LISEME JINA LANGU (14)

Zephiline F Ezekiel
LISEME JINA LANGU (14)
JINA: LISEME JINA LANGU Mwandishi: Pablo SEHEMU YA KUMI NA NNE ILIPOISHIA... Akiwa anachechemea mguu mmoja huku majasho mengi yaliokuwa yanamtiririka kwa kasi na kuzidi kulowesha shati akajikokota na kuchukua lile dude la shisha na kulinyanyua na kunielekezea mimi kwa lengo la kunitwanga nalo na kunifanya nibaki nimemtumbila macho huku Nikiwa najaribu kuinuka lakini maumivu ya mshale wa bega ulitosha kabisa kuniua nguvu na kubaki nikimuangalia tu Robertson aliyekuwa yupo tayari kabisa kunirushia dude lile............................. SASA ENDELEA... Bila hata ya huruma robertson akanirushia lile dude la kuvutia shisa ambalo lilikuwa lina moto wa kutosha ambalo baada ya kunifikia nikalivuia kwa mkono lakini mikaa mikaa ya lile dude lilitosha kabisa kuniunguza na kujikuta nikipiga kelele kutokana na maumivu makali niliyoyapata kutokana na moto ule.Mikono yangu ndio ulikuwa imebabuka kwa moto ule ambapo baada ya robertson kunirushia akaanza kucheka kwa nguvu na kuanza kunitukana wakati huo mim…