Machapisho

BALAA (12)

Zephiline F Ezekiel
Jina: BALAA
Mtunzi: Halfani Sudy

SEHEMU YA KUMI NA MBILI
ILIPOISHIA...
Baada ya maelezo hayo kila mmoja aliingia ndani kupumzika. Six killers walikuwa wamechoka sana. Wote pombe zilikuwa zimewaisha vichwani mwao. Ama hakika Six killers walikuwa wamepatikana, na kupata pigo kubwa sana, baada ya wapiganaji wao wawili kukutana na mkono wa Dokta Yusha! Wakati vijana wanne wa Six killers wakiwa wameenda kupumzika,

JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈

ENDELEA...
Don Genge yeye hakwenda kupumzika kabisa. Yeye ndiye alikuwa mkuu wa misheni hii. Na ilimpasa kupeleka ripoti kwa wakuu wake, na sio ripoti tu, wakuu walikuwa wanataka ripoti nzuri ya kueleweka toka kwa Don Genge. Don Genge atapumzika vipi wakati hakuwa na ripoti ya kueleweka hadi sasa?

Don Genge yeye hakwenda kupumzika kabisa. Yeye ndiye alikuwa mkuu wa misheni hii. Na ilimpasa kupeleka ripoti kwa wakuu wake, na sio ripoti tu, wakuu walikuwa wanataka ripoti nzuri ya kueleweka toka kwa Don Genge. Don Genge atapumzika vipi wakati hakuwa na ripoti ya kueleweka hadi sasa? Pamoja na kupata idadi ya mioyo waliyoagizwa lakini Tano alikuwa mgonjwa, Sita alikuwa kapotea, adui yao namba moja duniani, Dokta Yusha alifanikiwa kuwatoroka. Ni ripoti mbaya zaidi tangu Don Genge apewe kazi hii. Hakika hakupaswa kupumzika, na hakupumzika kweli. Don Genge alienda sebuleni, aliwasha kompyuta yake na kuanza kuikagua, kila kitu kilikuwa sawa. Alifungua kabati kubwa lililopo pale sebuleni, namo kila kitu kilikuwa sawa. Don Genge akajua kwamba Dokta Yusha hakuwa ameingia mle ndani. Alirudi kwenye sofa kubwa lililopo pale sebuleni, alikaa kwa mtindo wa kujitupia sofani. Alianza kuwaza mustakabali wa kisanga kile kilichokuwa kinawaendesha mrama sasa.
*****
Dokta Yusha aliendelea kuufuata ule ufukwe, cha ajabu ule ufukwe uliomfikisha katika kijiji cha Mpara, kijiji ambacho kipo ndani ya Kilwa Masoko. Alipofika hapo kijijini ndipo aligundua kumbe bado yupo ndani ya Kilwa. Porini Mpara Dokta Yusha alichimba shimo refu na kuifukia ile bunduki, huku akiweka alama kwa juu asiisahau sehemu ile. Alivyomaliza akaendelea kutembea na pori. Hakutaka kabisa kupita barabarani akiuhofia usalama wake. Lakini alitoka kule porini na kuikaribia vipori vidogo vilivyokuwa karibu na barabara kuu ya lami.

Alivyogundua kama yupo Mpara, nia na madhumuni yake ni kwenda hospitali ya Kilwa Kivinje kwa miguu! Ilikuwa ni safari ngumu lakini na ndefu lakini ilikuwa ni lazima aende Kilwa Kivinje, alihisi hatari kubwa sana kumuacha mke wake na ndugu zake wengine katika hospitali ya wilaya Kilwa. Dokta Yusha alitembea kwa miguu, ilikuwa safari ngumu sana, lakini hakukuwa na namna nyingine. Ilikuwa ni lazima atembee. Alipofika hospitali ya Kivinje breki yake ya kwanza ilikuwa ni wodi aliyowaacha wakina Nasra. Alipofika mlangoni tu na kuangalia katika kitanda alipokuwa amelazwa mkewe, Nasra. Alipingwa na butwaa! Kitanda cha Nasra kilikuwa tupu. Hakukuwa na mtu. Akiwa kasimama palepale mlangoni chozi la uchungu liligusa sakafu ya hospitali.

Dokta Yusha alikuwa analia. Kutumuona Nasra pale kitandani alijua kuna mawili, kama mkewe kipenzi hajafariki na kuhamishiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti basi kundi lile la wanaharamu itakuwa wamemteka. Lakini Dokta Yusha yote hayo mawili hakutaka kabisa yatokee. Alikuwa anampenda sana Nasra, na alikuwa anatamani sana kumuona Nasra anakuwa na siha njema kama zamani. Dokta Yusha alipiga hatua za taratibu kuingia ndani ya hospitali, huku akifuta machozi kwa kutumia kiganja chake, alikipita kitanda cha mkewe, Nasra akiwa anakiangalia sana, alifika katika kitanda alicholala Hasina, alipofika tu pale kitandani kilitokea kitu cha ajabu sana! Hasina alifungua macho! Dokta Yusha hakuamini alichokuwa anakitazama, ulikuwa ni ukweli ambao hakukubaliana nao.

"Umeamka Hasina, niambie mke wangu Nasra yuko wapi, naomba uniambie hata kama wamemchukua wale washenzi, wewe nambie tu" Dokta Yusha alikuwa anaongea na Hasina lakini ilikuwa ni kama anaongea na sanamu, Hasina alimwangalia tu, bila kusema chochote. Maneno yale ya Dokta Yusha yalimuamsha Mzee Mpaukha toka usingizini. Naye alishangaa sana kumuona Dokta Yusha pale. Kwa sauti dhaifu aliongea. "Ulikuwa wapi Dokta, umeacha watu wanateseka sana hapa, hii sio hospitali kabisa, hapa ni wakala wa kifo!"

Dokta Yusha alimwacha Hasina, alisogea taratibu kuelekea katika kitanda alicholala Mzee Mpaukha huku akiyasikiliza kwa umakini sana maneno akiyoyaongea Mzee yule. Yalimuingia kabisa akilini. "Nimekuelewa mzee wangu" Dokta Yusha aliongea kwa huzuni alipofika pale kitandani. Huku akijificha ili asijulikane kama alikuwa analia. "Katafute gari sasahivi Dokta, katafute gari kama unatujari, utuhamishe katika hospitali hii" "Nasra yupo wapi baba?" Aliuliza. "Nasra yupo ICU" "Tutaondoka vipi sasa baba na mke wangu yupo ICU?" "Ni kwa kudra ya Mwenyezi Mungu, hata huko ICU unafikiri anapewa huduma gani, amelazwa tu kama alivyolazwa hapa! Tuhamishe Dokta hii siyo hospitali!"
******
Don Genge alikaa pale sofani muda mrefu kidogo. Baada ya kutafakari sana akapata wazo kichwani kwake, na akalifanyia kazi wazo lake muda huohuo. Aliitoa simu yake katika mfuko wa suruali yake, akatafuta namba fulani na kuzipiga. "Hallo Dokta Zaidi Kilumba" "Nambie Don wa madon" "Huyu jamaa katoroka huku, lakini kwa vyovyote vile lazima aje hospitali kuviangalia hivyo vikaragosi vyake, weka mtu makini wodini atuambie pindi tu atakapotia mguu wake hapo hospitali" "Sawa Don, natekeleza hilo sasahivi"

Kwa bahati nzuri mtu aliyewekwa na Zaidi Kilumba alifika pale wodini wakati Dokta Yusha akiwa ameenda kutafuta gari kwa ajili ya kuwapakia wagonjwa wake na kuwatoa katika hospitali ile, iliyogeuka kuwa hatari sana sasa, au wakala wa kifo kama alivyoiita Mzee Mpaukha. Baada ya nusu saa Dokta Yusha alirejea, akiwa na gari aina ya Costa kwa ajili ya kuwapakia wagonjwa wake. Dokta Yusha alishuka garini, kwa mwendo wa kasi alielekea wodini. Alitembea kwa kasi kwa kuwa alijua hatari ya kukaa pale hospitali kwa muda mrefu. Uharaka wake lakini haukupunguza umakini wake, Dokta Yusha alikuwa makini pia. Alikuwa anamwangalia kila mtu , ili angalau ajue kama hatari ikiwa inamkaribia. Ghafla! Akiwa njiani Dokta Yusha alishikwa bega na mtu. Alistuka sana. Aligeuka kwa kasi na tahadhari kubwa sana.

Tayari kwa lolote. Alikuwa Mwanasheria mlevi. "Mbona faster Dokta" Mwanasheria aliuliza. "Nataka nihamishe wagonjwa wangu Mwanasheria" "Nimetoroka Polisi kuja kukwambia hiko kitu kaka" "Umetoroka Polisi?" "Hatuna muda wa kuongea hapa, wewe ni hatari zaidi kuonekana hapa, rudi garini nakuletea wagonjwa wako wote garini" "Unajua Nasra alipo Mwanasheria, basi twende wote" "Rudi garini!" Mwanasheria mlevi alisema kwa hasira. Hakuongeza neno, aliondoka kuelekea wodini, akimwacha Dokta Yusha amehemewa. Hakuwa na jinsi, alirejea kwenye gari huku akishangaa akili za Mwanasheria mlevi.

Sasa Dokta Yusha alianza kumhusudu Mwanasheria mlevi. Alianza kumwamini yule mlevi akiyemdharau sana kabla ya kisanga hiki. Mwanasheria mlevi aliingia wodini akiwa anaangaliwa na yule kijana, mlinzi aliyewekwa na kina Don Genge. Moja kwa moja alienda katika kitanda cha Mzee Mpaukha. Aliteta nae kidogo kisha akatoka nje. Mwanasheria mlevi alienda nyuma ya wodi ile, sehemu ambako kulikuwa na choo pia. "Mamaaa nakufaaaaaaa!" Mwanasheria mlevi alipiga makelele yasiyo na mfano kule nyuma ya wodi. Watu walichanganyikiwa. Na baadhi ya watu walikimbilia kule nyuma. Yule kijana aliyewekwa na Dokta Kilumba nae alivutwa na ukelele wa Mwanasheria. Naye alielekea kule nyuma ya wodi.

Wakati yule kijana akikimbilia kwa kupita upande wa mashariki kuelekea nyuma ya wodi, Mwanasheria mlevi alipita upande wa magharibi kurudi mbele ya wodi. Yule kijana umbea ulimponza, watu wengi waliendelea kukusanyika kule nyuma ya wodi bila kuelewa kilitokea nini. Mwanasheria mlevi aliingia wodini harakaharaka, kwa kushirikiana na mzee Mpaukha wakamweka Hasina katika kiti chenye magurudumu manne, na kuanza kuondoka nae kwa kasi kuelekea garini, Mwanasheria mlevi ndiye aliyekuwa akisukuma kiti kile huku akifuatwa kwa nyuma na Mzee Mpaukha, aliyekuwa akifuata kwa mwendo wa taratibu. Walifika ilikopaki ile gari, kwa kushirikiana na Dokta Yusha walimuingiza Hasina garini.

Mwanasheria mlevi alishuka katika gari harakaharaka ili akamchukue na Nasra, mkewe Dokta Yusha. "Unaenda wapi tena Mwanasheria?" "Kumchukua Nasra" "Nishamchukua tayari, ingia kwenye gari tuondoke" "Safi sana comrade" Mwanasheria mlevi alisema huku akimwangalia Nasra aliyekuwa amelala katika siti ndefu za nyuma ya ile gari. Safari ya kukimbia katika hospitali ile ya wilaya, ambayo sasa ilikuwa ni sawa na wakala wa kifo wa wilaya ilianza. Kule nyuma ya wodi watu walitafuta sana bila kumuona mtu aliyepiga kelele. Hawakuona kitu, watu walianza kuondoka kidogokidogo, huku wakionesha kukereka kwa kiasi kikubwa, na yule kijana nae alirejea katika lindo lake.

Kule nyuma ya wodi watu walitafuta sana bila kumuona mtu aliyepiga kelele. Hawakuona kitu, watu walianza kuondoka kidogokidogo, huku wakionesha kukereka kwa kiasi kikubwa, na yule kijana nae alirejea katika lindo lake. Alikaa palepale kwenye kiti akimsubiri Dokta Yusha afike pale, ili awape taarifa mabosi wake waliomtuma. Laiti angejuaaaaa... Alikuwa amechelewa sana. Hakujua kwamba Mwanasheria mlevi alimuona pale muda mwingi sana, na alimtilia shaka yule kijana pale kitini. Ndio akaamua kuucheza ule mchezo wa makelele.

Mchezo uliomuokoa awali Dokta Yusha bila kujua kipindi anaelekea katika chumba cha kuhifadhia maiti alipokuwa amejificha Tano, na sasa mchezo uleule wa makelele unaookoa watu wengi zaidi lakini safari hii ukichezwa kwa kukusudia Don Genge alibaki masikio wazi kusubiri taarifa katika simu yake. Lakini simu haikupigwa. Baada ya kukaa kwa muda mrefu kidogo, Don Genge alinyanyuka pale sofani na kwenda katika chumba wanacholala Six killers, aliwaamsha kwa upole na kuanza kuongea. "Six Killers, mmelala vya kutosha vijana, nina maana yangu kuwaruhusu mje kulala wakati kama ambao hamkupaswa kulala kabisa.

Kuanzia sasa hamtalala tena, mpaka mtakapomleta Dokta Yusha hapa! Kule wodini kuna kijana tumemweka endapo kama Dokta Yusha atawasili atujulishe kupitia kwa Dokta Kilumba. Lakini hadi sasa hakuna taarifa yoyote. Inamaana yule mwanaharamu hajafika pale hospitali. Sasa wote mnaenda wodini kumchukua yule mzee na yule dada na mtaenda kule ICU kumchukua yule mfu. Leo ndio siku yao ya kufa!. Vifo vibaya sana, ambavyo havijawahi kushuhudiwa na Dunia hii. Hakikisheni hamfanyi kosa lolote vijana " "Sawa Bosi"

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi

Chapisha Maoni