RANIA (33)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA THELATHINI NA TATU ILIPOISHIA... Mfalme alifungua barua ile ba kuisoma yoote....alionekana kukubaliana na yaliyoandikwa pale ingawa sina hakika sana😊. Wale wapambe walipotoka tu tayari Rania na Namadi walikua wameshafika.... SASA ENDELEA.. Barua ile ilikua imeandikwa na suya kumwomba Mfalme ashirikiane nae kwenye kuupindua ufalme wa Tharia kwa sababu Tharia wana huo mpango wa kuipindua Lazi.. Kwahyo Mfalme anatakiwa awawahi ili wasije wakampindua. Mfalme aliona hilo jambo ni jema kabisa lakini hakutaka kukurupuka kukubali ombi hilo... Alipanga kufanya uchunguzi kama aliyoyasema Mars ni kweli. Namadi na Dom tayari walikua wameshafika Lazi tena maeneo ya karibia ikulu.. Kwakua Namadi alikwenda kusimama pale lango kuu la kasri na kuomba aonane na mlinzi wa Mfalme. Kwakua alikua alishawahi kuja mara ya kwanza pale hakua mgeni sana machoni kwao. Muda mfupi baadae alikuja mlinzi mkuu wa mfalme na kumkuta Namadi pale. Akimchukua na kwenda nae pembeni. Namadi k…