AISEE KUMBE RAHA (18)
JINA: AISEE KUMBE RAHA Mwandishi: Pablo SEHEMU YA KUMI NA NANE ILIPOISHIA... "Haina haja hata ya kuwakaribisha licha ya kuwa nimewaita sasa basi twende moja kwa moja katika lengo la kukuita kuwa kwanza mwanao tumeshamfuta hapa chuoni." "Whaaaaaaaaaaaat.!!!! SASA ENDELEA... Baba akajikuta akipandwa na hasira za ghafla na kupiga ngumi ile meza iliyokuwepo pale ambapo nyuma yake alikuwepo mkuu wa chuo na Mbele yake tulikuwepo sisi.Kupiga meza ile kwa hasira ilikuwa ikiashiri kutoamini kile ambacho mkuu wa chuo alipomwambia kuwa nimefutwa jina chuoni ikiashiria kwamba nilikuwa nimefukuzwa. "Unasemaje mkuu wa chuo Mwanangu nini."Baba akaongezea huku akimuangalia yule mkuu ambaye kidogo alianza kuonyesha hali ya uoga fulani baada ya baba kupigwa ile meza kwa hasira.Wakati huo mimi nilikuwa kimya kijasho chembamba kikianza kunitoka kwa sababu nilishaanza kuhisi kuwa kosa la kufukuzwa chuo lilikuwa ni zile picha ambazo nilizopigwa nikiwa mtupu na kutangazwa katika mitandao ya…