MUUZA UBUYU (8)

Zephiline F Ezekiel
Mwandishi: Micky Mejah

SEHEMU YA NANE
ILIPOISHIA...
"...niliamua kuandika barua nikamkumbushia ile ahadi ndo unaona hawa wakina sam leo maana nilimpenda monica na sikutaka kumpoteza japo sikuwa na pesa kama yule jamaa ila nilikuwa na msimamo na nilijua kusimamia ahadi zangu wewe jiukize kenya airway kuna warembo wangapu niwaache nimfatilie binti wa kijijijni?"

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
Wote tulicheka ila ule ujumbe kwetu ulihusika mno nilimkanyaga sam akaniangalia na kunikonyeza, tuliongea mengi mpka muda wa kulala ulipofika tukaenda kulala.
********"""""""""""""""**********

Siku zilikatika elly akarudi tukawa bega kwa bega akitoka hapa nipo nikitoka hapa nipo ila kuna kipnd nilikuwa naangalia nikipata nafasi nachomoka namtafuta sam tunaenjoy kisha ratiba nyingine zinafata.

Nakumbuka siku hiyo nilimpigia salma simu na kumueleza ratiba zangu "shoga fanya fatilia madeni na kama watahitaji mzigo utanijulisha mimi nipo na sam tunaelekea royal hotel kuna mambo ya kibiashara pale".
*****************

" sam nitalipia hapa kwa siku mbili utakuwa hapa siku ya tatu ndo utaondoka sawa baba

"Poa haina noma"

"Baby relax nataka tuenjoy mapenzi sawa?

" aisee hii hotel kweli five stars yani km nipo ulaya"

"Haaaaaaaa its normal ni sehemu ya hadhi yko baby"
*********************

Sijui ni nini kilitokea usiku ila nilijikuta nipo chooni nikiwa uchi nimefunikwa shuka tu nililia mno baada ya kuona michirizi ya damu kweny sakafu na sam sikumuona.

Nilijivuta kutoka kwenye choo na niligundua kuwa mwili haukuwa na nguvu japo sikuwa nasikia maumivu yeyote mwilini mwangu zaidi ya mwili kutokuwa na nguvu tu.

Nilifanikiwa kufikia simu nikapiga costumer care angalau nipate msahada wa kufahamu tukio lile limetokeaje tokeaje na tulikuwa wawili mwenzangu yupo wapi.

"Yes ndugu mteja tukusaidie nini?
Ilisikika sauti ya kike.

" naitwa emmy mejah nipo chumba no:104 nimepata tatizo la kuvamiwa na nilikuwa na mpenzi wangu simuoni na chini kuna michirizi ya damu halii hii inaniogopesha dada yangu naomba msahada"

"Sawa dada tutatuma watu muda si mrefu kwa ajiri ya uangalizi, je kuna uharibifu mwingne umetokea?

Alivyoongea hivyo akanikumbusha niangalie pochi yangu na niligundua kiasi cha pesa nilichokuwa nacho kilikuwepo nikatafuta nguo alizovaa sam sikuziona kikubwa niliona kitambulisho chake cha chuo inaonekana kilikuwa njee na nguo zake ambapo pembeni pia kilikuwa na driving licence " no dada mimi nina kila kitu tatizo ni huyo mpenzi wangu sijui nini kimemkuta aah dadaaaaa" nilianguka na kupoteza fahamu.
**************

TURUDI KWA EMMY NA CINDY.

"Daaa jamani emmy pole sana baby wangu"

"Ndo hivyo ila bado sikata tamaa namtafuta bado sam wangu alikuwa ni mtu muhimu sana kwangu"

"Mmh nimesahau sasa baada ya kuanguka kule hotelini ilikuwaje??

TUENDELEE NA EMMY FEED BACK.
Nilijikuta nipo hospital nikiwa nimetundikiwa dripu huku pembeni walikuwa maofisa wa ile hotelin nahisi wao ndiowalinileta pale. Baada ya dokta kuja aliwapa maelezo machache juu ya hali yangu nami wasaha huo ndio nilipata kujua ni nini kilinikuta (wale maofisa waliact kama ni ndugu zangu).

"Mgonjwa wetu anaendelea vizuri nafikiri leo mchana mnaweza kuondoka nae, ila kilichokuwa kinamsumbua inaonekana alivuta hewa mbaya mfano wa madawa ya kumaliza ya kupoteza fahamu sasa madhara ya dawa hizo kwanza uathiri mfumo mzima wa upumuaji na pia umfanya mtu huyu kuwa unconsious(asijitambue), kupoteza nguvu za mwili na madawa haya ukaa ufanya kaxi takribani dakika 10-15 au zaidi"

"Sasa kwa hali ya mgonjwa wetu alikuwa affected kwa kiasi gani?

" aaah mgonjwa wetu huyu yeye pamoja na ili alikuwa na upungufu wa maji na inaonekana anapata muda mdogo wa kupumzika kwahiyo ningependa kuwashauri mxingatie sana haya ninayowaambia inabidi apate muda wa kutosha wa kupumzika na anywe maji mengi na si lazima yawe maji tu mnaweza kumpa juice na matunda kwa wingi".

Nilitafakari sana yale aliyokuwa anazungumza dokta na kweli nilikuwa sina mudawa kupumzika yani kwa masaa 24 ni masaa 4 ndio napumzika 20 yote kichwa kipo busy na shule, biashara, mapenzi na familia.

Tulifanikiwa kutoka hospitali saa tisa alasiri wale watu walijitambulisha kwangu kama Jimmy John meneja msaidizi wa mambo ya masoko na William Charles yeye alikuwa ni mkuu wa usalama pale hotelini.

"Sasa dada emmy tunahitaji kufanya mazungumzo nawe sijui ungependelea sehemu gani ya kufanya mazungumzo nawe?

" mmh kwakweli kwa leo sipo sawa naomba niwatafute baada ya siku ya leo"

Tulifanya makubaliano na kisha kuchange contact na walinisihi lile jambo nisiliriripoti police hadi hapo nitakapo kaa nao ila kwa ninavyojua mimi kuwa likitokea suala kama lile la utekwaji nyara, mauaji au ugomvi inapaswa jambo hilo litolewe taarifa ndani ya saa 48 hivyo sikuwa na wasiwasi sana kwani mpk kesho ndio masaa hayo 48yatakuwa yametimia. Walinipeleka mpka nyumbani kijichi ila sikuwa na amani maana nilipofungua tu geti nilihisi uoga wa hali ya juu.

"Mmh au niende temeke? Lakini mara ya mwisho niliondoka na sam nikiulizwa sam yupo wapi nitajibu nini? Aah nitakaa hukuhuku ila nitalalaje peke yangu? Nilijiuliza na kujijibu mwenyewe na muda nao ulizidi kwenda.. Kichwani likaja jina la salma ila nilipolikumbuka nilikosa amani ghafla.
**************

Nilishtuka baada ya kijua kikali kuniunguza miguuni mwangu ambacho kilipitia dirishani nakumbuka hiyo jana usiku nilisinzia palepale sebureni, kitu cha kwanza nilikumbuka simu yangu ambayo niliizima toka nikiwa hospitali sikutaka elly anitafute maana sikutaka ajue nimi imetokea japo nilikuwa na maswali mengi juu ya uhusika wake ktk hili swala la sam. " sijui niwashe simu? Hapana elly atanipigia siwezi kuwasha simu jambo mambo yangu yatakwama kule salma biashara na wale watu wa hotelini niliopanga kuonana nao leo"
Nilijiandaa nikaoga nikawa nafikiria niondoke na gari yangu au nifanyaje?
*********

Nilifika pale hotelini kwakuwa sikuwa na simu ilibidi niulizie kati ya yale majina ya jana pale reception. Nilielezwa ofisi ya jimmy james baada ya yeye kupigiwa simu na kuconfirm niende nikaonane nae.

"Eeh dada emmy karibu sana"
Niliingia ofisini kwake kulikuwa amazing sana computers za hatari malumalu nzuri na air condition safi juu picha ya mkuu wa hiyp hotel na picha ya rais wa tanzania mheshimiwa jakaya kikwete ilikuwa imepamba ofisi nzuri ya jimmy james ambaye inaonekana anakaimu kiti katk ile ofisi.

"Nashukuru kaka, vipi yule kaka mwingine" nilimkumbushia juu ya william ambaye pia tulikuwa wote hospitali jana, alinyanyua simu na kumpigia mimi muda huo nilikuwa naangalia wingi wa vile computer mule ndani.

Muda punde william nae aliingia
"Eeh dada emmy karibu sana, sasa inabidi mheshimiwa ili jambo tukaliongelee ofisini kwangu kule"

Tulitoka wote watatu tuenda ofisini kwa william muda ambapo tulipanda lift kuelekea juu zaidi. Tulitumia sekunde 30 tukatokea ilipo ofisi ya william sote watatu tukaingia ndani tayari kwa majadiliano.
**************

"Emmy umeona huyu mtu unamtambua?

Aliongea sam akimvuta mwanaume ambaye alichukuliwa na cctv ya pale hotelini japo sura haikuonekana ila alikuwa ni mwanaume mweusi mwenye mwili mkubwa william aliama na kwenda camera ya pili na ya tatu hadi ya nne atuweza kumtambua yule mtu zaidi ya sura yake kujificha na inaonekana alikuwa anajua kuwa pale palikuwa na camra za usalama alijitaidi kukwepesha sura mpk mwisho hatuweza kumuona yeye wala sam aliyepita kweny uso wa camera.

" hii ni kubwa emmy sasa tunafanyaje willy? Aliongea jimmy

"Nimekaa zaidi ya masaa manane kufatilia hili ila sijapata jibu sasa tuliacha ili itakuwa ni hasara kwako emmy na kubwa zaidi kwangu ambye ndo mkuu wa usalama hapa" aliongea william akionyesha kuchanganyikiwa

"Sasa emmy nikuulize kitu kimoja wakati unakuja hapa ni watu wangapi walikuwa wanalijua hili?
Aliuliza jimmy.

" nina rafiki yangu anaitwa salma pekee anajua"

"Anhaaa una ugomvi nae labda au mliwahi kukwaruzana hapo awali?
Alidakia william

" noo sijawahi kugombana nae"

"Sawa unajihusisha na nini hapa mjini na huyu rafiki yako anafanya shughuli gani?
Aliendelea william kuniuliza

" mimi ni mfanyabiashara za ujasiriamali na salma ni mtu ninayesaidiana nae"

"Sawa sasa salma ana ukaribu gani na mpnzi wako(sam)"

"Yani tunaishi wote mtaa mmoja ila sam tumepanga sehemu moja ila kwa muda nimekuwa sipo hapo nimeamia kijichi kule uwa naenda pia(temeke)

" ahaa sasa unahisi au uliwahi kuhisi km salma anampenda sam?

"Sikuwahi kuhisi kwani awaha ukaribu kabisa"

"Uko kijichi unaishi na nani na temeke ulikuwa unakaa na nani?

" mmmh kijichi nilinunuliwa nyumba na mpenzi wangu mwingine anaitwa elibariki kimaro na temeke ninaishi na mama mdogo wangu ambapo sam ni jirani yetu"

"Hapo naanza kukuelewa je sam na huyu elly vipato vyao vipoje na wewe una ukaribu zaidi na yupi kati ya hao wawili?

" sam ni mwanafunzi wa chuo kikuu mlimani na elibariki yeye ni mfanyabiashara, ila amenisaidia sana kiuchumi ila hapo kabla nilikuwa nimeshanza mahusiano na sam hivyo nipo nao wote ila nampenda sana sam"

"Salma ana ukaribu gani na elly?

Nilichukua muda kulijibu lile swali kwani nilianza kufikiria jambo ambalo liliwahi kutokea huko nyuma.

TURUDI NYUMA.
(Simulizi ya emmy kwa william na jimmy)

Nakumbuka kuna siku nilikuwa nimetoka shule sikuwa nimewasiliana na salma muda mrefu kutokana na ratiba zangu za shule na pia kuamia kwangu kijichi kulinifanya nikose time kabisa. Siku hiyo nilimua kupitia temeke nikaona sio mbaya nipitie kwao na salma nilikuwa dirishani kwa salma nikijaribu kumtisha ile nachungulia nilimuona salma kalala kitandani anaongea na simu nilifanikiwa kusikia maneno machache " na ukitaka kujua mengi kuhusu yeye nitakwambia ila naomba na mimi unitafutie kazi yani analinga sana siku hizi mmh wenye mapenzi yao"

Nilijua anaongea na shoga yake maana salma kwa kuuza ubuyu hajambo nilimuita ila alishtuka saba akakta hiyo simu aliyokuwa anaongea nayo.

Tuliongea mengi nilikumbuka kuna vocha nilirushiwa na rafiki yangu nikiwa shule kama tarakimu tu ilibiidi nitafute mahali pa kuzinakiri ili niingize.

"Salma niazime simu yako mara moja"

Nilipoishika tu ile simu ujumbe uliingia nikaufungua kwa bahati mbaya "mbona umekata simu sasa ila akikisha unafatilia nakutegemea na unajua mimi huyo mwenzio nampenda sana" nilishtuka nikiitazama ni namba ngeni amby aikusaviwa ilikuwa ni voda ya elibariki kabisa hapo nilishangaa ila aliposikia mlio wa ujumbe kuingia alinipokonya simu yake...

Niliishia kushangaa kwa lile jambo ila sikutaka kulifatilia tuliendelea na story nyingine kisha niliaga na kuondoka japo yeye alikuwa anajishtukia mno.

"Emmy nikusaidie mkoba basi"

Nilimshangaa maana si kwa kujibaraguza kule ila sikuwa na time nae nilimkatalia tu. Na kumbuka hapo nilikuwa nafikiria nimpate mtu wa kuishi nae kijichi anisaidie hata usafi maana nyumba ni kubwa mno na nipo alone(mpweke) nilipoona zile dalili za salma niliogopa kumsogeza karibu na nyumbani kabisa.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger

Chapisha Maoni