivi unampango gani?. Aliuliza Namadi.
Rania alikua amekaa kimya ameinamisha kichwa akiwaza.
Nataka kwanza nionane na Fasha. Nataka kujua kama watakua wameacha kuwaua watu kupitia hii mbinu..ikishindwa kufanya kazi nitajua cha kufanya. ..alisema Rania
Na ikiweza je? Aliuliza Namadi
Basi itakua vyema sana..basi baada ya hapo nitaanza rasmi mpango wa kwenda ikulu maana huu ulikua ni wa kuzuia mauaji kwanza.
Utaenda vipi kuishi ikulu?. Aliuliza Namadi
Nataka kwenda Lazi.. Nikaonane na mfalme wa lazi na mwanamfalme Assa mtoto wa malikia wa Lazi
Lazi tena!!!!.. Ukafanye nini?.
Hii ndio njia rahisi ya kuishi ikulu kwa halali halafu bila kushtukiwa... Alisema Rania.
Njia gani hiyo?. Aliuliza Namadi
Ni hivi.. Alianza kusema Rania.
*****
Huku mganga aliwahi kuangalia dawa zake kama ziko sawa
Alifika na kufunua chungu chake cha dawa na kuchunguza kwa uwezo wake wote.
Mganga hakuamini macho yake kwa alichokigundua..dawa zote kwenye chungu zilikua zile zile ila hazifanyi kazi...hii ina maana kwamba kuna mtu aliziharibu..tena kwa kutumia nguvu kubwa mno..
Nini?..hii inawezekanaje?. Alijiuliza Mganga akiwa amechanganyikiwa...ITAKUAJE KWA MGANGA?..
RANIA ANATAKA KWENDA LAZI AKAFANYE NINI?..
USIKOSE SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO