SORRY MADAM (94)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA TISINI NA NNE ILIPOISHIA... “Umekua mwanangu, hadi leo unatimiza miaka ishirini na tato, kweli umekua mwanangu” Nikashikwa na kigugumizi hata sikuweza kuzungumza, mama akanikaribia na kunitazama usoni mwangu, nami nikashindwa kuyazuia machozi yangu. NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... Tukajikuta tukikumbatiana kwa pamoja na kuwafanya watu, waliopo ukumbini kupiga makofi “Nakupenda sana mwanangu, Eddy” Sikutarajia kama ninaweza kukutana na mama yangu, baye nimepotezana naye kwa kipindi kirefu sana “NA…KU..PENDA PIA MAMA” Nilizungumza huku, machozi yakinimwagika, yakiendana na sauti iliyo jaa kigugumizi. Kati ya watu walio simama ukumbibi, nikamuona Sheila , akipiga makofi huku akimwagikwa na machozi ya furaha Taratibu mama akaniachia na kunibusu kwenye paji la uso wangu. Akasimama pembeni yangu nakuniomba nizungumze chochote, kwa watu walio nifanya sasa hivi kuwa na furaha. “Siamini, kitu ninacho kiona mb…