MAMA MWENYE NYUMBA (62)
JINA: MAMA MWENYE NYUMBA Mwandishi: Mbogo Edgar SEHEMU YA SITINI NA MBILI ILIPOISHIA... Aliongea Rose akisimamisha gari nje ya jingo la benk ya wananchi na kushuka akiwa na note book yake ile aliyo kuwa nayo safarini, pamoja na karamu akawafwata polisi walio kuwa wanalinda benk hile SASA ENDELEA... Edgar akawaona wale polisi wakimpigia salute Rose, naye akaitikia kwa kupiga salute, kisha akaona wanaongea maneno flani flani huku Rose akiyaandika kwenye ile note book yake, baada ya hapo akamwona askari mmoja akiiga salute na Rose akaitikia kisha Rose akarudi kwenye gari, “hongera sana yani unaonekana mdogo, alafu unacheo kikubwa sana” alosema Edgar akijaribu kuzigusa nyota za Rose kwenye mabega yake, huku gari likiondoka na kuendelea na safari zao “ongera wewe kwa kumpagawisha afisa wa polisi” aliongea Rose wote wakacheka Sophia akiwa njiani akitokea Tumbi hospital akielekea nyumbani kwake mbezi kwa msuguri, na sasa alikuwa mitaa ya Kiluvya gogoni wengi wanapenda kupaita njia panada ya kawawa,…