UTAMU WA JIRANI (13)
JINA: UTAMU WA JIRANI Mwandishi: Dismas Godfrey SEHEMU YA KUMI NA TATU ILIPOISHIA... Alikuwa ni mzee wa makamo kiasi huku kichwa chake kikiwa kimejaa mvi nyingi kama mtu mwenye miaka tisini na kuendelea mikononi mwake alikuwa ameshika kibuyu na msinga huku mwilini mwake akiwa amejiviringishia kamba zilizojifunga vifundovifundo kama vile ilizi kidevuni mwake alikuwa na ndevu mbili zilizojisokota kama rasta huku akiwa amevaa kaniki nyeusi iliyojitanda kama khanga. NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... Mganga yule alipofika mahala pale nilipokuwa nimelala akatoa msinga wake na kuanza kunizungushia kichwani mwangu kizunguzungu cha haja kilinipata baada ya mganga yule kunizungushia msinga ule na haikuchukua mda mrefu nikapitiwa na usingizi mzito mwanga mkali wa jua uliokuwa unanipiga usoni ndiyo uliyonitoa kwenye dimbwi la usingizi ule mzito nilinyanyuka kiuvivu na kuanza kupekecha macho huku nikipiga mihayo mfululizo ambayo ilitokana na uchovu mkali wa kulala pi…