MTAA WA TATU (3)
JINA: MTAA WA TATU Mwandishi: Hafidhi J Ikram SEHEMU YA TATU ILIPOISHIA... “Hivi wewe hujui kama huyu ndio Baba mwenye nyumba, kwanza tokea lini mtoto wa kiume akapiga deki. Wakati basha wako hata kulenga shimo la choo hawezi mikimba inaenda pembeni. muone kwanza pua imemkauka kama kikwapa cha mbuzi" SASA ENDELEA... Ndani ya nyumba hiyo kuna mabinti wanaongea hatari tupu mmoja wapo ni Joyce kisha kuna Beatrice . tisa kumi kuna Zainabu hakika huyo ni kiboko ana mdogo wake anaitwa Amina kama bange basi wanavuta zile mbichi moshi wanatolea makalioni. Watoto wamedata vibaya mno yani wakasahau kama kuna kufa, baada Joyce kumchamba yule binti akamgeukia Hafidhi na kumwambia “hata usijali kaka yangu wee nenda kaendelee na mambo yako. Kama kudeki atadeki yeye kishankupe " Hafidhi akatabasamu tu na kuingia ndani Akiwa anakatiza ukumbini kuna binti akapigana nae kikumbo bila shaka mmoja kati yao kafanya makusudi Hafidhi akamtizama yule binti hakika mtoto maishaallah binti kaumbika si mchezo. “Mijitu mingine bwana si…