SORRY MADAM (34)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA THELATHINI NA NNE ILIPOISHIA... Kuepusha shari nikatoka kwenye kituo cha polisi na kuingia ndani ya gari na kumsubiria Sheila ambaye baada ya robo saa akatoka na kuingia ndani ya gari “Wamesemaje?” “Wametaka tuwalipe gharama za matibabu pamoja na gharama za vitu vilivyo haribika kwenye hoteli.Kumbe yule mzee ndio mmiliki wa hoteli na yule mwanaye alikuwa kama msimamizi pale” NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... “Na wanataka kiasi gani cha pesa” “Milioni moja na nusu” “Waache upuuzi wao tuondoke watapewa na babu zao” “Eddy” “Tuondoke zetu wasilete uhuni yeye si amesema sisi hatuwezi kumlipa basi achana nao” “Edd achana kuwa mbishi mume wangu wameniomba nije kujadiliana na wewe ili tujue tunawalipa nini?” “Ahaa basi majadiliano yetu mimi na wewe ni kwamba hakuna swala la kuwalipa cha msingi tuondoke zetu kwanza ninahitaji tufike Dar leo hii kabla ya saa nne usiku na sasa hivi ni saa kumi na mbili jioni” “Edd…