RANIA (28)

Zephiline F Ezekiel
JINA: RANIA
SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE
ILIPOISHIA...
Kumbuka kitu kimoja....nitakusaidia kwenye kua mfalme lakini kwa shariti moja...alisema suya.

Lipi hilo?...

Utanifanya malikia wako...alisema suya..

Hilo halina shida... Alisema mkuu wa majeshi.

Waliagana na mkuu wa majeshi akaondoka.

Njia nzima mkuu wa majeshi alikua akiwaza juu ya kumuua Fasha....

SASA ENDELEA..
Baba..naomba ruhusa nifanye kitu kimoja... Alisema Fasha akimwambia mfalme.

Sema mwanangu... Alisema Mfalme.

Naomba nikaonane na mama mmoja huko nje ya ikulu.. Alisema Fasha.

Kwanini?..aliuliza mfalme.

Kwa sasa ninataka niwafahamu wazazi wangu..wawe wako hai au wamekufa...sasa huyo mama anaonekana kua na ujuzi na mambo mengi hapa ikulu... Alisema Fasha.

Ni nani huyo?.. Aliuliza Mfalme.

Simfahamu jina ila kuna mtoto wake yuko hapa ikulu anafanya kazi...ndo nimemfahamu huyo mama kupitia kwake....alisema Fasha.

Mmh...haya nenda... Alisema Mfalme.

Nashukuru baba kwa ruhusa yako...alisema Fasha.

Baada ya hapo Fasha alikwenda kumtafuta Dom na kumwomba ampeleke kwa mama yake ili aanze uchunguzi wake rasmi.

Huku malikia suya na Mganga walikua wakiendelea na mipango yao...

Malikia.. Je ikitokea Bakanga akashindwa kumuua Fasha inakuaje?...aliuliza Mganga.

Ni kweli, bakanga anawezaa shindwa kumuua Fasha.. Kama ikishindikana basi tutaifanya hii kazi sisi wenyewe na majeshi yetu ya siri...alisema malikia.

Kitu kimoja muhimu sana...baada ya bakanga kumuua Fasha hata yeye nae lazima tumuue..kwa ninavyomjua Bakanga amekubali tu kwa sasa..ila kama akiyapata madaraka ya ufalme wala hatakidhi mahitaji yangu.. Alisema malikia.

Ni kweli... Tunamtumia tu lakini tukifanikisha na yeye tutammaliza...alisema Mganga.

Kwa sasa nahitaji kufanya utaratibu wa kupata majeshi kutoka Lazi ambayo yatatusaidia ilitokea ufalme ukashindikana kwa njia ya kawaida.

Unazani Mfalme wa lazi atakubali?..aliuliza Mganga.

Kwa ushawishi wa binti yake Mars atakubali tu... Alisema suya.

Leo usiku nahitaji kukutana na Mars ili niongee nae juu ya hili swala...alisema suya.

Sawa nitawataarifu vijana Wangu wakamfuate ikulu na wamsindikize hadi hapa huyo Mars.

Dom na Fasha waliondoka kuelekea kwao Dom majira ya usiku hivi. Rania hakuongozana nao... Alibakia ikulu.

Rania akiwa nje mara alimwona mtu anaongea na Mars kwa siri.. Alijibanza kusubiri kinachofuatia.baada ya muda Mars alitoka na mtu yule wakatoka nje ya ikulu.

Rania alianza kuwafuatilia kwa nyuma aone wataelekea wapi.

Aliwafuatilia watu wale akizani kua wapo wawili tu kumbe kuna na wengine wamejificha msituni ili kwamba kama kuna mpelelezi anawafuata wamshughulikie.

Rania aliwafuata muda mrefu hadi wakafika mbali kidogo.

Kumbe wakati huo Rania anawafuatilia kulikua na watu wanamchora tu..

Akiwa anaendelea kuwafuatilia Mara alishtukia anakabwa kwa nyuma na watu asio wajua...

Alipiga kelele mara moja tu kisha akawekewa dawa puani iliyomfanya apoteze Fahamu.

Huku Dom aliisikia saut ile.. Ilifanana sana na sauti ya Rania iliyokua ikiomba msaada siku ile alipokua amekamatwa na wale vijana..

Fasha... Nimesikia kitu... alisema Dom.

Nini umesikia?..aliuliza Fasha.

Nimesikia sauti ikipiga kelele za msaada ila imesikika mara moja na kutulia...alisema Dom kisha akaweka kituo.

Ila mbona inafanana sana na ya Rania?.alisema Dom.

Nini?.. Rania?.. Amefikaje huku?.. Aliuliza Fasha.

Sina hakika ila sauti kama ya Rania... Alisema Dom.

Kwahiyo Rania alikua anatufuatilia? Hatuamini?..aliuliza Fasha.

Hapo sijajua.. Ila nimemsikia humu humu msituni.. Alisema Dom.

Walikubaliana kufuatilia ilikosikika sauti.

Walitembea kwa tahadhari kubwa sana.

Mbona hakuna kitu.. Alisema Fasha baada ya kutembea muda mrefu bila mafanikio..

Ona wale pale... Alisema Dom baada ya kuona watu kama wanne wakiwa wamebeba mtu begani..

Haaa...watakua wamemfanya nini?..alisema Fasha kwa wasiwasi mkubwa.

Tuwafuatilie...alisema Dom.

Waliwafuatilia watu wale kila walikoenda.

Muda huo Mars na yule mpambe mmoja walikua wamepita njia nyingne baada ya kutaarifiwa kua kuna mtu kakamatwa anawafuatilia.

Wale watu walitembea hadi wakafika kwenye kambi aliyokuwemo suya na Mganga.

Huku Fasha na Dom nao walikua wameshafika pale ingawa walikua walikua wamejificha.

Suya na Mganga wakiwa ndani mara aliingia Mars.

Karibu ukae..alisema malikia suya baada ya kumwona Mars.

Mars nimekuitia jambo moja hapa... Alisema suya.

Lipi hilo malikia....?Aliuliza Mars.

Kabla suya hajaongea waliingia wale wapambe wakiwa wamembeba Rania.

Na huyu ni nani?...aliuliza suya.

Malikia.. Huyu alikua anatupeleleza...alisema mpambe mmoja.

Mleteni hapa halafu mumfunue nimwone...alisema malikia suya.

Walimsogeza Rania na kumfunua sura yake.

Mars alishtuka baada ya kumwona Rania.

Mars umemfahamu huyu?.. Aliuliza malikia baada ya kumwona suya akiwa ameshituka.

Ndio...ni mmoja wa watumishi wangu niliotoka nao Tharia.

Sasa hapa imekuaje?..aliulza malikia.

Huenda atakua ametumwa na Fasha maana huyu ndie yule aliemfanya Fasha akadodondosha machozi siku ua ndoa...atakua anafahamina na Fasha huyu...alisema Mars.

Sasa Fasha anajuaje mipango yetu?..aliuliza malikia.

Hapo sasa sijui..Alisema Mars.

Nendeni mkamfunge kwenye mti wa mateso...akizinduka tu anzeni kumsulubu kisha mumlazimishe aseme ukweli nani kamtuma..aliamuru suya.

Sawa malikia... Walisema wapambe na kwenda kumfunga Rania.

Huku Fasha na Dom walikua karibu pale kwenye kambi ila walikua bado hawajajua Rania amepelekwa sehemu gani maana kambi ilikua kubwa.

Rania alipelekwa kwenye mti wa mateso akafungwa hivyo hivyo amezimia.

Baada ya ile dawa kuinshiwa nguvu alizinduka.

Rania alishtuka kuona amefungwa kama mwili mzima kwenye mtu

Nimefikaje hapa?. Alijiuliza Rania kwa woga.

Alipoinua kichwa chake alishangaa kuona watu wanne wako mbele yake.Rania alishtuka sana.

Mtu mmoja alimsogelea na kumuuliza..nani amekutuma?...

Sijatumwa na mtu.. Alisema Rania.

Yule mtu alitabasam kwa dharau..kisha akatoa amri.

Piga!!!!!.

Rania alianza kupokea kipigo kikali sana...walimpiga kwa minyororo mizito

Damu nyingi alianza kumtoka Rania kwenye majeraha aliyoyapata kutokana na kipigo cha minyororo..

Hakuweza kutoa sauti maana alipotaka kupigwa walimziba mdomo kwa kitambaa.

Sema nani kakutuma?..aliulza mpambe huyo kwa mara nyingne.

Sijatumwa na mtu..nimekuja mwenyewe... Alisema Rania.

Anatuletea dharau huyu...leteni maji yenye pilipili ya kutosha..atasema ukweli tu huyu... Alisema mpambe huyo..

Wapambe wengine walileta maji yenye pilipili ya kutosha na kuanza kumwagia Rania sehemu zote zenye majeraha.

Rania alisikia maumivu yasiyo ya kawaida... Alihisi anakufa muda huo.

Waliendelea kumpiga na kumwagia maji yenye pilipili .

Dom na Fasha muda huo walikua wanatafuta Rania huku na kule...hatimaye walimwona.

Maskini Rania alikua katika hali mbaya sana... Alikua kama mtu anaekata roho muda huo..

Dom alitaka kufuatuka aende ila Fasha alimzuia..

Usiwe na presha Dom... Tukikurupuka hapa tunaweza kushindwa kumsaidia Rania na sisi wenyewe tukakamatwa..alisema Fasha.

Wakiwa wanaangalia mara suya na wapambe wake walifika.

Ameshasema ukweli huyo?... Aliuliza suya.

Hapana....hajasema kitu....

Binti utakufa hapa usiposema ukweli.. Na aliekutuma hata hatakuja kukusaidia..ni bora useme...alisema Suya.

Fasha na Dom walishangaa kumwona suya pale.

Kumbe ni huyu Suya ndo amefanya haya...alisema Fasha huku hasira zikimpanda.

Hata sasa hivi mwanamfalme aliekutuma hajaja kukusaidia.. Huoni kua utakufa hapa?.. Alidakia Mars.

Fasha alishtuka kusikia sauti ile.. Aliitambua kua ni ya Mars.alipoangalia vizuri alimwona Mars pale.

Mars???!!!...alisema Fasha kwa mshtuko.

Mkeo yuko hapa?!!!....aliuliza Dom kwa mshangao.

Wakiwa wanashangaa mara ilitolewa amri kutoka kwa suya:

Anzeni kumkata kiungo kimoja kimoja hadi afe kama hataki kusema ukweli..!!...

Dom na Fasha walihisi kuchanganyikiwa..

Bila kuchelewa mpambe mmoja aliushika mkono wa Rania na kuufunga kwenye mti na kuinua upanga unaong'aa kumkata Rania...

Fasha.. Liwalo na liwe mimi naenda kumsaidi Rania... Alisema Dom.

Walitoka wote kwa kasi kubwa kwenda kumsaidia Rania..

Kumbe muda huo wapambe wawili wa ngomeni pale walikua wameshawaona...ile wanaondoka kumsaidia Rania wale wapambe walifyatua mishale yao na......NINI KINAFUATA?..

USIKOSE SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA

TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni