MAMA MWENYE NYUMBA (50)
JINA: MAMA MWENYE NYUMBA Mwandishi: Mbogo Edgar SEHEMU YA HAMSINI ILIPOISHIA... Kama ilivyokuwa kwa mzee Mashaka , nao wakalazwa kwenye chumba chao wawili, nayule mwingine nae akiwa amelejewa na fahamu lakini bado hajitambui SASA ENDELEA... Mzee Mashaka ile kutambua tu uwepo wa mke wake pale, akiwa ame kaa karibu yake kabisa kwenye kitanda, akamwonyesha ishala ya kumwita kwa mkono, maana hasinge weza kuongea kutoka na ganzi ya kushona shavu lake, ambalo lilikuwa na zinga la kidonda, mke wake akamsogelea zaidi, lakini mzee mashaka akashindwa kusema chochote, “ngoja nikachukuwe peni na kalatasi” alisema mama Sophi akiinuka na kutoka nje, ya kile chumba alicho lazwa mume wake, ikapita dakika kadhaa akarudi akiwa na peni na karatai mkononi mwake, akampatia mume wake, mzee Mashaka ambae licha ya mwili mzima kuuma, kunakitu alitaka kumwambia jambo mke wake, mzee Mashaka kwa shida sana akaandika maneno flani kwenye lile karatasi kisha akampatia mke wake, ile kuangalia tu mama Sophi aka tumbua macho…