RANIA (34)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA THELATHINI NA NNE ILIPOISHIA... Mfalme aliamua kukaa kimya.. Suya na watu wake walikua wakisubiri majibu mazuri kutoka kwa Mfalme kwa hamu kubwa. Mars aliona baba yake hasemi kitu akaamua kumfuata ili ajue angalau nini anachowaza baba yake. SASA ENDELEA.. Mfalme, Mars anahitaji kuonana na wewe... Alisema mtumishi wa Mfalme. Mwambie aingie.. Alisema Mfalme. Mars aliingia na kukaa karibu na baba yake. Baba..hivi mbona uko kimya?...ukichelewa sana Mfalme wa Tharia atakushambulia wewe kabla ya wewe kumshambulia.. Alisema Mars. Najua hilo mwanangu... Nina mpango wangu mwenyewe.. Alisema Mfalme. Kwanini usishirikiane na malikia suya?..aliuliza Mars. Mfalme aligeuka na kumwangalia Mars kwa muda mrefu hadi Mars akashituka. Sitashirikiana na Suya... Nitajua mimi cha kufanya.. Alisema mfalme. Baba... Kwanini usishirikiane na Suya?.. Aliuliza Mars. Mars binti yangu... Aliita Mfalme. Abeee baba..aliitika Mars. Hebu acha Mara moja hayo mambo unayoyafanya kwa cheo cha bin…