RANIA (39)

Zephiline F Ezekiel
RANIA (39)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA THELATHINI NA TISA ILIPOISHIA... Suya hakuamini macho yake.. Alizani yanamdanganya. Muda huo Rai alikua njiani anakuja kwa kasi licha ya hali mbaya aliyokua nayo. SASA ENDELEA.. Suya..Muda ukifika umefika..huwezi kupeleka mambo yote kama wewe utakavyo kwakua dunia sio yako..alisema Mtu yule. Kumbe uko hai.. Kwahiyo nilidanganywa!...alisema Suya. Hauna muda wa kufikiria hilo..haitabadili kitu.. Alisema mtu yule. Hata kwako haina faida yoyote ya wewe kurudi...alisema Suya. Ipo faida.. Mke wangu na watoto wangu wawili watakua wanahitaji kuonana na mimi bila shaka... Alisema mtu yule. Watoto wawili?... Wawili?... Aliuliza Suya kwa dharau. Hakuna siri zaidi kua Mwanamfalme Fasha sio mtoto wako wa kuzaa...alisema Mtu yule. Funga mdomo wako!!!...alisema suya kwa ukali. Sawa nafunga..ila huo ndio ukweli... Alisema mtu yule. Suya alikasirika sana...alihema kwa hasira. Hata kama huo ndo ukweli.. Mfalme hatakubali kirahisi na wala hajui...alisema Suya. Hadi nakuja hapa…