BABA KIUMBE WA AJABU (12)
Jina: BABA KIUMBE WA AJABU Mtunzi: Ally Mbetu SEHEMU YA KUMI NA MBILI TULIPOISHIA... “Mimi na ninyi nani kaamua kumuua mwenzake?” “ Masalu kumbuka baba yetu ni huyuhuyu, akifa hatutampata mwingine.” “Kwani kuna mbadala wa dada Monika , baba ni huyo huyo, dada Monika mwingine yupo wapi?” JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 SASA TUENDELEE... “Masalu makosa yamekwisha fanyika rudisha moyo uokoe maisha ya baba.” “Kwanza mnaniambia hivyo mimi nimemfanya nini baba?” niliwauliza swali gumu. “Inaonekana umekwenda kwa mganga kurudisha nguvu zako za kiume.” “Mlitaka niwe hivihivi milele kwa raha zenu, mbona ninyi mna watoto na wanaume?” “Kwani Masalu upo wapi?” “Tokea lini mlinitafuta?” “Basi zungumza na mama,” baada ya muda nilimsikia mama akiniita. “Masalu.” “Naam mama, shikamoo.” “Marahaba mwanangu upo wapi? hali ya baba yako ni mbaya sana.” “Anaumwa nini?” “Ameanguka kwenye mishughuliko yake, kama ni kweli umefanya wewe njoo umsaidie ba…