RANIA (29)

Zephiline F Ezekiel
JINA: RANIA
SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA
ILIPOISHIA...
Fasha,Liwalo na liwe mimi naenda kumsaidi Rania... Alisema Dom.

Walitoka wote kwa kasi kubwa kwenda kumsaidia Rania..

Kumbe muda huo wapambe wawili wa ngomeni pale walikua wameshawaona...ile wanaondoka kumsaidia Rania wale wapambe walifyatua mishale yao na......

SASA ENDELEA..
Dom na Fasha wakiwa wanaelekea alipo Rania ili wamsaidie mara Dom alishtuka kuona mshale wa kwanza huo unaelekea kutua kwenye bega lake la kulia...

Bila kuchelewa aliupangua na kumvuta Fasha pembeni ili ule mshale wa pili usimpate...

Alifanikisha kujiokoa na kumwokoa Fasha.

Hatuna muda wa kupoteza..haraka twende....alisema Dom.

Walikimbia na kwenda kujificha sehemu fulani na bila kuchelewa Fasha alifyatua mshale ambao ulienda kutua moja kwa moja kwenye mkono wa yule mtu aliekua anajipanga kumkata Rania mkono.

Suya na watu wote waliokua pale walishtuka sana kuona hivyo..

Wakiwa wanashangaa bado Fasha na Dom walifika pale na kuanza kuwashambulia.

Watumishi wa pale ngomeni nao hawakua wazembe..walipambana nao vilivyo.

Mars alipomwona Fasha pale alitamani kukimbia Fasha asimwone.

Nimeshakuona Mars... Hata usijisumbue kukimbia.. Alisema Fasha.

Mars alihisi kuzimia...duuh..Alikua ameumbuka si kidogo.

Mars,suya na watu wao waliduwaa kidogo.

Dom hakua na muda wa kupoteza.. Alimfungulia Rania haraka huku akiendelea kupambana.

Fasha.. Ondoka na Rania mimi nitapambana nao..alisema Dom.

Hapana nenda nae wewe.. Mimi ni mzoefu wa haya mambo ya vita...hautawaweza hawa Dom..haraka hatuna muda wa kuongea sana....mchukue Rania uondoke nae...alisema Fasha.

Dom hakutaka kubisha..haraka alimchukua Rania na kwenda nae ingawa alikua na wasiwasi mkubwa juu ya litakalomkuta Fasha

Fasha una akili sana...maana kama ungembakiza huyo mwingine wewe ukaenda na Rania basi angekufa hapa... Ila kwakua umebaki wewe hautauawa kwa leo maana hatujawa tayari kupambana na mfalme... Alijisemea suya kimoyomoyo.

Watu wa suya walitaka kumfuata Dom lakini walikutana na kipingamizi kikubwa kutoka kwa fasha.

Mnafanya nini nyinyi?.. Mtu mmoja anathubutu vipi kuwasumbua?...alisema suya kwa ukali.

Baadhi ya wapiganani wa Suya walikua wanaogopa maana Fasha anajulikana kwa kutembeza kichapo cha muno.

Kwa kujikaza walianza kumshambulia Fasha..walipata kipigo wote hadi wakawa hoi...

Hata hivyo hawakukata tamaa..waliamka na kuanza mashambulizi upya... Katika wale wapiganaji alikuemo mmoja ambae nae alikua shujaa kipindi cha vita... Huyu ndo anagalau aliumudu mziki wa Fasha.

Katika kupigana mpiganaji yule alimjeruhi Fasha kwenye bega lake.

Rai alikua nyumbani kwake amelala..ila ghafla hofu ilimpata...wala hakujua nini tatizo..

Wakati Fasha anajeruhiwa mwili ulisisimka sana...

Mwanangu Dom atakua matatizoni...alijisemea Rai

Malikia... Tulete wapiganaji zaidi tumdhibiti huyu fasha... Alisema Mganga..

Hapana...mwache aende kwa leo..alisema suya..

Ni kweli... Hatakiwi kuuawa leo..alisema Mganga.

Fasha alimwangalia Mars jicho bata..Mars aliangalia chini.

Baada ya hapo Fasha aliondoka na kwenda kuwatafuta Dom na Rania.

Alitembea muda mrefu bila kuwaona hatimae akawakuta pale ambapo waliwaacha Farasi wao kipindi wanaenda kumsaidia Rania.

Hali ya Rania ilikua mbaya sana...aliwaangalia kwa mbali sana na baada ya muda akapoteza fahamu.

Twende nyumbani haraka... Mama atamtibu Rania.. Alisema Dom.

Ni tabibu pia?..aliuliza Fasha.

Ndio ni tabibu ...alisema Dom.

Walimpandisha kwenye farasi na kuanza safari ya kuelekea kwao Dom.
*****

Malikia... Nitafanya nini wakati Fasha ameniona?..aliuliza Mars kwa wasiwasi mkubwa.

Cha kufanya ni kimoja... Alisema Mars.

Inabidi usirudi ikulu...alisema suya.

Kwanini malikia?.. Aliuliza Mars.

Haraka kesho unatakiwa unanze safari ya kwenda Lazi....Alisema suya.

Malikia!!.. Nikafanye nini?..aliuliza Mars kwa mshituko.

Unatakiwa ukamsingizie Fasha na ufalme mzima kua wamekufanyia mambo mabaya sana na umeamua kuondoka kwa siri.

Hapo itakua rahisi kwa Mfalme wa Lazi kukubali kutusaidia pale tutakapomshwishi maana atakua anaamini kua binti yake wamemfanyia mabaya.

Mmh...haya...mambo gani hayo nitakayowasingizia?..aliuliza Mars.

Suya alimwambia mambo ya kuwasingizia na Mars akakubali.

Wakati huo Dom na Fasha walikua wakiendelea na safari yao ya kwenda kwao Dom.

Muda huo Rai alikua hana usingizi... Alikua na wasiwasi kwa kitu ambacho hakijui.

Akiwa anawaza mara mlango uligongwa...Rai alishtuka sana maana ilikua usiku sana.

Mama!!....aliita Dom.

Rai alishtuka kusikia sauti ya mwanae Dom.

Mama fungua....alisema Dom.

Rai aliwahi kufungua baada ya kujua hakika huyo ni mwane Dom.

Dom..mnatoka wapi usiku huu?.. Aliuliza Rai.

Mama...Rania yuko vibaya... Alisema Dom.

Rai hakutaka kuuliza sana maana Rania alikua katika hali mbaya sana...haraka alimchukua na kumfanyia huduma ya kwanza.

Baada ya kumaliza kumhudumia alianza kuwauliza Fasha na Dom.

Kabla hajaanza kuwahoji mara aliona damu kwenye bega la Fasha.

Oooh...na wewe una majeraha..hebu njoo hapa..alisema Rai.

Fasha alisogea na kufunua alipojeruhiwa...

Mmmh...kidonda kikubwa sana... Alisema Rai kisha akamfanyia Fasha huduma nzuri kwenye kidonda chake.

Dom huyu ni nani?..aliulza Rai baa ya huduma.

Ni mwanamfalme Fasha....

Haa...mwanamfalme!!!... Ngoja nimwangale vizuri usoni nimkariri...alisema kisha akacheka.

Rai alichukua taa yake na kumsogezea Fasha ili amwone vizuri.

Rai alishtuka baada ya kumwona Fasha.

Mama...kuna nini?..aliuliza Dom baada ya kumwona mama yake ameshituka.

Fasha alifanana sana na baba yake habiri... Yaani walifanana sana.

Mwanamfalme???...... Alijiuliza Rai kwa mshangao.

Mama kwani kuna nini?..aliuliza Fasha.

Rai alikumbuka siku alipoambiwa kua Fasha sio mtoto halali wa Mfalme... Hakika alichanganyikiwa sana

Lakini mwanangu mbona alikufa?..au habiri atakua alizaa na mwanamke mwingine?.. Au ni mtoto wa ndugu yake habiri?.. Alijiuliza Rai bila kupata majibu sahihi..NINI KINAFUATA?..

USIKOSE SEHEMU YA THELATHINI

TAZAMA VIDEO HII KISHA BONYEZA SUBSCRIBE CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni