SEHEMU YA SABINI
ILIPOISHIA...
Moyo ukaanza kunienda mbio huku mapigo ya kawaida yakibadilika na kuwa ya kasi sana kiasi kwamba nikaanza kujihisi vibaya
“Ahh….haaa sio mimi?”
Wakanitazama kwa umakini
“Samanani ninaomba niende msalani”
NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
Nikawaaga na kunyanyuka, nikatamani kutoka nje ya baa ila macho yao yote tapo kwangu, nikamuuliza muhudumu ni wapi kilipo choo, akanielekeza na bahati mbaya kipo ndani ya baa hii na kama kingekuwa ni nje ingekuwa ni nafasi nzuri ya mimi kuwakimbia.Nikaingia chooni na kusimama kwenye moja ya kioo kilichomo humu ndani, nikaivua kofia yangu na kujitazama vuzuri
“Sijabadilika chochote usoni mwangu”
Nilizungumza kwa sauti ya chini, nikajiweka sawa na kuivaa kofia yangu na taratibu nikaanza kuelekea ulipo mlango, nikakishika kitasa cha mlango huku nikiwa ninahema sana, nikashusha pumzi nyingi na kuufungua mlango, nikapiga hatua mbili, gafla nikastukia nikizibwa pua na kitambaa chenye harufu ambayo tangu nizaliwe sikuwahi kuinusa, mtu aliye nikaba kwa nyma sikujua ni nani, na nilipo jaribu kuminyana naye, ndvyo naye alivyozidi kukikandamiza kitambaa puani mwangu na taratibu nikajikuta nguvu zikiniishia na nikapoteza fahamu.
***
Kwa mbali nikaanza kuona kitu nikiwa kinazunguka juu yangu, nikajaribu kuyakaza macho yangu, ila bado nikashindwa kuyafumbua, nikutokana na uchomvu mwingi ulio ambatana na usingizi mzito, nikajaribu kuinyanyua mikono yangu ila nikaihisi kuwa ni mizito sana, nikakigeuza kichwa changu upande wa kushoto na kukuta jamaa lenye miraba miine likiwa limekaa kwenye kiti, huku sura yake ikiwa na mindevu mingi sana.Hapa ndipo nilipo anza kugundua kwamba nimelala chali juu ya kindanda, sikuona kitu chochote kilicho ufunga mkono wangu, na sikuelewa ni kwanini nimekuwa mchovu kwenye mikono kiasi hichi
Nikaendelea kuvuta kumbukumbu ya nimefika vipi katika eneo hili, ila ubongo haukusoma kitu chochote zaidi ya kukumbuka kwamba nilikuwa nipo baa.Baada ya masaa kadhaa nguvu za mwili wangu zikaanza kurejea taratibu, nikapata nguvu hata ya kuyafumbua macho yangu hapo ndipo nikagundua kitu kinacho zunguka juu yangu ni feni
“Nipo wapi?”
Nilimuuliza jamaa, hakunijibu chochote zaidi ya kunitazamaa kwa macho makali, hukua akiendelea kuzichezea ndevu zake nyingi nyingi
“Nipo wapi?”
“Wee koma”
Jamaa alizungumza huku akininyooshea kidole, akionekana kukasirishwa na swali langu nililo tumia sauti ya ukali kumuuliza.Akasimama na kuitoa simu yake ya mfukoni
“Mtu wenu ameamka”
Sikujua anazungumza na nani, mapigo ya moyo yakaanza upya kudunda huku yakiandamana na wasiwasi mwingi, wazo la kwanza kunijia kichwani nikajua tarari nimeingia kwenye mikono ya Mzee Godwin, nikajaribu kusimama ila jamaa kwa haraka akaniwahi kunisukuma kitandani
“Ukilete ujinga jombaa nitakupoteza duniani?”
Nikazidi kuchanganyikiwa, baada ya muda wakaingia Rajiti na Sashah, wote wawili wamevalia suruali nyeusi na tisheti nyeusi, huku miguni wakiwa wamevaa, buti nyeusi
“Habari yako, Eddy?”
Rajiti alinisalimia, hapo ndipo nikadata kabisa na kutambua kwamba hawa si watu wazuri kwangu, kutokana niliwatambulisha kwa jina la Thomas, inakuwaje wananiita mimi Eddy
“Kamletee chakula”
Jamaa likatoka na kutuacha ndani ya chumba
“Eddy ninaimani utajiuliza imekuwaje hadi upo hapa” Sashah alizungumza
“Ndio”
Rajit akatoa picha mfukoni na kunirushia mimi kitandani nilipo lala, picha aliyo nirushia ina sura yangu na mama yangu zikiwa zimeambatanishwa kwa pamoja na kuitoa picha moja
“Usishangae sana, na kujiuliza ni wapi tumeitoa picha yako, kwa ufupi sisi tulikufwatilia kwa siku nyingi hadi jana tulipo fanikiwa kukupata” Rajit alizungumza
“Munataka nini kutoka kwangu?”
“Kikubwa tunacho kihitaji sisi ni wewe kukusaidia”
“Kunisaidia kivipi?”
“Utaelewa”
“Sisi ni wanajeshi wa kikundi cha Al-khaida, na kazi yetu kubwa ni kutafuta vijana wenye matukio makubwa kama yako, pia isitoshe tunahitaji kukupa msaada wa kumpata mama yako”
Baunsa akaingia huku akiwa amebeba sahani kubwa yenye vitu mbali mbali vya kufungua kinywa, akaviweka kwenye meza na kutoka nje
“Tunahitaji tukupeleke Iraq, yalipo makazi yetu kisha ukirudi Tanzania tukusaidia kwenye kazi moja tu”
Rajit alizungumza
“Kazi gani, unajua hadi sasa hivi sijawaelewa?”
“Eddy fungua akili yako, Tanzania nzima unatafutwa wewe, Je ukikamatwa ni wapi utapelekwa?”
“Gerezani” Nilimjibu Rajit
“Je upo tayari kuishi, gerezani?”
Swali la Rajiti likanifanya nikae kimya pasipo kumjibu chochote
“Hapa kwani nilipo ni wapi?”
“Hapa ni Mombasa, nchini Kenya.Jana tulisafiri usiku kucha hadi hapa”
“Kwa nini muniteke?”
“Ilitulazimu”
Rajiti na Sashah wakendelea kunishawishi hadi nikakubali kwenda nao Iraq kwani nikiangalia kwa jinsi maisha yangu yalivyo ya kuruka ruka kama ndege nikaona ipo siku nitanaswa kwenye jumba bovu.Akaja daktari mwenye asili ya kiarabu, waliye niambia anahusika na kazi ya kuchonhesha sura bandia, dakatari akanifanyia vipimo vya haraka na kazi ya kuchongesha sura nyingine itakayo kaa sawa kwenye uso wangu ikaanza mara moja.Ndani ya masaa sita tarari daktari akawa ameikamilisha kazi aliyo agizwa na Sashah.Kazi ya kupandikizwa sura bandia ikaanza mara moja, huku daktari akiifanya kwa umakini wa hali ya juu, haikuchukua muda mwingi sana kuvishwa sura bandia, nikaa lisaa moja kwenye kifaa ambacho daktari aliniambia kinaghusika na swala zima la kuikausha sura yangu mpya
Baada ya zoezi zima la kubadilishwa sura kuisha, Rajiti akanipa kioo niitazame sura yangu niliyo pandikizwa juu ya sura yangu halisi, sikuyaamini macho yangu kwani nimebadilika kupita maelezo hata mimi mwenyewe nikajisau
“Ebwaane eheee ni mimi kweli au naota?”
“Ni wewe, mbona hapo umetokelezea”
“Etii eheee?”
“Ndio”
“Hahaaaa”
“Sashah yupo wapi?”
“Amekwenda Mjini mara moja”
Sashah akarejea akiwa na furaha sana usoni mwake,
“Vipi kitu kimetiki nini?” Rajiti aluliza
“Ndio, chezea mimi wewe”
Rajiti akamkbidhi Sashah hati tatu za kusafiria, na akaanza kuzisoma taratibu
“Kweli wewe kiboko, kitu feki kama orijino”
“Ahaa, kila kitu kinawezekana duniani”
“Ila kipo kisicho wezekana” nilichangia mada
“Kama?”
“Kutengeneza pumzi ya mtu”
“Kweli”
“Mpe Eddy aone passport yake jinsi nilivyo itengeneza”
Sashah akanikabidhi hati yangu ya kusafiria iliyo na sura yangu mpya, huku jina langu likiwa ni Suleima Bin Yahaya
“Mbona jina ni hili?”
“Nisingeweza kuweka jina lako kutokana na wewe kuwa muhalifu, hapa mwenyewe nimetoka Jomo Kenyeata Airport na kuzikuta picha za sura yako zikiwa zemebandikwa kwamba unatafutwa”
“Mmmm”
“Unaguna? Tutakwenda na utaziona”
“Sawa bwana”
“Eheee umekata tiketi ya ndege ya saa ngapi?” Rajit aliuliza
“Saa sita uskuku”
“Ipo powa”
Tukaendelea kupiga stori za hapa na pele na nikawasimulia mkasa mzima wa nyuma uliopita kwenye maisha yangu, hadi ninamaliza wote machozi yakawa yanawamwagika
“Eddy pole sana”
“Asante”
Sashah na Rajiti wakabadilisha mavazi na kuvalia sketi ndefu nzuri na kuwafanya wapendeze sana, huku na mimi nikivalia suti kali waliyo nipa cha kushukuru Mungu imenikaa vizuri mwilini mwangu na kunifanya nionekane kama muheshimiwa wa kitengo fulani cha serikali.Tukaanza safari kwa kutumia usafiri wa gari yao ndogo, inayokwenda kwa kasi sana, kutokana ni usiku hapakuwa na magari mengi sana barabarani,Tukafika katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyata, sote tukashuku na zimesalia dakika ishirini kabla ya ndege tunayo ondoka nayo kupaa angani.Moja kwa moja tuakelekea sehemui ya ukaguzi wa hati za kusafiria, Rajiti akawa wa kwanza kukaguliwa hati yake pamoja na mwili wake kwa kutumia kifaa cha ulinzi, akapita na kupewa hati yake iliyo tiwa muhuri na muhudumu wa kike anaye ifanya kazi hiyo huku akionekana kuwa makini sana, akafatia Sashah akakaguliwa kama alivyo fanyiwa Rajit na akafanikiwa kupia
Nikamkabidhi msichana hati yangu ya kusafiria cha kwanza akanitazama machoni, kisha hati yangu ya kusafiria akaiweka kwenye mashine inayotoa ripoti kwenye kioo kikubwa cha ‘computer’.Askari anaye kagua akaanza kazi yake ya kukipitisha kifaa chake kuanzia miguuni, msichana akanitazama kwa macho makali kisha akatazama tena kwenye kioo cha kumputer yake, nikatazama pembeni na kuwaona askari wawili walio shika mbwa wakubwa weusi wakianza kunisogelea, huku wakiwa na bubduki zao mikononi, kifaa cha ukaguzi kikaanza kutoa mlio wa kelele huku kikiwaka taa nyekundu kilipo fika maeneo ya shingoni
“Vua cheni yako”
Askari anaye nikagua aliniambia na kunifanya niivue cheni, niliyo ivaa shingoni mwangu.Akaendelea kukipitisha kifaa chake kwenye mgongo hadi chini kwenye miguu,
“Safari njema”
Dada aliyekuwa anaikagua hati yangu ya kusafiria alizungumza huku akinikabidhi hati yangu ya kusafiria, huku usoni mwake akiwa ameachia tabasamu pana lililo pendezeshwa na mwanya wake mwembamba.
“Asante na wewe pia kazi njema”
Nikapita kwenye kizuizi na kuwafanya Sashah na Rajiti kushusha pumzi nyingi kwani walihisi kwamba tayari nimeingia kwenye mikono ya askari, tukaingia ndani ya ndege, cha kushukuru Mungu, siti zetu tatu zipo sehemu mmoja, hatukukaa hata dakika nyingi, rubani akatuomba tufunge mikanda yetu kwani ndege itajiandaa kuruka muda sio mrefu.Ndani ya dakika kadhaa tukaanza kuiacha ardhi ya nchini Kenya
“Eddy” Rajiti aliniita
“Naam”
“Unajua kwamba unaonekana tofauti sana”
Alizungumza kwa sauti ndogo
“Kweli?”
“Ndio, umekuwa bonge la handsome”
“Mmmmm”
“Kweli vile”
“Jamani acheni kelele watu wamelala” Sashah alizungumza
“Ahaaa shauri yao, bwana”
Masaa yakazidi kusongo mbele, na ndege yetu ikatua baadhi ya nchi ambapo, baadhi ya abiria walishuka na kupanda abaria wengine na safari ikaendelea.Tukafika nchini Iraq, majira ya saa moja saa tisa alasiri huku sote tukiwa tumechoka kwa uchovu wa kukaa kwenye ndege takribani masaa kumi na tano, kutokana hatukuwa na mizigo tukawahi kupanga mstari wa kutokea sehemu ya kukaguliwa, huku moyoni mwangu nikiwa ni naomba sana nisiweze kushtukiwa kwa lolote, na nikafanikiwa kutoka njee ya uwanja wa ndege pasipo mtu yoyote kunistukia kwamba nimevalia sura bandia,
Sikuwa na sehemu yoyoote ninayo itambua na wenyeji wangu wakubwa ni Sashah na Rajit.Tukapanda kwenye taksi mojawapo iliyopo kwenye maegesho ya uwanja wa ndege na Sashah akazungumza kwa lugha ya kiarabu na dereva tuliye mkuta ndani ya teksi hii, Tukafika kwenye moja ya Hotel kubwa iliyo andikwa kwa maandishi ya kiarabu na kila kitu ambacho wanakizungumza Shasha na watu wengine, sikuweza kukifahamu kutokana siitamui lugha ya kiarabu
Sashah akamaliza kuzungumza, na wahudumu na akakabidhiwa funguo moja, akatufwata sehemu tulipo simama na Rajit, tukaingia kwenye lifti iliyo tupeleka hadi ghorofa ya sita, na tukaingia kwenye chumba ambacho Sashah alikodisha
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com