RANIA (31)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA THELATHINI NA MOJA ILIPOISHIA... Kweli kaka Dom.. Angekufa huyu mapepe...alisema Fasha. Mmmh...kaka Dom?....alisema Rania kiumbea zaidi asijue kinachoendelea... SASA ENDELEA.. Nini kwani..umbea tu...alisema Fasha. Kama wewe... alisema Rania. Dom alicheka tu kusikia hivyo. Walikaa pale kwa muda mrefu. Huku Mfalme alikua ameshapata wasiwasi juu ya Fasha kwakua alikua hajarudu hadi muda huo... Baada ya muda mrefu waliondoka na kwenda ikulu. Mfalme alisubiri sana lakini Fasha hakua akija...ila baada ya kusubiri sana Mara Fasha alikuja. Mfalme akiwa anamawazo mengi mara alikuja Fasha na kubisha hodi. Aah..Fasha.. Umechelewa sana...haya niambie ulichokipata..alisema Mfalme baada ya Fasha kuingia. Fasha alikaa na kusema... Baba ni mengi niliyokutana nayo huko...alisema Fasha. Yapi hayo?...aliuliza Mfalme. Fasha alihofia kumweleza yaliyotokea kipindi Rania anamfuatilia Mars maana Mfalme hakua akijua habari ya Rania na uhusiano wake na ufalme.. Ilibidi tu amweleze up…