KITABU CHA SHETANI (6)

Zephiline F Ezekiel
KITABU CHA SHETANI (6)
Jina: KITABU CHA SHETANI Mtunzi: Aziz Hashim SEHEMU YA SITA TULIPOISHIA... Tayari yule daktari aliyempiga kikumbo alishamsogelea na kutaka kumtoa kwa nguvu lakini alipoendelea kusisitiza kwamba alikuwa na dawa ya kumsaidia mgonjwa huyo aliyekuwa kwenye hatua za mwisho za uhai wake, IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI 👉INSTALL👈 TUENDELEE... madaktari walitazamana kwa sekunde chache kisha wakapeana ishara ya kumruhusu awasaidie kwani nao walishaonesha kushindwa. Aliporuhusiwa tu, harakaharaka alisogea mpaka kwenye kitanda alichokuwa amelazwa Edmund ambaye bado alikuwa akiendelea kutapatapa, akamchomoa mpira wa kumsaidia kupumua aliokuwa amevalishwa puani na mdomoni kisha kwa kasi ya ajabu akaanza kumpuliza mdomoni. Aliendelea kumpuliza kwa nguvu, baada ya takribani sekunde thelathini za kufanya hivyo, Edmund aliacha kutapatapa, akaendelea kumpuliza na katika hali ambayo hakuna aliyeitegemea, mapigo ya moyo wake yalianza kupanda. Yalipofika katika kiwango …