SORRY MADAM (2)

Zephiline F Ezekiel
SORRY MADAM (2)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA PILI ILIPOISHIA... Usiku mzima sikulala kutokana na mawazo ya kuhisi inaweza ikawa ndio safari yangu ya mwisho katika shule hiyo.Ila kingine kinachonifanya nishindwe kulala ni kutokana na hali ngumu iliyokuwemo ndani ya kibanda hicho kwani kina meza na viti viwili na mbaya zaidi hawakunipa hata shuka la kujifunika kujikinga na baridi kali iliopo hapa mkoani Arusha . NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... Kila wakati ninaangalia saa yangu ya mkononi huku nikiomba asubuhi iweze kufika kwa haraka.Saa kumi na mbili na nusu waalimu wakaanza kuingia katika geti la shule ambalo lipo karibu na kibanda cha walinzi.Nikamuona Madam Mery akiingia getini na kituo chake cha kwanza akafika katika kibanda nilichopo.Akasalimiana na walinzi waliopo katika kibanda hicho huku akionekana kunishangaa kuniona katika kibanda hicho “Ehee Eddy vipi mbona huku asubuhi yote!?” “Madam wee acha tu jana” “Niache nini sasa jamani kaka…