MAMA MWENYE NYUMBA (49)
JINA: MAMA MWENYE NYUMBA Mwandishi: Mbogo Edgar SEHEMU YA AROBAINI NA NNE ILIPOISHIA... Alitembea mpaka, kwenye kiuo cha daladala za kwenda kibaha, yani upande wa morogoro, akaingia kwenye gari (coster) la kwenda msata, akakaa kwenye siti yap eke yake, na kuliweka lile begi la mzee Mashaka chini ya siti SASA ENDELEA... Dakika kumi natano mbele alikuwa amesha fika mzani wa zamani, wa kibaha maili moja, akashuka baada ya kulipa nauli kwa kondakta, nakulitelekeza lile begi la mzee Mashaka, ilisha timia saa saba kamili za mchana, hapo Edgar akasogea pembeni kabisa ya barabara pana ya eneo lile, na kutulia macho akiwatazama polisi ambao walikuwa wame tanda pale wakikagua magari yenye makosa, Edgar aliwatazama wale polisi akijaribu kumchagua ambae angeweza kumsaidia kumtafutia usafiri wakumfikisha Songea, akiamini anaweza kupata atakama ni gari kubwa la mizigo, maana kwa bus mida hii ata kwabahati mbaya usingeweza kulipata, mabus ya Songea uwa yanapita kuanzia saa kumi nambili na nusu adi saa moj…