AISEE KUMBE RAHA (14)

Zephiline F Ezekiel
AISEE KUMBE RAHA (14)
JINA: AISEE KUMBE RAHA Mwandishi: Pablo SEHEMU YA KUMI NA NNE ILIPOISHIA... "Na....aaa..m" "Ujasikia au unafanya kusudi nakuuliza tena je ni wewe ndiye uliyepost picha za utupu za mwanadada catherini na kuziweka hadharani katika mtandao wa facebook naomba unijibu na ukileta ujinga basi pasi hii nitaichomeka vyema katika mbavu zako hizo.".... SASA ENDELEA... Maneno yale yule jamaa yalizidi kunipagawisha na kunitisha kiasi ambacho nilijikuta nikitokwa na majasho mengi kama nilikuwa nakimbia huku mikono yangu ikiwa inatetemeka kama mgonjwa aliyekuwa akisikia baridi. "Kijana pablo unanikera maana nakuliza swali ujibu nakuuliza mara ya mwisho na usiponijibu basi ujue kuwa hiyo pasi itakufanya useme yote."yule jamaa akaendelea kuniambia huku akainiangalia mimi niliyekuwa namuangalia yeye huku yeye akiwa amenikazia macho ili kuniogopesha kwa sababu mpaka muda huo alishajua kuwa mimi tayari nimeshaanza kuogopa. "Pablo je ni wewe uliyepost picha za utupu za mwanadada …