PENZI LA DADA (9)

Zephiline F Ezekiel
PENZI LA DADA (9)
JINA: PENZI LA DADA Mwandishi: Khamis Kambi SEHEMU YA TISA ILIPOISHIA... "John niambie nn uliota unanipa wasiwasi" baada ya kuona sasa nnakoelekea naweza kuulizwa maswali mengi nikaamua kutunga tu! ili nikwepe maswali "niliota tumepata ajali niliogopa sana ndio mana unaniona nna waswas!" NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... "Ooooh! John basi mm nipo hapa ilikua nindoto isikuumize sana" basi tukakumbatiana lakini bado wasiwasi wangu haukunitoka nikawa nahisi itakuaje endapo siku Coleen angenikuta namfanyia vile ambavyo hua namfanyia angenipiga kama alivyofanya!? swali hilo halikuacha kunisumbua akilini hata baada ya masaa 2 kupita Coleen akapitiwa tena na usingizi mm nilikua bado nimekaa tu! pembeni namuangalia ila haikuchukua mda sana na mm nikapitiwa nikiwa nimekaa katika kiti kidogo pembeni ya kitanda nikaja kushtuka baada ya Sweeet kunishtua asubuhi amkaaa! mjomba ndio nami nikaamka kisha nikasalimiana na watoto Coleen nae akaja, nikasalimian…