AISEE KUMBE RAHA (1)
JINA: AISEE KUMBE RAHA Mwandishi: Pablo SEHEMU YA KWANZA Ilikuwa ni mida mida ya jioni kama saa kumi na mbili hivi jua lishazama ilibaki kuwa saa kumi na mbili na nusu saa tu kutokana na giza kuingia nakuashiria ilikuwa tayari usiku. wakati huo nilikuwa chumbani kwangu nikijisomea masomo ya chuo kupitia laptop yangu kutokana na mitihani iliyokuwa ikikaribia kufika. nikiwa naendelea kusoma ghafla mlango wa chumba changu ukagongwa na kunifanya ninyanyuke kwa kujikokota kwa uchovu na kuufungua mlango ambapo nilikutana na sura ya mama yangu mzazi ambaye alionyesha ana kitu cha kuniambia kutokana na kugugumia kuniambia na kubaki akiniangalia kwa muda bila ya kuniambia chochote. "Sasa mwanangu nikuambie kitu" "Nambie mama" "Najua umechoka sana na unajiandaa na mitihani yako sitaki kukusumbua ila nina shida mwanangu nilikuwa naomba nipelekee mzigo wangu kwa shoga yangu Mama Chiku. yeye hayupo utamkuta rafiki yako chiku utampatia halafu utarudi mara moja nashika pesa hizi u…