
SEHEMU KWANZA
Ndani ya nyumba moja hivi, kuna kelele ziliweza kusikika.
kelele ambazo bila shaka mpigaji atakuwa kapandisha mashetani.
“niachee"......uuwiiiiiiii huyu mchawi
Nimesema tokaa!!!...
ndani ya nyumba hiyo milango yote ilifungwa si uwani wala barazani,
Wakati nyumba hii kelele za Binti aliyepandisha mashetani zikisikika,
Nyumba nyingine kulikuwa na sauti ya vicheko,
sijui wanacheka nini,
nyumba nyingine kulikuwa na sauti ya vilio sijui wanalia nini.
Nyumba nyingine kulikuwa na ugomvi baina ya vijana wawili kila mmoja akisema
“Matrida ni wangu mimi"
Katika purukushani kukuru kakala
baina ya vijana wale mmoja kati yao akadondoka chini huku akipaza sauti jamani...."
Nakufaa".....kumbe mwenzake alitoa kisu na kuanza kumchanachana.
Yote yanatokea ndani ya kitongoji kimoja,
kitongoji ambacho kipo nchini Tanzania jijini
Dar es salaam, kinaitwa Mtaa wa tatu
Mtaa ambao
Ni zaidi ya sodoma na gomora watu wanaishi kama wanyama,
Wengi wa vijana wanaoishi pande hizo wamepinda sijui kunyongorota,
Katika mitaa yote hiyo
kuna mtaa wa kwanza kisha mtaa wa pili na huo mtaa wa tatu hakika usiiguse kabisa moto wa mitaa hiyo ni hatari tupu.
Mwizi akikamatwa atajuta kuzaliwa
“Hivi mume wangu unataka
Hafidhi aje kuishi hapa nyumbani hivi uoni kama utamsababishia matatizo, bure"
“kuhusu hilo wala usitie shaka mke wangu, kumbuka
Hafidhi namfahamu vizuri sana, ndio kiboko ya wajinga wote na nimemwita makusudi
Aje kuishi nasi
yani kama moto ule auzimiki hata kwa faya"......
“mmh wee msifie tu sio akija hapa
mtoto wawatu ageuzwe shoga
au akatwe ile naniliu yake"
“Ahaa sasa hizo dharau Ankor wangu Mimi hawezi kugeuzwa shoga kwanza nitake radhi kwa niaba yake"
“haya nisamehe mume wangu".....
Yalikuwa mazungumzo baina ya wanandoa wawili kuhusu swala la kijana anaesemekana anakuja kuishi hapo,
Tukija ndani ya
Mkowa wa Iringa tunamuona kijana mmoja akiwa kifua wazi akifanya mazoezi ya Wushu akipiga zile style za
hayati
hakika alikuwa yuko faster mwepesi mno yani alidank huku na kule kijasho kilimvuja,
siku zote mazoezi ndio muhimili wa hafya ya binaadamu,
“ongera sana mwanangu binafsi inaonyesha ni jinsi gani Mwalimu wako amekufunza vyema"....
Ilikuwa kauli ya pongezi kutoka kwa
Baba mmoja hivi yani mtu mzima kiasi,
Kijana yule
akatabasamu na kusema,
“ndio Baba yangu Master Santos kanifunza vyema hakika najihisi niko
na niko tayali kwenda jijini Dar es salaam nikafanye kazi aliyoniitia
Ankor"......
“Hafidhi mwanangu kuna mengi naitaji kuongea nawe kabla hujaondoka nikiwa kama mzazi.
Kwanza kabisa ukifika huko usipende kujionesha wewe ni nani
usimpige au kupigana na mtu yeyote yule pasipo
Chanzo chochote jalibu kutatua matatizo yako au ya wengine kwa maneno ya busara"
kingine kaa mbali na Wanawake kumbuka wewe ni kijana mdogo sana
nafahamu fika kuna vishawishi vingi sana utakutana navyo
huko uendako"....
Wakati wakiwa wanaongea
Sauti ikasikika ikiita
“Hafidhi j Ikram"..
nae akaitikia
“naam Mama"
“embu njoo kila kitu tayali huku,
Bila kupoteza muda akaingia ndani yeye na
Baba yake kumbe
Mama yake kamuandalia kila kitu kwa ajili ya safari
na siku hiyo ndio alikuwa anasafiri.
basi akajiandaa kwa ajili ya safari
yapata saa tatu
Asubuhi ndani ya Bus
Hafidhi j ikram alikuwa ndani yake na kuwapungia mkono wa kwaheli wazazi wake,
Anaiyacha Iringa, na kwenda jijini
Dar es salaam
hakika safari ilikuwa ndefu kidogo
“wee konda mwambie dereva wako apunguze mwendo kasi
Maana hakubeba magunia humu ohoo"....
“mwambie mwenyewe kwani hauna mdomo au?"
“mimi nishamwambia zaidi ya mara tatu hasikii tu,
Tena anaongea na simu huku akiendeesha kwa mkono mmoja si dharau hizi"
Wakati abilia wote wapo kimya
ni mtu mmoja tu tena mwanamama ndio aliyekuwa akikemea kitendo
cha dereva kuendeesha gari kwa speed.
Kibaya zaidi anaongea na simu,
Japokuwa mama yule aliongea hivyo.
Ikawa kama vile kamwambia ongeza mwendo Baba
dereva hakujali mashimo wala matuta
Alikanyaga tu
wenye roho nyepesi wakapiga kelele za tunakufaa!!!
Hafidhi j Ikram akiwa amekaa kwenye siti ya katikati nae alishtuka kutoka
usingizini kumbe alikuwa kalala.
Akacheki mbele
na kutamka neno moja tu
“Mungu wangu".....
Bus ilikuwa uso kwa uso na scania kama hakika
Mungu akawapigania kwani dereva alikunja kushoto na kuweza kupishana na ile Scani ikiwa nyuma imebeba makontena.
Kila mmoja kiroho kilimdunda.
Mpaka gari inafika pande za Ubungo
yule mama akatapika kabisa
“wee mama embu njoo uzoe matapishi yako"
“wee mshenzi nini nani azoe utazoa mwenyewe aliyekwambia utuweke roho juu nani?
Dereva baada kuona
kajibiwa vile kwa hasira akamfata yule mama na kutaka kumpiga kibao
Ghafla mkono ukadakwa na
Hafidhi kwa sauti ya upole akasema,
“tafadhali kaka yangu hutakiwi kufanya hivyo, tambua kitu kimoja
huyu ni kama mama yako tu"....
Dereva akautoa mkono wake na kumkunja
Hafidhi huku akiwa kamkazia sura
“wee dogo unajifanya unajuwa sio.
Kwanza nani amekuruhusu unidake
mkono?"
kabla
Hafidhi ajataka kuongea chochote yule mama akatoa kitamburisho chake,
Huku akisema
“sikia wewe nyau mimi ni afisa wa jeshi la polisi kuanzia
Sasa upo chini ya ulinzi
Ghafla dereva akawa mdogo kama vile kidonge cha pilitoni
Kitendo bila kuchelewa akafungwa pingu na makofi juu
“haya ongoza njia twende kituoni
Nyie ndio madereva ambao mnasababisha ajali kila kukicha
kitu kingine nimegundua kumbe
Abilia nao wazembe baada ya kukemea wapo kimya tu wacha wafe pumbavu zao embu twende,,,,,,"
“samahani afande, sirudii tena"
Hafidhi j Ikram akabaki kutabasamu tu maana dahaa,
hakika mwanamama yule kacheza kama Pele
ina maana alitapika makusudi akifahamu fika kama si konda
basi dereva atamfata tu.
Kudadeki zake anabahati alivyonikunja nilishaandaa kumpa zinga la
kombora"......
wakati anajisemea hivyo akasikia
anaitwa
“ahaaa Ankor Hafidhi huyoo"
kuangalia ni mjombaake
nae akaenda mbio kumkumbatia kisha wakaingia ndani ya gari safari ya kwenda Mtaa wa tatu ikaanza
“yani siamini kabisa kama mtoto wa Dada yangu mpendwa umekuja"
“kwanini usiamini Ankor ndio nimefika hivi yani hapa kazi tu"...
“ha!ha!ha! kumbe msemo wa muheshimiwa Raisi mpaka Iringa umefika duhuu"...
“Ankor bwana kwanini usifike umefika tena hilo neno wakwanza kulisikia ni sisi hapa kazi tu,
Wacha sukari ipande bei hapa kazi tu kama hamtaki kunyweni uji"
Ndani ya Tax ilikuwa full vicheko mpaka dereva tax
nae akacheka na kuuliza
“hivi mzee huyu kijana wako katokea njombe nini"
Hafidhi akadakia kujibu
“hapana sitokei njombe mimi ni Muhehe original kabisa natokea Iringa yenyewe"
“kwani njombe si ipo ndani ya mkoa wa Iringa au"
“ndio ilikuwepo kipindi hiko sema baada kutanuka sana sasa hivi njombe ipo mkowa wa Makete
kumbuka zote zilikuwa ndani ya Iringa"
“ok! Nimekupata kaka yani inamaana hata hii wilaya ya kinondoni ikitokea siku ikazidi kutanuka itakuwa sio wilaya tena utaitwa mkoa
Au sio?"
“ndio maana yake"
Mpaka wanafika kwenye mtaa mmoja hivi tax ikasimama
kama ujuavyo uswazi watu wambea wakabaki kukodoa
Macho kuangalia nani kina nani wanashuka,
“hii jamani muoneni yule kaka ni handsome balaa"
“wee tulia na nyege zako kila mtu kwako handsome muone kwanza miziwa imekushuka kama vile
Kandambili"...
“toka zako ndio maana unanuka kikwapa",,,,
Yalikuwa mazungumzo baina ya wamama wa kikubwa wakiwa wamekaa kwenye kibaraza cha nyumba moja
hivi.
Inayotizamana na nyumba ambayo
Hafidhi j Ikram ndio kafikia
“karibu sana Mjomba jisikie upo nyumbani hiki ndicho kitakuwa chumba chako"...
Wakati Mjomba yake anamwambia hivyo, yeye ndio
Kwaanza anashanga shangaa jinsi
alivyo waona mabinti kuanzia ukumbini
kuna wasichana wawili mmoja anakuna nazi
Mwingine anasonga ugali.
Kule uwani ndio usiseme
kuna anaefua anaemsuka mwenzake
sijui anafuma kitambaa kila mmoja
yuko busy
“mmh! Shost umekiona chombo hiko?"
“nimekiona sijui katoka America au South maana mwanaume anang'aa
si mchezo"....
“sasa sikia nikwambie kitu Zulfa huyu kijana lazima awe wetu sote yani tumuwai kabla kina
Zainabu hawaja mchukuwa, au unasemaje"......
“ndio penyewe hapo kwa ushenzi nitaanza kumtega leo hii hii
tusije kusubilia embe iive wakati wenzetu wamle kwa chumvi"....
Vicheko vya kimbea vikaweza kusikika kutoka kwa mabinti wale
“ha!ha!ha!
Hallo,,,,hallo,,,utanifunuaa,,,manuu".....
ukishindwa funika,,,,
Hafidhi mwili ukamsisimka kwa yale maneno.
Baada kuelekezwa kila kitu
Mjomba yake akatoka kuelekea kazini maana aliomba ruhusa mara moja tu.
Akatoka mpaka ukumbini na kuongea na mmoja kati ya mabinti wale wawili
“Joyce"...
“abee baba"
“embu shika hii pesa kwanza samahani sana kwa usumbufu kama umeniona nimekuja na mgeni.
Ni kijana wangu naomba umuandalie chakula",,,,,,
“hapana Baba wala haina haja ya kuniomba samahani wala kunipa hii pesa nitamuandalia kila kitu
Atakacho hitaji wala usijali"
Baada Joyce kusema vile Mjomba mtu akatoka
Joyce akamgeukia Zulfa na kugongeana mikono
“wewee dili limetiki
Mulemule"......
“Sasa Joyce tumuandalie chakula gani mgeni wetu, tusije kubugi hapa tukaandaa mataputapu tukaonekana washamba"
“mimi naona tumpikie ubwabwa na nyama ya kuku au unaonaje hapo,
Hakika mabinti hao walikuwa wakijiuliza
chakula gani atakacho kipenda Hafidhi j Ikram
basi wakaanza kukarangiza,
yapata saa kumi alasir
Hafidhi akiwa bado kajifungia chumbani kwa wakati huo alikuwa yuko busy na
Laptop yake kama ujuavyo yeye ni mtunzi wa story,
na story aliyokuwa akiiyandika ni Chanduka
wakati akiwa busy kuumiza kichwa,
Akashtuliwa na sauti ya mlango kupishwa hodi.
Akaiweka laptop yake pembeni na kwenda kufungua
Mlango
akashangaa baada macho yake
kugongana na sura ya binti mrembo mwenye kila sifa ya kuitwa hivyo.
Akapagawa zaidi
baada sauti
tamu kupenya kwenye ngome ya masikio
yake,
“mambo vipi kaka yangu?"
ilikuwa salamu kutoka kwa binti yule si mwingine ni
Zulfa mtoto kajikwatua mpaka kwenye unyayo,
kwa sauti
ya kubabaika
Mwanaume akaitikia
“ahaa po...aa"
Zulfa alianza kucheka na kusema
“ha!ha!ha!
Kumbe una kigugumizi kaka yangu pole sana"....
“hapana sina kigugumizi mbona naongea vizuri tu"
Hafidhi akakaza face na kuongea hivyo,
“ok! Sasa baba kabla hajatoka kaniachia maagizo nikuandalie chakula
sijui unapendelea chakula gani?"
“niandalie chochote kinacholiwa"
“hata kama ugali wa muhogo?"
Zulfa akauliza hivyo
Mpaka Hafidhi akaguna
“mmh ugali wa muhogo tena
Zulfa akaondoka kumbe msosi ulikuwa tayali kila kitu chakula kikabebwa
mtoto wakike
Kabla ya kukipeleka akajiangalia mara mbilimbili kwenye kioo
kikubwa kilichopo kwenye
Kabati la nguo.
NAOMBA SAPOTI, KUNA MATANGAZO(ADS) YANAJITOKEZA KWENYE APP YETU, LIMOJA LINAJAA KWENYE KIOO CHAKO JINGINE LINANG'ANG'ANIA HAPO CHINI KABISA, BONYEZA JAPO MARA 2 AU 3 KILA UKIFUNGUA SIMULIZI HIYO ITANIPA NGUVU YA KUENDELEA ZAIDI NA SIMULIZI ZETU🙏🙏
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

USIKOSE SEHEMU YA PILI
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Maoni, Ushauri na Chochote Share Namimi Katika Mawasiliano Haya:
+255 718 274 413 Ipo WhatsApp
+255 764 339 438
ZephilineEzekiel@Gmail.Com