AISEE KUMBE RAHA (5)

Zephiline F Ezekiel
AISEE KUMBE RAHA (5)
JINA: AISEE KUMBE RAHA Mwandishi: Pablo SEHEMU YA TANO ILIPOISHIA... "Jamani shosti wangu catherini vipi??"suzan akajitutumua kumsalimia catherini ambaye hakuitikia ila taratibu akaanza kutosegelea kwa shauku kubwa ya kutaka kujua kilichomnyoa kanga manyoya.............. SASA ENDELEA... ‘’Enhe shosti vipi jamani mbona uongei mbona kimya??’’ suzan akamuuliza swali lingine catherin swali ambayo lilimfanya atoe tabasamu pana lilizidi kunichanganya mimi ambaye sikuwa na la zaidi la kuongezea wala kuongea kutokana na kuanza kuona msalaa mwingine unaanza kutokea bila ya kutegemea ‘’sio siongeii na shangaa kwanza mlivyokuwa mnashikana viuno tena etiiiiiii ndio mtu na shemeji yake’’catherin akajibu swali lilinifanya sasa nianze kutetemeka kwa mbali.nilianza kujilaumu sasa kufanya vile mimi na suzan ambaye baada ya Catherine kujibu swali lile naye akaatulia kimya nakuinamisha kichwa chini na kutokuwa na lakujitetea. ‘’Yaani wee Pablo na wewe una hata haya mwanaume mzima ovyooo kazi kufanya…