AISEE KUMBE RAHA (17)

Zephiline F Ezekiel
AISEE KUMBE RAHA (17)
JINA: AISEE KUMBE RAHA Mwandishi: Pablo SEHEMU YA KUMI NA SABA ILIPOISHIA... Lakini kabla hata sijafika mbali baada ya kushuka katika daladala na kuelekea nyumbani kizunguzungu cha ghafla kikanikumbaa na kunijikuta nikijishika kichwa baada ya kuanza kuhisi maumivu lakini kabla hata sijaendelea ghafla ukungu mzito ukatanda katika mboni zangu nakujikuta nikishindwa kujizuia na Haikuchukua hata dakika nikadondoka mzima mzima mpaka chini na kuzimia Hapohapo............... SASA ENDELEA... Nikuja kushtuka na kukuta watu wengi wakiniangalia nikiwa chini ya Ardhi nimelala ambapo baada ya kuangaza angaza Macho nilikuja kugundua kuwa yalikuwa ni maeneo yale yale nilipodondoka baada ya kukumbuka mapema nini kilichonitokea kwa sababu mara ya mwisho nilikuwa nijisikia maumivu ya kichwa.Watu wengi waliokuwa wakiniangalia wengi wao nilikuwa nawajua kwa sababu ilikuwa ni mtaani kwetu ambapo watu wengi walikuwa wananifahamu kwa sababu mtaani pia nilikuwa najichanganyaga na vijana wenzangu ambao wote tulikuw…