RANIA (22)

Zephiline F Ezekiel
JINA: RANIA
SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI
ILIPOISHIA...
Fasha alipogeuza macho yake alikutanisha macho ana kwa ana na Rania akiwa kama mmoja wapo wa watumishi wa binti mfalme...

Nini???...alijisemea Fasha kimoyomoyo kwa mshangao mkubwa...

SASA ENDELEA..
Rania alipoona Fasha anamwangalia sana aliangalia chini.

Mwanamfalme... Mbona unashangaa sana?..aliuliza jao kwa sauti ya chini.

Aaa..hamna kitu.. Alisema Fasha huku akionekanankabisa kuna jambo linalomsumbua.

Walifanya mapokezi vizuri bila tatizo lolote..

Kuanzi siku hiyo Rania aliishi ikulu kama mtumishi wa Mars binti mfalme na mke mtarajiwa wa Fasha.

Kesho yake asubuhi mwanamfalme akienda kumsalimia mchumba alikutana na Rania mlangoni.

Baadae unione...alisema Fasha na kuingia ndani.

Rania hakujibu kitu..aliendelea na kazi zake.

Baadae kama walivyokubaliana walionana kwenye sehem ya faragha ya mwanamfalme.

Rania... Kwanini umenifanyia hivi?.. Aliuliza Fasha.

Nimekufanyia nini kibaya sana mwanamfalme?... Aliuliza Rania.

Tuseme kwamba hujui ulichonifanyia?..aliuliza mwanamfalme..

Rania aliikaa kimya.

Rania.. Hata kama hunipendi ni sawa..Kwahiyo hiyo haitoshi ukaona uje uwe mtumishi wa mtu nitakae muoa ili uje uniumize zaidi?..aliuliza Fasha kwa uchungu.

Ningefanya nini basi?..hii ndio ilikua njia pekee ya mimi kuweza kuishi ikulu.. Alisema Rania.

Rania... Hebu fikiria maumivu ninayoyapata nikiwa nakuona wewe unaambatana na mke wangu kila unapoenda...alisema Fasha.

Nisamehe sana mwanamfalme...ungenisaidia kukaa hapa kwa njia yako nisingefika hapa nilipo... Alisema Fasha.

Fasha alikaa kimya kwa muda huku akimwangalia Rania.

Ni kweli.. Haya nimeyataka mwenyewe.. Ningekusaidia tangu zamani kuishi ikulu kama ulivyoomba haya yote yasingetokea...alisema mwanamfalme huku akifuta machozi yaliyokua yakimtoka..

Rania aliumia moyoni mwake kwa jinsi Fasha alivyokua..alihisi amekosea sana lakini nafsi nyingne ilimwambia kua yuko sahihi...

Rania aligeuza mdogo mdogo na kuanza kuondoka.

Fasha alimshika mkono kumzuia asiondoke pale.

Kabla Rania hajakaa sawa Fasha alimvutia kifuani kwake na kumkumbatia kwa nguvu na hisia nzito.

Rania,mimi sitakutoa moyoni mwangu hata siku moja.. Kaa ukijua hilo Rania... Alisema Fasha.

Rania alikua amekodoa macho muda huo akiwa hajui la kufanya..

Wakati hayo yote yanaendelea Dom alikua akiwaona kwa mbali.. Roho yake iliuma sana..pale mwanamfalme alipomkumbatia Rania ndo aliumia zaidi na kuamua kuondoka ili asiumie zaidi.

Baadae Fasha alimwachia Rania..Rania kwa woga aliondoka haraka sana.

Muda huo Mars alikua tayari alishaanza kumtafuta Rania

Rania aliwahi sana..alitembea haraka kama anaumwa kuhara😸.

Akiwa njiani anatembea bila kuangalia mbele mara alimparamia Dom aliekua amesimama..

Rania alishtuka baada ya kumparamia mtu..ile alipoinua macho kuangalia ni nani amemparamia alikuta ni Dom.

Kwanini hukuniambia mpango wako Rania... Aliuliza Dom.

Nisamehe sana Dom.. Nilijua fika kua huwezi kukubali niende Lazi kwa kuhofia usalama wangu na ndio maana sikukwambia..alisema Rania.

Ni njia nzuri umetumia kuingia ikulu.. Ila jitahidi kuchunga mienendo yako na mwanamfalme usije ukagundulika..alisema Dom.

Rania alishtuka kidogo baada ya Dom kusema vile..alihisi kua Dom atakua amewaona..

Dom.. Nisamehe....alisema Rania kwa sauti ya chini.

Haujafanya kibaya chochote Rania... Kua na amani tu na mimi..ukianza mkakati mwingine nijulishe nikusaidie...alisema Dom.

Sawa Dom.. Nashukuru sana...alisema Rania kisha akaanza kuondoka.

Dom alimsindikiza Rania kwa macho hadi alipoishia.

Rania.. Kumbuka kwamba hapa ikulu nimekuja kwa ajili yako tu na si vinginevyo..alijisemea Dom huku akimsimdikiza Rania kwa macho.
***

Omandi,maandalizi ya harusi yanaendeleaje?..aliuliza Mfalme.

Yanaendelea vizuri chini ya uangalizi wa malikia.. Alisema mfalme.

Omandi... Nina maadui wawili wakubwa ninaopambana nao..Alisema mfalme

Najua NADISH, kuna nani mwingine nae ni nani?..aliuliza omandi.

Ulishawahi kujua kwanini mapenzi yangu kwa malikia yalipungua na hata mambo yangu ya siri simwambii?...aliuliza mfalme.

Hua najiuliza ila sijawahi kupata majibu sahihi..alisema omandi.

Malikia wangu anatamaa sana.nimeshamwona tu.. Anampango wa kuniua ili amuweke Fasha ili kwamba apate nguvu maana mimi namtenga mbali... Alisema Mfalme.

Omandi alishangaa sana kusikia hivyo

Kwahyo anashirikiana na Fasha?.. Aliuliza omandi.

Hapana.. Hashirikiani nae..wala Fasha hajui.na ninavyomwona Fasha hana habari na mambo ya ufalme kabisa...alisema Mfalme.

Sasa tutafanya nini Mfalme wangu?.. Aliuliza omandi.

Muite Fasha hapa...alisema Mfalme.

Ndio Mfalme... Alisema omandi.

Baada ya muda mfupi Fasha alikua tayari alishafika.

Baba..unajisikiaje?..aliuliza Fasha.

Hali yangu sio mbaya sana...alisema Mfalme

Fasha mwanangu...aliita Mfalme.

Naam baba..aliitika Fasha.

Muda sio mrefu utakua Mfalme wa Tharia... Naomba uwe makini sana na mama yako.. Nahisi na wewe unamjua...alisema mfalme

Hilo nimeweka akilini baba...alisema Fasha

Halafu hakikisha mkeo anakua chini ya uongozi wako sio wa mama yako..mama yako anamaana yake kukuozesha kwa huyo binti.. Angalia asije akamtumia mkeo kukuendesha....alisema Mfalme.

Sawa baba nimekuelewa..alisema Fasha.

Baada ya maongezi hayo na baba yake Fasha alitoka na kwenda nje.huko alikutana na mama yake.

Mwanangu..ninaimani umefurahia ndoa hii..binti huyu ni mrembo sana.. Bila shaka atakufaa..alisema malikia.

Fasha hakujibu kitu maana hakupendezwa na kauli za mama yake..

Muda ulisonga mbele...siku ya harusi ya Fasha iliwadia.

Maandalizi yalifanyika vizuri na ndoa ikawiva.

Muda wote Fasha alikua akimwangalia Rania tu..hakua na furaha hata kidogo na ndoa yake ile.

Rania alikua pale kama mtumishi wa Mars na mhudumu wa bi harusi.

Ulifika wakati wa Fasha kumvisha pete Mars.

Fasha aligeuka pembeni na kumwangalia Rania.. Hakuamini moyoni mwake kama ndo anaoa na Rania hatakua wake tena.

Daaah..Fasha alijikuta anatoa machozi kwenye tukio lile la kihistoria.

Mama na baba yake na watu waliomwona vizuri pamoja na Mars walimshangaa Fasha.. Haraka wapambe walivungankama wanamfagilia kumbe wanafuta machozi yake

Rania alijisikia vibaya sana... Ilibidi aondoke maeneo yale ili Fasha angalau asiumie sana

Dom nae hakua mbali.. Alimwona Fasha alipodondosha machozi hadi akamhurumia ingawa wanashea.

Namadi.. Mwanamfalme anatia huruma sana...alisema Dom akimwambia Namadi ambae pia alihudhuria harusi.

Kwanini.. Halafu mbona amelia?..aliuliza Namadi.

Anampenda mtu mwingine tofauti na anae muoa...inauma sana lakini ndo mambo yenyewe ya ufalme.. Alisema Dom.

Mars alijisikia vibaya kwa alichokionesha Fasha..

Baada ya ndoa Fasha alikua amekaa na mkewe Mars.

Fasha... Hata kama hunipendi huwezi kunifedhehesha hivyo mbele za watu...alisema Mars.

Fasha alikaa kimya tu wala hakujibu kitu maana alikua na mawazo mengi tu kichwani.

Fasha naongea na wewe... Alisema Mars huku akimvuta Fasha.

Fasha alikua kimya tu.

Nitamtafuta huyo ulietoa machozi kwa ajili yake nimuone yeye ananini kunizidi...alisema Mars.
*****

Rania, kwahyo mpango wako wa pili ni upi?..?aliuliza Dom.

Kwa sasa nataka nijue nguvu ya ufalme imesimama wapi.. Nataka nijue kitovu cha nguvu ya utawala huu na pia nijue udhaifu wao uko wapi...alisema Rania.

Sawa Rania.. Basi tugawane majukumu...alisema Dom.

Lakini Dom mimi nina wasiwasi Fasha atakavyokua..alisema Rania.

Ingawa simwamini sana.. Ila sizani kama atabadilika..mwanamfalme ni mtu mzuri upande wako..alisema Dom.

Sawa..mimi nitatafuta kujua udhaifu wao..wewe tafuta nguvu yao..alisema Rania.

Sawa..nitafanya hivyo..

****************MIEZI MITANO BAADAE***********

Rania alikua ameshafanya uchunguzi na kugundua kua kuna mpasuko ndani ya familia ya kifalme.. Ila hakua na uhakika sana...alihitaji kufanya uchunguzi zaidi.

Rania alikua anatoka zake kutembea.. Mara alipokua chodo alisikia sauti za watu wanaongea kwa chini sana..

Alibana na kuanza kuwasikiliza.

Dasu(jina la mganga)..kumbuka jambo hili ndo la kutunza zaidi..hakikisha kamwe Mfalme hajui kua mimi na wewe ni ndugu.. Akijua tu tumeisha..alisema malikia.

Sawa dada.. Nalizingatia hilo..sisi njia yetu moja...alisema mganga Dasu.

Pia hakikisha Mfalme anaendelea kukuamini na ujifanye hushirikiani na mimi maana hicho ndio mfalme anapenda na anaamini iko hivyo.. Alisema Suya.

Sawa malikia... Alisema Dasu.

Haaa...kumbe malikia na mganga ni ndugu na wanashirikiana kumwangusha mfalme!!!... Alijisemea Rania.

Hapa tayari uchunguzi wangu umekamilika...alijisemea Rania kisha akaondoka kwa kunyata.

Baadae Dom na Rania walikutana kujadili mambo yao na mipango yao.

Kwahiyo umeshagundua nini Rania... Aliuliza Dom.

Kwanza ufalme huu una ufa...alisema Rania.

Kiaje?..aliuliza Dom.

Yaani ndani ya ufalme kuna matabaka...malikia ana watu wake na mipango yao ya kumwangusha mfalme muda huohuo wakimuwinda Rania.Mfalme nae ana watu anaoshirikiana nao mambo yake ikiwemo kuniwinda mimi...alisema Rania..

Haya na wewe sema ulichokipata..alisema Rania.

Nguvu kubwa ya hapa wanategemea jeshi..alisema Dom.

Kwakua hatuwezi kulidhoofisha jeshi basi hatutakiwi kutumia mbinu za kijeshi kwenye mambo yetu... Alisema Rania.

Hii kazi inatakiwa iishe ndani ya miaka mitano maana kama alivyosema mama yako kwamba laana ya yule ndege inaaminika kuisha ndani ya miaka mitano.. Kwahiyo miaka mitano ikiisha wanaanza tena kuwaua wazawa wa kelkuni.. Alisema Rania.

Ni kweli... Itabidi ufumbuzi ufanyike kabla miaka mitano haijaisha....alisema Dom.

Kabla hatujafanya chochote kwanza inabidi tutambue kwamba hapa tunapambana kuutoa utawala kwa hii familia na kuurudisha kwa watawala halali ili kunusuru maisha ya wazawa wa kelkuni. kwakua huu utawala unakusudia kuwaua.

Sasa baada ya kuwatoa atatawala nani?..aliuliza Rania.

Hilo kweli hatujalizingatia kwakweli..sasa tufanye kitu kimoja.. Mama atakua anajua haya mambo angalau kidogo,twende tukamuulize kama kuna familia yoyote ya Mfalme Kelkuni anayoifahamu iliyobakia na ina watoto wakubwa...alisema Dom.

Sawa..basi kesho tutaondoka maana sio zamu yangu kumhudumia malikia... Alisema Rania.

kesho yake waliondoka na kuelekea kwao Dom ingawa kwa kutoroka.

Huku mama yake Dom nae alikua akiwaza

Habiri baba yake Dom pamoja na mama yake Rai wote alikua ukoo wa kelkuni..Kwahiyo Dom na Fasha walikua wa kelkuni.

Malikia suya alijua Fasha ni damu ya ukoo wa kelkuni lakini alimwamuru mganga akamwekea kinga kiasi kwamba hawezi kudhurika na dawa ambayo Mganga aliiweka ili familia ya kelkuni wakikanyaga tu ikulu wakaripuka..

Kwa upande wa Dom yeye aliwekewa hiyo kinga na mama yake tangu akiwa mdogo maana mama yake alijua kilichokua kimetegwa ikulu na huenda kwa namna yoyote ile Dom atakanyaga ikulu.. Kwahyo hata Dom hakuweza kudhurika.

Baba yake Dom ndie alikua mtu wa karibu zaidi na mfalme kelkuni maana Mfalme alikua mjomba wake.

Akiwa kwenye mawazo juu ya hatima ya mwanae wa pekee Dom mara alisikia mlango ukigongwa

Alipofungua tu alikutaba na Dom na Rania.

Aliwakaribisha kwa furaha wakaingia ndani. Baada ya maongezi ya hapa na pale Dom alihitaji kusema shida yao halisi.

Mama...nina jambo nahitaji kukuliza mama yangu.. Alisema Dom..

Sawa uliza..alisema Dom.

Kuna mtu yeyote wa familia ya kelkuni ambae yuko hai na ni mtu mzima?.aliuliza Dom.

Mbona umeuliza hivyo Dom?.. Aliuliza mama yake.

Mama...kama unavyojua.. Baada ya huu utawala wa kuondoka madarakani anatakiwa kuwepo mtawala mpya, tena wa familia ya kelkuni.. Sasa atakua nani huyo?.. aliulza Dom.

Kiukweli waliokua wamebakia alikua ni yeye na Fasha tu ingawa Rai hakujua kuhusu Fasha.

Rai alitambua kua Dom ndo aliebakia maana wengine hawakujua habari za ikulu wala NADISH.. Dom peke yake ndie alifaa.

Rai alipata kigugumizi juu ya lile jambo.. Alijiuliza aseme au la..

USIKOSE SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU

TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni