
SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU
ILIPOISHIA...
Kiukweli waliokua wamebakia alikua ni yeye na Fasha tu ingawa Rai hakujua kuhusu Fasha.Rai alitambua kua Dom ndo aliebakia maana wengine hawakujua habari za ikulu wala NADISH.. Dom peke yake ndie alifaa.
Rai alipata kigugumizi juu ya lile jambo.. Alijiuliza aseme au la...
SASA ENDELEA..
Mama...aliita Dom baada ya kuona kua mama amekaa kimya muda mrefu.Mwanangu...wewe ni damu ya ukoo wa mfalme kelkuni....alisema Rai.
Mimi?..alisema Dom macho yamemtoka.
Ndio mwanangu... Wewe ni damu ya kelkuni.. Mimi na baba yako wote ni ukoo wa mfalme aliepinduliwa..alisema Rai
Ulipokua mdogo nilikuwekea kinga juu ya dawa iliyowekwa ikulu ya kuwaua uzao wa kelkuni pindi tu wanapokanyaga ikulu..... Kwahyo Ndio maana hata ulipoenda ikulu hakuna kibaya kilichokukuta..alisema Rai.
Dom na Rania wote walibaki wanashangaa..
Mama..kwangu mimi haitawezekana kwamba niwe kiongozi maana siwezi kukosana na Fasha sababu tu ya madaraka...alisema Dom.
Sasa kwanini umlinde mtu alie katika njia moja na watu wanaoua kizazi chako?...aliuliza Rai.
Mama..mwanamfalme hayuko hivyo.. Halafu isitoshe..alisema Dom kisha akasita kidogo.
Nini?..?aliuliza Rai baada ya kuona Dom anasita.
Sio mtoto halali wa Mfalme... Alisema Dom.
Nini?.. Sio mtoto wa mfalme?.. Unamaana gani kusema hivyo mwanangu?.. Aliuliza Rai.
Huo ndo ukweli wenyewe mama...Fasha sio mtoto halali wa Mfalme wala sio mtoto wa malikia...alisema Dom.
Wewe ulijuaje?...aliuliza Rai.
Fasha mwenyewe ndo alisema... Alisema Dom
Rai alibaki kinywa wazi asijue cha kusema.
Baada ya muda mrefu wa kushangaa Rai alisema..
Nazani hii itakua njema zaidi... Kwakua Fasha sio mtoto wa Mfalme basi wewe utakua mtawala..
Nitakua mtawala kama Fasha akiridhia...maana najua chini ya utawala wake hakutakua na uonevu huu..alisema Dom.
Wewe unawaza Fasha tu..vipi kuhusu wengine?.. Kama Fasha akifa na akatawala mwingine unazani na yeye atakua kama Fasha?.. Aliuliza Rai.
Dom alikaa kimya kidogo maana ni kweli kilichosemwa na mama yake.
Fasha anaweza kua mtu mzuri lakini waliomzumguka wakawa wabaya.. Mfano mama yake malikia suya.. Vile vile haijulikani kama atakae tawala baada ya fasha atakua na tabia gani.. Huenda nae akawa na masimamo wa kuwaua watu wa kelkuni... Aliwaza Dom akajikuta anashindwa cha kusema.
Dom... Kwahiyo kama angekuepo mwingine wa kutawala tofauti na wewe ungekua huru kupambana?. Huoni kwamba hata hapo pia ungekua unashindana na Fasha?... aliuliza Rai.
Ni kweli... Alisema Dom.
Haya kumbe mnatakiwa kupambana kabla Fasha hajatawala maana hamtakua na ali ya kupambana na Fasha kwa kua ni mtu wenu wa karibu
Ngoja tumshirikishe Fasha katika hili ili ajue yote.. Alisema Rania.
Fasha tena!!!...alisema Rai kwa mshtuko..
Ndio mama....hii ndio njia nzuri..alisema Rania.
Walikubaliana na wakaondoka na kurudi ikulu.
Kesho yake walimwita Fasha na kumweleza yote waliyojadili.
Fasha alishtuka kidogo kusikia Dom ni ukoo wa kelkuni..
Dom kama wewe ni damu ya kelkuni imekuaje umeweza kuishi hapa bila tatizo?.. Aliuliza Fasha.
Dom alimweleza Fasha kua alikingwa na mama yake toka utotoni.
Mmh....huyo mama yako ni Mtu wa namna gani?.. Aliuliza Fasha.
Mama aliwahi kua msaidizi wa mganga aliekufa zamani...alisema Dom..
Atakua anajua mengi kuhusu ikulu....Alisema Fasha
Dom.. Huu utawala sio wangu.. Kwa sasa mpango nilionao ni kuwatafuta wazazi wangu wala sio mambo ya ufalme.. Kwa sasa mfalme yuko vizuri kiafya...atatawala mwenyewe... Alisema Fasha
Hata mkifanikisha azima yenu msimuue baba na mama yangu walezi tafazali.. Mimi nitawachukua na nitahakikisha hawaleti tatizo..najua haipo njia nyingne ya kuwalinda watu wenu tofauti na hii ya kuutoa ufalme huu maana ndo ilivyotabiliwa maana Mfalme hatakubali wabaki hai hata iweje...alisema Fasha.
Sawa mwanamfalme ...alisema Dom.
Wakati Dom,Rania na Fasha wakieendelea kuongea huku majadiliano kati ya malikia na mganga yaliendelea.
Dasu. .muda unakwenda sasa na hakuna tunachokifanya.kwanza hujajua nani alieitegua dawa na ile na hata nadishi hujamjua ..kazi yako ni nini hasa?..aliuliza suya kwa ukali.
Malikia sio kwamba nakusudia kutokamilisha hii kazi...tatizo ni kwamba anaeshindana na sisi hatumjui ila yeye anatujua na hata hivyo ananguvu sana...alijiteta mganga
Sasa kwahiyo una mpango gani?.. Aliuliza malikia.
Malikia.. Kama unavyojua Fasha ni ukoo wa kelkuni.. Nikisema nitengeneze dawa mpya inabidi kumkinga Fasha upya..unazani utamweleza nini Fasha ukitaka kumkinga?..aliuliza mganga.
Kwani hakuna njia nyingne ya kumkinga tofauti na kumfukizia moshi?...aliuliza malikia.
Labda kumwekea kwenye chakula...ila hii itampelekea kuugua sana ingawa hatakufa.. Alisema mganga.
Malikia alichanganyikiwa kusikia hayo..
Sasa wewe unashauri tufanye nini?..aliuliza malikia.
Inabidi tu tupambane kumjua alieitegua maana huyo ndie hatari zaidi hata ya wazawa mia moja wa kelkuni.
Kwahyo kuna uwezekano wa kumjua huyo Mtu?.. Aliuliza malikia.
Nikifanya ibaada ya kama mwezi mzima kwa uwezo wangu wote naweza kumjua mtu huyo..alisema mganga.
Unasubiri nini?..kamuage mfalme ukafanye hiyo ibaada.. Alisema malikia.
Mganga aliondoka na kwenda kumwambia mfalme juu ya mpango ule.
Mfalme alimpa ruhusa na kumsihi ajitahidi sana apate ufumbuzi.
*******
Huku maongezi kati ya Dom, Rania na Fasha yaliendelea.
Kwahyo mtatumia mbinu gani kuutoa ufalme bandia?...aliuliza Fasha.
Kwakua hatuna nguvu za kijeshi tutatumia mbinu yoyote itakayomfanya mfalme aachie madaraka yeye mwenyewe.. Alisema Rania.
Ndio mbinu gani hiyo?..aliuliza mwanamfalme.
Mwanamfalme sijui kama utaridhika na hili..ila mimi nimepanga hivi.
Nimeshagundua malikia anataka kumuua Mfalme ili wewe utawale maana Mfalme hampi nafasi ya kusema neno kwenye hii nchi ndo maana anataka wewe uingie haraka kwakua wewe ni mtoto wake basi utampa nguvu na madaraka makubwa kwenye hii nchi na atakutumia wewe kukamilisha matamanio yake.
Pia malikia anataka hili lifanyike mapema maana umri wake unaenda..kwahyo anatakiwa kufaidi juhudi zake kabla hajazeeka..alisema Rania.
Najua hilo Rania... Kwahyo utafanya nini juu ya hili?.?aliuliza Fasha.
Mwanamfalme.. Mfalme hajajua jambo moja tu...amiri jeshi ni Mtu wa malikia.. Kwahyo kwenye upande wa jeshi mfalme hana chake....kwahyo kama wakisema waanze uasi..mfalme atauawa mapema sana....alisema Dom kisha akaweka kituo.
Nini?...aliuliza Fasha kwa mshangao..
Sio hivyo tu..hata Mganga ambae ni mtu anaeaminiwa sana na mfalme ni mtu wa malikia... Mfalme amezungukwa na nyoka kila kona...aliongeza Rania.
Mmmh....hivi kumbe kuna mambo humu siyajui....alisema Fasha kwa mshangao.
Cha mwisho....mganga ni ndugu wa damu wa malikia... Alisema Rania...
Fasha hakuamini aloyoyasikia...kiukweli yalikua mageni machoni mwake.
Kwahyo mtafanya nini juu ya hili?..aliuliza Fasha.
Kwakua malikia na kundi lake ndo waananguvu basi hatuna budi kumwangusha malikia kwanza..ni rahisi kumwangusha kwa sasa kwasababu hajashika nguvu ya utawala bado... Alisema Rania.
Hatuna nguvu ya kijeshi..kwahyo tutamwangusha kwa mbinu zisizo kua za kijeshi... Alisema Rania.
Zipi?..aliuliza Fasha.
Nina mpango mmoja....najua hadi leo hawajawahi kujua nani alitengua yale madawa waliyokua wameyaweka kunikamata mimi na uzao wa kelkuni.....kwahyo wanahofu nani alifanya hivyo....alisema Rania.
Ni kweli..hawamjui na wanamwogopa sana kiasi kwamba hadi Mfalme alipoteza fahamu baada ya kusikia ametegua dawa yao.... Na hata sasa hivi Mganga ameenda kufanya ibaada ya mwezi mzima kumtafuta huyo mtu....alisema Fasha.
Rania alishtuka..hata hivyo Dom alimtoa wasiwasi kua hawataweza maana kinga aliyowekewa ni kubwa sana.
Baada ya kushusha pumzi Rania aliendelea..
Sasa ninanitaji kuandika ujumbe na kuupeleka kwenye makazi ya Mfalme...
nitaandika kwamba ""Mfalme asiwaze tu juu ya kumtafuta NADISH bali cha kwanza ashughuliikie watu wanaomzunguka ambao wanasubiri Mfalme awamalizie tatizo la NADISH halafu wao wamuue Mfalme na wajitawale huru bila wasiwasi..na wengine ni wale anaowaamini sana.
Sitawataja mimi..ila inabidi uwatafute wewe kama wewe ili uwe ha hakika...najua kua kuna baadhi unawajua..ila nikujulishe...kuna wengi usiowajua wala kuwazania..wanakusaliti na wanamambo mengi ya siri usiyoyajua....ukiwapata hao basi hautashinswa kuipata NADHISH pamoja na mtu hatarishi aliitegua dawa yenu.. Usiwaze sana kua Mimi ni nani...utanifahamu siku chache sana zijazo""
Nitaandika hivyo... Alisema Rania
Mmmh...utaweza?...aliuliza Fasha.
Naamini nitaweza...najua baada ya huo ujumbe Mfalme atahitaji kujua alieupeleka ujumbe ila hata hivyo atahitaji kujua ni nani hao wanaomsaliti tofauti na malikia anaejua kua nu msaliti tangu mwanzo.
Mfalme ni mtu wa hasira sana kwa ninavyomwona..watu wa hasira Siku zote hawawazi upande wa pili wa shilingi...kwakua anajua kua malikia anamsaliti basi atataka kujua zaidi na wengine wanaoungana na malikia kuliko kuwaza ni nani kaleta barua na ni kwanini ailete na anayajuaje haya.. Alisema Rania
Hata kama atanitafuta...ila hata wao atawatafuta...nanatawajua iwe isiwe...alisema Rania.
Sawa... Ni mpango mzuri.
Lakini Rania utanisamehe kwakua mimi sitashirikiana na wewe kwa ukaribu kuupindua ufalme wa mtu alienilea kama mwanae..nakutakia kazi njema...alisema Fasha.
Hilo halina tatizo mwanamfalme.. Hata kunihifadhi hivi ni msaada tosha...alisema Rania.
Kama walivyopanga...Rania aliiandika barua ile na kujiandaa kuipeleka..
Rania aliwaza kua itakua ngumu kuifikisha moja kwa moja kwa Mfalme bila kukamatwa..
Usiku ulipofika Rania alivaa mavazi ya walinzi wa jumba la kifalme aliyoyaiba kwa msaada wa Dom na kujichanganya ba walinzi wale...
Alikua anavunga kuzunguka zunguka kama mlinzi kweli hadi alipopata sehemu ambayo kuna dirisha la chumba cha Mfalme
Kwa bahati nzuri mfalme na omandi walikua wako nje wanaongea..Rania aliona hiyo ndio nafasi nzuri ya kufanya uharifu wake..
Taratibu aliitioa ile karatasi na kuanza kuipitishia dirishani..?
Ile anaiweka tu mara alishtuka kusikia.....
USIKOSE SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO