
Mtunzi: Halfani Sudy
SEHEMU YA KUMI
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Wakati akiwaza hayo alisikia mlango ukifunguliwa kwa nje. Ukafunguka kidogo na mtu mpya alisukumwa kwa nguvu kuingizwa mle ndani. Dokta Yusha alimwangalia vizuri mtu yule walitambuana.
"Wamekuleta huku Dokta"
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
"Nawe wamekuleta huku"
Ilikuwa ni kushangaana tu. Mtu yule alikuwa ni mmoja wa askari wa kituo cha Polisi Masoko. Tena ndiye askari aliyemhoji dokta Yusha alipoenda Polisi …..
"Eeh imekuwaje ukafika huku" Dokta Yusha aliuliza kwa wahka mkubwa.
Huku akiwa amesimama yule askari alianza kuelezea.
"Ulivyoomba kutoka pale Polisi ili kwenda kwenye mazishi ya Mwanasheria tulikukubalia, lakini ulivyotoka tu tulikubaliana tukufuate kwa nyuma, na ni mimi ndiye niliyepewa jukumu hilo. Nilikufuata kwa nyuma kila ulikoenda. Mpaka wanakuingiza kwenye gari mimi nilikuwa nashuhudia. Lakini nikiwa nimejibanza nyuma ya wodi moja nikisubiri muda muafaka wa kuja kukuokoa, nikiwa pale nyuma ya wodi nilipojificha nilistukia nimepigwa na kitu kizito kisogoni. Toka hapo sikujua nini kiliendelea. Nimeamka toka ndani ya gari dakika kama sita zilizopita na wakanileta moja kwa moja humu"
"Hivi tuko wapi hapa Afande?"
"Hata sifahamu, maana nilizimia kabisa, nimezinduka nimejikuta nipo humu"
"Itakuwa tuko mbali sana Afande, saa nane tumetumia mpaka kufika hapa"
"Saa nane?"
"Ndio, Afande"
"Mh itakuwa wametuleta wapi washenzi hawa" Yule askari alikuwa anaongea huku anapiga hatua kuelekea kukaa katika kile kiti pekee cha chuma mle ndani. Alikikaribia kile kiti na kusema.
"Sijui watakuwa wana mpango gani hawa wanaharamu"
"Nooooo afande usikae hapooooo!" Dokta Yusha alipiga kelele kali kumuonya yule askari asikalie kile kiti chuma, lakini alikuwa amechelewa sana.
Jamaa alikaa kwenye kiti kilichotokea………..Dokta Yusha alifumba macho!
Kiti kilibadirika rangi na kuwa chekundu sana, askari hakutoa hata ukelele mdogo, rangi nyekundu ya kiti ilienda sambamba na rangi ya askari yule. Kumbe kiti kile kilikuwa na shoti ajabu ya umeme!
Dokta Yusha alithubutu kufumbua macho, macho yalimtoka pima! hakutegemea kabisa kitendo kile. Ingawa alikuwa anahisi kiti kile sio kizuri tangu alivyoingia katika chumba kile, lakini hakudhani wala kufikiria kwamba kina madhara namna ile. Yule askari alianza kubadirika rangi tena, akawa mweusi tii huku akikakamaa ilhali kiti kilibaki na rangi yake ileile nyekundu. Dokta Yusha aliyaangalia yote huku huku akitetemeka, mikono yake ikiwa kauziba mdomo wake. Alikuwa anaangalia picha mbaya sana!
Huku akitetemeka dokta Yusha alisimama, kwa kiasi kikubwa akisaidiwa na ukuta katika kumsaidia kunyanyuka pale chini. Alivyosimama tu alikaribishwa na kitu kingine, harufu, ule mwili uliokakamaa pale chini ulianza kutoa harufu kali sana!
Dokta Yusha alijitahidi kubana pumzi ili harufu ile isiyoeleweka isiingie puani mwake, ilikuwa ngumu sana, maana kuendelea kubana pumzi kulimaanisha anakiita kifo chake mwenyewe. Hata hivyo hakutaka kabisa kuvuta harufu ile, aliendea kuziba pumzi huku anaachia mara chache chache, akiwa katika hali hiyo ngumu sana katika maisha yake, mara alisikia kelele za mlango, ishara kuwa mlango ulikuwa unafunguliwa. Mlango ukafunguliwa, aliingia Sita wa Six killers kwa majigambo makubwa sana. Alienda hadi pale ukutani ambako Dokta Yusha alikuwa amesimama.
"Hahaha Dokta nawe unahisi harufu, siamini. Wewe ni daktari bwana unakutana na harufu mbaya zaidi ya hii. Hebu simama" Sita alisema kwa urafiki zaidi.
Dokta Yusha alimwangalia Sita huku akionesha sura ya upole sana. Lakini sura yake ya upole haikusaidia kitu. 'Maji aliyavulia nguo…………..'
"Haya toka nje" Sita wa Six killers alimwambia huku akionesha kwa kidole cha shahada mahali mlango ulipo.
Dokta Yusha alitoka nje ya chumba kile huku akifuatiwa na Sita. Alipotoka tu nje, alikutana na jamaa mmoja akiwa amekaa katika kiti cha plastiki huku anavuta kiko. Jamaa yuleyule aliyekuwa anaongea kwa majivuno na kujiamini kule katika chumba cha kuhifadhia maiti. Alikuwa anaitwa Don Genge.
Dokta Yusha alisimamishwa mbele ya Don Genge huku nyuma yake akiwa amesimama imara Sita. Pembeni ya Don Genge upande wa kushoto walikuwa wamesimama watu wawili, na upande wa kushoto walikuwa wamesimama watu wawili. Don Genge alikuwa kati mithili ya Mfalme.
"Naitwa Don Genge, umeshawahi kulisikia hilo jina" Don Genge aliuliza punde tu Dokta Yusha alivyowasiri pale.
Dokta Yusha alikataa kwa kutingisha kichwa.
"Wewe ni bubu?"
"Hapana"
"Kwanini unapenda sana kufatilia mambo ya watu?" Don Genge aliachana na mwendelezo wa swali la awali na kuuliza swali jipya.
Dokta Yusha alikaa kimya, kimya ambacho kilimkasirisha sana Don Genge.
Don Genge alinyanyuka, akamsogelea Dokta Yusha huku akitabasamu. Ghafla, Don Genge alirusha kibao kilichotua sawia katika shavu la kushoto la Dokta Yusha. Dokta Yusha aliyumba kidogo, kisha akasimama tena wima. Alijishika shavu lake la kushoto kwa mkono wake wa kulia.
"Kwanini unapenda kufatilia mambo ya watu?" Sasa Don Genge aliuuliza uso wake ukiwa karibu sana na uso wa Dokta Yusha.
"Nisamehee sirudii tena" Dokta Yusha aliamua kuomba msamaha bila ya kujielewa.
"Hakuna mtu aliyewahi kuingia katika nyumba hii, akatoka hai, wote wameuwawa, tena kikatili sana! Ila wewe utakufa kifo cha tofauti….." Don Genge aliacha kuongea, aliacha maneno yale yamuuingie vizuri Dokta Yusha. Akavuta kiko kidogo, halafu akampulizia moshi Dokta Yusha. Dokta Yusha alikohoa kutokana na ule moshi.
"………Utakufa kifo cha tofauti sana, utakufa kwa njaa!
Siku nyingi nilikuwa najiuliza hivi binadamu anaweza kukaa siku ngapi bila kula? Lakini nitapata jibu la hilo swali kupitia wewe" Don Genge alikuwa anaongea wakati Dokta Yusha alikuwa anaendelea kukohoa kutokana na ule moshi. Lakini Don Genge hakujari kama kasikia ama hajasikia.
"Hebu mrudishe ndani kule"
"Hapana, musinipeleke katika kile chumba" Dokta Yusha alikuwa anakataa kurudi tena katika chumba kile chenye harufu ya mbaya na ya kuchukiza.
"Kile ndio chumba chako, lile ndio kaburi lako, usilikatae, ulipende Dokta, peleka huyo!"
Sita alimshika suruali kwa nyuma Dokta Yusha mithili ya kibaka ashikwavo na askari na kumrudisha katika kile chumba chenye harufu kali sana…
Hali ilikuwa ngumu sana katika chumba kile, ambacho nd'o ilikuwa selo ya Dokta Yusha, au kubali la Dokta Yusha kama alivyosema Don Genge. Lakini Dokta Yusha ilimbidi akae katika selo ile, hakuwa na jinsi. Aliishi mule kwa hofu kubwa sana, kila kitu alichoongea Don Genge bado kilikuwa kinarindima katika kichwa chake, kwamba kile kitakuwa chumba chake, pia litakuwa nd'o kaburi lake.
"Nakubari kitakuwa chumba changu, tena kwa muda bila shaka, lakini haliwezi kuwa kaburi langu kamwe" Dokta Yusha alijisemea mwenyewe kwa ujasiri.
Sasa alikuwa anaivuta harufu yote ya chumbani, hakuwa anaziba tena pua, aliamua liwalo na liwe, harufu yoyote iingie puani mwake, lakini lazima atoke mle ndani.
Usiku uliingia, usiku ambao Dokta Yusha alipanga nd'o uwe kilele cha yeye kuishi katika selo ile, lazima atoke mle ndani. Ndani ya chumba kile kulikuwa na giza kubwa sana. Dokta Yusha alinyanyuka kwenye sakafu alipokaa na kuusogelea mlango. Alishika komea la mlango na kujaribu kulizungusha taratibu.
Mlango ulikuwa umefungwa!
Dokta Yusha ilimpasa kutafuta njia nyingine mbadala ya kumuwezesha kutoka katika chumba kile cha kifo. Ilimpasa kutumia akili za ziada kutoka katika chumba kile cha mauti.
'Lazima nitoke humu, siwezi kufa kikondoo humu'
Dokta Yusha aliangalia juu ya kile chumba, alikutana na vigae vilivyowezekwa vizuri sana kule juu. Hakuna mjanja atakayeweza kufanya chochote ili kupita katika vigae vile. Ilikuwa ngumu sana!
Dokta Yusha alirudi nyuma, akarejea tena ukutani, akauangalia ukuta, akautomasa ule ukuta kwa kidole, ulikuwa ukuta mgumu sana!
Mlango, ukuta, bati vyote havikumruhusu kabisa Dokta Yusha kutoka katika chumba kile cha hatari.
Dokta Yusha alichoka, alikaa chini ili kusubiri kukiona kifo cha njaa jinsi kinavyokuwa.
Saa kumi kamili alfajiri ilimkuta Dokta Yusha akiwa macho. Alikuwa hajasinzia hata kidogo, muda wote alikuwa anafikiria namna ya kutoka katika chumba kile lakini hakupata namna ya kutoka.
Mara, alisikia tena kelele za mlango kwa nje, ishara kama ya mwanzo kuwa mlango ulikuwa unafunguliwa.
'Ama zake, ama zangu!'
Aliingia tena Sita, akiwa kashika bunduki aina ya SMG mkononi. Alisimama pale mlangoni na kumwangalia Dokta Yusha. Sita wa Six killers alikuwa ameenda kuhakikisha tu kama Dokta Yusha hajafanya ujanja wowote wa kujaribu kutaka kutoroka. Sita alimshuhudia Dokta Yusha akiwa amekaa palepale alipomwacha awali. Akadanganyika kwamba Dokta Yusha hajafanya kitu chochote kile cha kujaribu kutoroka.
Alijidanganya. Dokta Yusha alitafuta sana njia ya kutoka mle ndani lakini hakuipata.
Sita aligeuka nyuma ili arudi nje kuendelea na lindo lake.
Kwa kasi ya haraka Dokta Yusha alinyanyuka pale chini na kupiga hatua mbili kubwa sana, hatua zilizomfikisha mpaka pale mlangoni. Alipokuwa Sita wa Six killers.
Wakati Sita anataka kugeuka nyuma kujua sababu ya vishindo viwili alivyovisikia, alichelewa sana!
Alikuwa kakabwa vizuri sana na Dokta Yusha. Kabali maridadi iliyomtetemesha Sita na kuidondosha bunduki chini.
Dokta Yusha hakujari, alimvuta Sita kwa nyuma kwa nguvu. Mwanzoni Sita alijikomaza lakini baadae Ilibidi ajilegeze, maana kukomaa ilimaanisha kuumizwa zaidi na ile kabali.
Kujilegeza nako lilikuwa kosa kubwa sana alilolifanya Sita. Kosa ambalo atalijutia mpaka kesho, kama kuna maisha baada ya kilichomtokea pale. Dokta Yusha alimvuta Sita kwa nguvu na kujikuta akimsukumia pale katika kiti cha kifo!
Balaa!
Sita alibadirika naye, mwili ulibadirika sambamba na kiti, Ilikuwa ni rangi nyekundu mithili ya tanuru la moto!
'Auae kwa upanga siku zote huuwawa kwa upanga' Iko hivyo, na wahenga walishasema zamani sana. Sita wa Six killers alikufa aina ya kifo sawa na aliyokufa yule askari. Na watu wengine wengi waliouwawa na kiti kile cha kifo! Sasa Dokta Yusha alikuwa huru tena lakini katika jumba hatari sana. Jumba ambalo hakuwa anajua linalindwa na walinzi wangapi, jumba ambalo hakujua ni aina gani ya ulinzi wanaoutimia. Ni mbwa ama binadamu? 'Bora nife kwa bastola, bora nife kishujaa, kuliko kufa kwa njaa!" Dokta Yusha aliiokota ile bunduki iliyokuwa inatumiwa na Sita, SMG ambayo dokta Yusha alikuwa anajua kuitumia. Alifunzwa Kiwira Mbeya, katika Chuo cha Magereza,
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi