AISEE KUMBE RAHA (16)

Zephiline F Ezekiel
AISEE KUMBE RAHA (16)
JINA: AISEE KUMBE RAHA Mwandishi: Pablo SEHEMU YA KUMI NA SITA ILIPOISHIA... "Weeee suzaniiiiii.!!!??" ile tunatoka tu nje ya gesti ile nikasikia sauti kali ikimuita suzan na kujikuta wote mimi na suzan tegeuke kwa uoga lakini bila ya kutegemea kabisa macho yangu yakamshuhudia Chiku akiwa Na mama yake akiongoza na Mama catherini na catherini mwenyewe "Tobaaaaa!!!"............. SASA ENDELEA... Maneno ya uoga yakatamka katika kinywa cha suzan ambaye hakuamini kabisa hali ile ambayo ilikuwa imetokea na kujikuta mpaka akijiziba uso wake kwa kutumia mikono yake na kuganda pale na kuanza kutetemeka kwa uoga.Hata mimi hofu kubwa ikatanda na kujikuta nikiungana na suzan pale kuganda na kujikuta nikiinamia chini baada ya kuona Mama chiku na chiku wakiwa wananiangalia kwa hasira sana. "Suzan shoga yangu yani hata wewe.??" Chiku akasema kwa hasira na kumuangalia kwa jicho baya suzan ambaye alikuwa kainamia chini huku kaziba macho yake kwa uoga mkubwa kutokana na hali ile am…