SHINDU LA KIHAYA (1)

Zephiline F Ezekiel
SHINDU LA KIHAYA (1)
Jina: SHINDU LA KIHAYA Mtunzi: Geofrey Malwa SEHEMU YA KWANZA Ilikuwa ni mitaa ya uswahilini kidogo,mahali ambapo gari nzuri kuwasili ni kwa nadra sana,kwa jina mtaa huo ulijulikana kama Machinjioni.Wengi wakazi wa huko walikuwa ni waswahili. Kuna familia moja ambayo ilikuwa inaishi maisha ya kitofauti kidogo japo hawakujitangaza kwa majirani.Maisha ya kubadilishana mboga nzuri na kuvaa vyema hakukuwapiga chenga,kazi ya mama huyo ilikuwa ni kuuza samaki wabichi kabla ya kuwa na maisha mazuri ya kubadilisha mboga wanazozitaka,na walikuwa wawili tu wanaoijenga familia hiyo,mama na mtoto wake aliyeitwa Lisa. Lisa alikuwa ni msichana mzuri sana kupita maelezo,alikuwa ni mwanafunzi wa kidato cha nne,aliwatoa udenda vidume wengi sana mtaani kwao.Kingine kilichomfanya apendwe zaidi na watu ni kutojiona mzuri na kujisikia,aliwapenda watu wote na kuishi nao kama ndugu zake.Kuna muda akipiga dili la maana basi anawapa fedha kidogo watu waliomzunguka kwa mtindo wa mahitaji yao na kwa nyakati tofauti. …