LISEME JINA LANGU (1)

Zephiline F Ezekiel
LISEME JINA LANGU (1)
JINA: LISEME JINA LANGU Mwandishi: Pablo SEHEMU YA KWANZA "Priiiiiiiiii!!!"ilikuwa ni sauti ya filimbi iliyotoka mdomoni mwa refarii na kuruhusu mtanange wa kukata na shoka wa mpira wa miguu ambao uliovuta hisia za watu katika Uwanja huo.licha ya kuwa ilikuwa mechi ya kirafiki katika uwanja huo ulizozikutanisha timu ya mtaani kweti The orland na timu kutoka Mtaa wa jirani iliyoitwa Black Mambaz lakini ulihudhuriwa na watu wengi ambao pia hawakusita kushangilia huku wakiwa na hamu kubwa ya kuuangalia mechi hiyo.jina langu lilikuwa likitajwa tajwa na Mademu wa timu ya mtaani kwetu huku baadhi yao wakiniita na kunitungia majina yaliozidi kunipa kichwa "haloow msiniumizie Pablo wangu!!!"ni maneno ambayo yalizidi kunipa morari mara nyingi macho yangu yalituwa katika demu wangu Jackline Ambaye wakati huo alikuwa Yupo hoi kwa kunishangilia.Mpira ulianza huku timu pinzani ikifanya mashambulizo ya hapa na pale yaliosababisha madhara kidogo kama kona Zilizowafanya mashabiki wetu…