
SEHEMU YA TISA
ILIPOISHIA...
Mama alizuka kila kona kuangalia uwezekano wa kuchangiwa damu bila mafanikio, alikodi vijana wawakamate watu walionekana kuranda randa mtaani waje wapime damu kama ikiwezekana ikiwa salama wanichangie lakini hadi watano hapakupatikana hata mmoja.
Hali ilizidi kuwa mbaya zaidi nikawekwa kwenye life support machine na ili hali mama ameficha siri nzito katika # secret_diary.
NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
WHO ONE CAN SAVE MY LIFE?
SONGA MBELE..
Hapo paliitajika kudra za mwenyezi mungu kupona, nilikumbuka niliwahi kuchangia damu salama mara mbili nikiwa shule nilikuwa na card yangu kwenye kabati alipokuja dada mary mtoto wa mjomba nikamuandikia kwenye kikaratasi "nenda chumbani kwangu fungua kabati tafuta kadi ya uchangiaji damu salama ilete dada yangu huu ndo msahada wako wa mwis" nilishindwa kumalizia kutokana na hali kuzidi kuwa mbaya kuna kipindi nilikuwa napoteza fahamu kabisa na wakati mwingne kama huu ninakuwa sawa na ninaweza kumtambua kila anayekuja.
***
Namshukuru mungu nilianza kupata afuheni baada ya kuchangiwa damu, nakumbuka kuna siku walikuja watumishi wa mungu ambao ufanyakazi ya kuwatembelea wagonjwa mahospitalini na kuwaombea au kwa wale wahitaji upewa mahitaji madogo madogo. Walikuja hadi kule ICU na kunikuta bado napumulia machine huku damu ikiingia mwilini mama aliwaruhusu waniombee na walipomaliza wakatoa namba zao wakaondoka.
Mambo yalienda vizuri nikaanza kupata afya na kuruhusiwa kurudi nyumbani sikuwa na nguvu kabisa nilikuwa napepesuka na aliyeniona angejua tu mimi naumwa sana. Nilikuwa ni mtu wa kulala tu na mara chache nilianza kufanya mazoezi ya mwili madogomadogo, sikuwai kumuona dadie akija kuniona na hata familia aliisusa na kuamia kwa demu wake mamdogo jane.
Nakumbuka siku moja wanafamilia waliandaa kikao kujaribu kupatanisha ili mamie na dadie warudiane kama zamani na kumaliza tofauti zao. Kweli dadie alikuja japo kwa kuchelewa na kama bahati wale watumishi nao walikuja kututembelea wakakuta kikao nao wakawa sehemu ya kile kikao, yaliongeleka mengi sana kila mtu akimlaumu mwenzie. Sijui alitokea wapi sister mary alikuwa na ile diary yangu nilitamani kumzuia asisome mbele ya hadhira lakini nilishindwa kumzuia akaanza kusoma yale yote yaliyo ndani ya # my_secret_diary nilikuwa situlÃi kwenye kiti hasa mambo ya mama ya kutembea na mfanyakazi wa garden
Mzée pia kutembea na ashura, kumjengea nyumba mamdogo jane na kumsomesha mdogo wake princes wote walishika vichwa baada ya kuwepo hadi tarehe ya matukio yaliyofanyika na mahali yalipofanyikia. Yalianza ya kwangu watu walingua vilio na hakuna aliyeamini kwa umri wangu huu ningeweza kufanya niliyoyafanya nilitembea na ashura, mamdogo jane mdogo wake princes, mfanyakazi wa dukani kwetu/ lisah, kibaya zaidi nilipotembea na wanafunzi wa masasi girls wasiopungua 20 na huo ndo ulikuwa mwanzo wa kuumwa nikaamua kuokoka napo sikusimama nikatembea na wasichana wengine wawili na wa mwisho alikuwa ni matroni sikujui huu ugonjwa niliupata kutoka kwa nani hapo, nilipiga magoti nikalia machozi mengi, mama na baba pia wakaungana na mimi kisha ashura na makele wote tukatubu mbele za mungu kwa kuongozwa sala ya toba.
***
Namshukuru mungu kwa sasa nasoma shule ya seminary huku natumia muda wangu kuwahubiri vijana wenzangu juu ya nguvu za mungu na kuwapa ushuhuda kwa yaliyonitokea wengi wao wameamini japo wengne wamekuwa wakinikejeri bado nasonga mbele. Mama ni mwinjilisti pale kanisani calvary assemblies of God na dadie sasa anasomea uchungaji dodoma. Nimejifunza mengi sana kuwa mungu akiamua kukubadilisha hata kwa dakika moja utabadilika kama alivyokuwa sauli ambae hapo baadae aliitwa mtume paulo.
¤GOD MAKES THE WAY FOR THE SEEMS TO BE NO WAY¤
***MWISHO WA SEASON 1***
***TUENDELEE NA SEASON 2***
"jacob kuna kitabu nimekipata library/maktaba ni cha mambo ya magic sana ebu kiangalie"
"wow steve unajua me napenda sana kusoma kama hivyo maana natamani siku moja nije kuwa mchungaji kama baba yangu na pia nataka nitoe nakala nyingi juu ya kile nitakachokifanyia utafiti"
"vipi juu ya nguvu za giza unaamini zinatenda kazi? Maana hapo pananipa shda"
"sikiliza nikwambie steve na hii ni siri nakwambia wewe kama rafiki yangu wa pekee, kumtegemea mungu kuna faida hapa nilipo nimeshafanya uchafu wa kila aina ebu ngoja nikuletee diary yangu ilikuwa ni # my_secret_diary hakuna mtu aliijua"
Niliinama na kufungua tranka langu la vitabu na kufunua kifuko kilichokuwa chini ya tranka na kutoa diary mbili moja ilikuwa mpya na nyingne ilikuwa ya zamani ambyo ndio yenye historia ya maisha yangu ya shule nikamkabidhi steve akaanza kuisoma kwa takribani dakika kumi.
"dah kaka ni wewe huyu au ni ndugu yako!!!!;"
"kaka ni mimi si unaona hata mwandiko si wa kwangu?"
"ndio wa kwako kweli mungu yupo leo unahubiri mstalini unaimba na watu wanaokoka unasifika una tabia njema hadi shule nzima wanakujua hadi wakurugenzi wa shule mr&mrs laurance kumbe umetoka mbali kaka mungu akusaidia kaka"
"amen! Tena kaka hapa nilipo ni muathirika na ndio maana nimeamua kutoa maisha yangu yaliyobaki kwa mungu"
"dah kaka bado siamini kabisa na huo ni ushuhuda mkubwa sana utakaobadilisha maisha ya wengi me nakuahidi nitakuwa na wewe bega kwa bega"
"nitashukuru sana kaka na ndio maana nimekuja hapa mungu ana makusudi yake"
Nilirudisha ile diary kisha nikaitoa ile mpya "sasa steve hii ni diary yangu mpya ya maisha yangu mapya" steve alicheka sana na kuniachia kile kitabu kilichoandikwa juu "the magic island" nilipomaliza kupanga vitu vyangu nikavuta kiti na meza mulemule bwenini nikaanza kusoma.
Kadiri nilivyoanza kukisoma kile kitabu nilijikuta kama nipo ndani ya kile kitabu maana mwandish aliyeandika kile kitabu alifanya wewe unayesoma uwe muhusika katika kile kitabu, ni kitabu cha mambo ya kale na kilitisha mno nami nilijikuta akili zangu zinaama kuna sehemu nilisoma "baada ya kuingia kwenye kile chumba ambacho manahodha wa ile meli walikufa kila mmoja kwa wakati tofauti nilistajabu kukuta ile meli inaenda bila kuwepo kwa nahodha mwili ulinisisimka na upepo mkali ukavuma ndani ya kile chumba hadi nywele zikasisimka" nilichokuwa nakisoma kwenye kitabu kilikuwa kinatokea pia katika hali ya kawaida nywele zilinisisimka sana nikajikuta nimejawa na uoga sana.
"hey jacob! Jacob! We jb vipi?"
Alikuja pascal na kunitikisa baada ya kuona kama naweweseka vile. Kitendo kile kilinirudisha katika hali ya kawaida.
"vipi paschal?"
"safi mbna ulikuwa unatetemeka sana?"
"paschal we acha tu ebu ngoja niandike kumbukumbu hiki kitabu sitakuja kukisahau"
Nilitoa diary ile mpya nikaandika kwenye page ya mwanzo kabisa 15/09-the magic island book sitakuja kusahau namna nilivyoyajua mambo mengi ya nguvu za gÃza yanavyotenda kazi" nilimaliza kurekodi nikawa namsikiliza paschal.
"kaka mchungaji anakuita amina zodo amepandwa na mashetani uende ukamuombe ofisini kwake"
Nilivaa tshirt harakaharaka nikawa napandisha ngazi kuelekea ofisini kwa mchungaji, nilipofungua mlango nilimkuta mchungaji kalowa tepetepe kwa jasho kwa ajiri ya kumuombea amina zodo. Nilimfata hadi karibu hapo ndo mchungaji akaniambia.
"sasa jacob wewe mfanyie maombi me naenda kubadilisha nguo nakuja humu ndani ufunge atakiwi kuingia mtu wasilete dhihaka"
"sawa mchungaji"
Kitendo cha mchungaji kutoka nikafunga mlango kwa ndani ile nageuka amina alikuwa amevua nguo zote hadi nguo ya ndani na kubakiwa mtupu.
Nilihisi ili jaribu ni kubwa na mwanaume rijali kama mimi kulishnda inahitajika roho wa mungu haswaa kwani alikuwa anavutia sana na maeneo yote yenye kumfanya mwanaume yeyote adate yalikuwa wazi kabisa roho mbili zikawa zinakindhana ndani yangu.
"wewe fanya ebu ona pale chni ya kitovu palivyonona?
"jacob wewe ni mtumish wa mungu usifanye ikimbie dhambi kumbuka dhambi yeyote haifanyayo mwanadamu ni nje ya mwili lakini dhambi ya uzinifu unaifanya ndani ya mwili wako na tena unalichafua hekalu la mungu, kumbuka pia wewe ni muathirika unataka kumuambukiza hata huyu nae ni innocent?"
Zile roho zilikidhana sana nikakumbuka ile stori ya yusufu aliyeikimbia dhambi ya kuzini na mke wa bosi wake{mwanzo18/26} na mimi nikalipoona vile nikaona ndo wakati wangu wa kukimbia nikafungua mlango na kutoka nje kama bahati nikakutana na patricia kiongozi wa dini/spiritual leader nikamwambia waende na rafiki yake wakamvalishe amina huku mimi nikiwafata kwa nyuma.
"mama yangu wee frora umeona amina alichofanya?"
"ooh my Godnes kweli jacob una roho wa mungu angekuwa kijana mwingne asingemuasha hivihivi huyu ana pepo la ngono sio bure"
Nilibaki nje mpaka walipomvalisha nguo wakaniruhusu niingie sasa, nilipoingia nilianza maombi ya kujitakasa kwanza mimi mwenyewe kisha nikaanza kupiga fire pale huku patricia na frola wakiimba wimbo wa kuabudu yale mapepo yalifulumuka yakawa yanataja mambo yangu ya nyuma ili kunimaliza nguvu nisifanye maombi lakini nilisimama imara mpaka yakatoka muda huo amina hajiwezi kwani alishagalagala na kujibamiza ukutani sana.
"amina"
"abee"
"unajisikiaje sasa hivi?"
"najisikia mwili wote unauma hasa kwanzia kichwani"
"ebu nikuulize swali katika familia yenu kuna mtu anapandishaga mashetani"
"ndio yani mama yangu na mimi pia na hata nilipokuwa o-level ubungo islamic niliwahi kujirusha kama lotion moja mpaka chni na mara zote nikipandisha mpaka waje wa kama nane ndo wanaweza kunituliza nashangaa nyie mpo watatu tu"
"ni mungu wala sio sisi watatu ukimwamini mungu hayatakurudia tena, unaamini?"
"naamini tena siyapendi maana kila mara nikipandisha lazima nikalazwe maana huwa naumia alafu mama atajua tu kama mmeyatoa nahisi atapiga simu kuulizia"
"we usiogope yatakwisha"
***
Nilipata umaarufu wa ghafla kila sehemu niliyokuwa napita utasikia pastor Jb kutokana na ile skendo ya kumkimbia amina akiwa uchi kuna walio niona mjinga kwani amina anavutia na anashepu nzuri hapo akivaa nguo sasa ilikuaje alipotoa nguo? Kuna walionisifia hasa walimu, uongozi wa juu na mchungaji alimpigia simu baba na mama mbele yangu.
"yani mchungaji hongera kweli umemlea mtoto vizuri"
"yani mchungaji namshukuru mungu jacob hakuwa hvyo alivyo leo ni mungu tu ukisimuliwa mambo aliyoyafanya huko ndanda boys na masasi girls ameasha historia mpaka leo wananipiaga simu kumuulizia nawaambia jacob amebadilika"
Waliongea pale nikamuaga mchungaji kwakuwa ilikuwa mida ya jioni jioni nilienda darasani kuchukua begi langu ili nilipeleke bwenini kwa bahati mbaya nilimkuta msichana mmoja anaitwa azinaeli yupo combi ya ECA nilimsalimia kisha nikafungua meza yangu na kutoa begi na kufunga tena wakati nafika mlango nilisikia naitwa.
Nilipogeuka alikuwa azinael tena amefunua sketi yake na kunionyesha nyeti zake huku akiniita kwa kidole niende "ooh my God"
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com