KITABU CHA SHETANI (8) Jina: KITABU CHA SHETANI Mtunzi: Aziz Hashim SEHEMU YA NANE TULIPOISHIA... “Nimeshawaua wanaume wengi sana Edmund, hata wewe ilikuwa ufe kwa njia hizohizo, nimekuokoa kwa sababu kwa mara ya kwanza maishani mwangu nimetokea kukupenda Edmund, IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI 👉INSTALL👈 TUENDELEE... nimechoka kuwa muuaji! Nimechoka naomba unisaidie kuondokana na hali hii,” alisema Samantha huku akianza upya kuangua kilio kwa uchungu. Maelezo hayo yalimshtua mno Edmund, bado akawa anajihisi yupo ndotoni kwani ilikuwa vigumu sana kuamini kwamba Samantha alikuwa akiongea ukweli. “Kwa hiyo... kwa hiy..o nini huwa kina...to..kea,” Edmund alimuuliza kwa sauti ya kukatakata huku akitetemeka mno kutokana na hofu kubwa iliyokuwa imemuingia, hasa baada ya kuambiwa kwamba hata yeye alitakiwa kufa ila akaponea kwenye tundu la sindano. Samantha akamwambia kwamba anapotongozwa na wanaume, wakishakubaliana kwenda kukutana kimwili, kuna dawa huwa anaitafuna muda mfupi k…