AISEE KUMBE RAHA (8)

Zephiline F Ezekiel
AISEE KUMBE RAHA (8)
JINA: AISEE KUMBE RAHA Mwandishi: Pablo SEHEMU YA NANE ILIPOISHIA... Baada ya catherini kusema vile mmoja kati ya wale majamaa akanisogelea karibu na kuzamaa mfukoni nakutaka kuchukua simu nilipojaribu kuzuia wasiitoe simu yangu teke lingine likatua usoni na kusababisha ukungu mzito utande katika macho yangu……………… SASA ENDELEA... Hakika teke lile likanizimisha kabisa nakuzimia papo hapo.nilikuja kushtuka nikiwa naburuzwa na wale majamaa ambao waligawana kuna wengine walikuwa wamenishika mguu wengine mikono na nilijaribu kuangalia nyuma macho yangu yakamuona catherini ambaye alikuwa naye nyuma akiwa ameshika simu yangu ya samsung galaxy akiwa anaibonyeza bonyeza jambo ambalo liliniuma sana. "Jamaani nani huyo mbona mnamburuza hivyo??" Yalisikika maneno kutoka upande ambao nilipojaribu kuangalia nikawaona akina mama ambao walikuwa wanashauku kubwa ya kutaka kujua kwanini walikuwa wananiburuza vile. "Huyu ni mwizi tumemkamata alikuwa ameiba simu yangu" katika hali nisiyoitege…