RANIA (32)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA THELATHINI NA MBILI ILIPOISHIA... Baba mwanao yamenikuta makubwa...nimenusurika kifo baba..Tharia ni watu wabaya sana..alisema Mars. Wamekutenda nini?..aliuliza Mfalme kwa hamaki.... SASA ENDELEA.. Baba...nchi ya Tharia ina mambo mengi sana ya ajabu...baada ya Mfalme na mwanae Fasha kujua kua mimi nimeyafahamu wakataka kuniua...alisema Mars. Mfalme alishituka sana. Yapi hayo mambo?.. Aliuliza mfalme. Ni mambo tu ya ukatili na mauaji wanayoyafanya kwa watu wasio na hatia.. Wameshawaua wengi hata watoto wa viongozi wa nchi na ndio maana wanahofia yasijulikane usije ukatokea uasi... alisema Mars. Yaani yeyote atakaejua tofauti na mfalme na mwanae basi anauawa..hata malikia suya na Mganga kwa saaa hawapo ikulu walitoroka kwa kuogopa kufa kwakua walikua wameshajua siri...Alisema Mars. Mfalme alishangaa sana kusikia vile na alipatwa na hasira sana.hakuwaza hata kidogo kua mwanae ni mwongo. Baba...mimi siwezi kurudi huko tena...kwanza sasahivi Mfalme anampango…