AISEE KUMBE RAHA (11)
JINA: AISEE KUMBE RAHA Mwandishi: Pablo SEHEMU YA KUMI NA MOJA ILIPOISHIA... Mwanaume baada ya kuona mama chiku tayari kashauliwa na yule mume wake nikajikuta nikihaha zaidi ya pale nilizidisha kuomba ukelele wa kuomba msaada bila ya mafanikio yoyote jasho lilizidi kunidondoka na kujikuta. SASA ENDELEA... "Kidume mbona unakelele sana kabla hata haujapigwa." Yule mume wake mama chiku akaniambia kwa sauti ya ukali iliyosababisha ninyamaze kimya nakumuangalia yeye kwa hofu kubwa sana.ghafla yule mjeshi akatoa ishara baada ya kupiga kofi mara moja nakusababisha wale wenzake wakae sawasawa kisha mume wake mama chiku akaninyooshea mimi kidole na wale wenzake haraka haraka wakanisogelea na waliponifikia wala hawakuniuliza bila ya huruma wakaanza kunishambulia kwa mikanda katika mwili wangu mikanda ambayo haikuwa na idadi.Hakika wale majamaa hawakuwa na huruma kabisa licha ya mimi kupiga makelele ya kuomba msaada na msamaha kwa wale hakuna hata mmoja hakika walinishambulia nakuanza kunito…